Biashara gani inaweza ikafanikiwa ndani ya Same mjini mkoa wa kilimanjaro?

Biashara gani inaweza ikafanikiwa ndani ya Same mjini mkoa wa kilimanjaro?

kevin strootman

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2017
Posts
1,114
Reaction score
1,872
Kama tittle inavyojieleza, ni biashara gani inaweza ikatiki ndani ya wilaya ya same pale same mjini? nafikiria nifungue duka la nguo, duka la vyakula la kawaida au duka la spea za simu.

je, mzunguko wa pesa katika wilaya hii ukoje? au ni biashara gani ya mtaji mdogo ambayo inaweza ikatiki kwa wenyeji wa hapo?

kama kuna mwenyeji wa same au mwenye experience na biashara anipe muongozo.
 
Same labda biashara ya Vinyago tu 😄😄😄 maana kukaribishwa tu kuna sanamu ya Faru Rajabu
 
Same naifahamu.

We kuwa na duka ambalo lina kila kitu.

Kuanzia vyakula.
Nguo.
Mpaka mabati, misumari, viatu.

Yani kila kitu.

Ila hujasema tu mtaji wako.

Mira nawe ni mpare kana u Shuve ya nyika?
hahaa ni ihangajiko ilo
 
Mkuu unatakiwa kusoma Mazingira mwenyewe ili kuona unaweka nini kulingana na unavyo yaona mazingira.

Same nimekaa kwa muda naijua fika.

Ila mambo yamebadilika sana so lazima Uangalie kuna Changamoto gani pale na zibadili kuwa furusa.

Usiingie tu kichwa kichwa na pia kikubwa unatakiwa kufanya kile unacho penda
 
Same naifahamu.
We kuwa na duka ambalo lina kila kitu.
Kuanzia vyakula.
Nguo.
Mpaka mabati, misumari, viatu.
Yani kila kitu.
Ila hujasema tu mtaji wako.
Mira nawe ni mpare kana u Shuve ya nyika?
Mimi ni mpare ndio, mtaji wangu ni mdogo sana, nataka kuanzia chini
 
Back
Top Bottom