Biashara gani nikiwa bado nasoma?

Majigo

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
5,519
Reaction score
1,828
toka DAR,
Salam kwenu wakuu
Ni kwamba hivi karibuni natarajia kuanza masomo ktk chuo flan hapa mjini....

mbali na Ada, nina Shiling LAKI 8 hivi kama mtaji wa biashara,

sasa wakuu naomba mnishauri kitu/biashara gani naweza fanya ambayo haitanibana ukizingatia sina kazi na nategemea kuizungusha hii hela ili niweze kuendesha maisha nikiwa chuo bila kuathiri masomo yangu
MDA CHUONI NI MASAA MATANO ,TUNAINGIA SAA 6 MCHANA KUTOKA SAA 11 JIONI
NB:Tafadhari!! Kama huna ushauri kuwa msomaji tu!!!

AHSANTEN!!
 
Safi sana hyo na ukitaka laundry machine.....please check me out there!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
unaweza pia ukaanzisha biashara ya kuuza vitu mbalimbali chuoni kama saa, nguo, viatu, wallet na manukato.
unatafuta kijana anakuzingushia chuoni au kama utaweza unafanya Mwenyewe
 
Safi sana hyo na ukitaka laundry machine.....please check me out there!


Sent from my iPhone using JamiiForums

mkuu samahani ,nilitoka kidogo siioni post ya loundry
hiyo biashara inakuwaje, na inahitaj vifaa gani?
Ahsante sana
 
unaweza pia ukaanzisha biashara ya kuuza vitu mbalimbali chuoni kama saa, nguo, viatu, wallet na manukato.
unatafuta kijana anakuzingushia chuoni au kama utaweza unafanya Mwenyewe

mkuu nitazingatia ushauri wako
kutokana na mazingira ya chuo (wasichana ni robo tatu ya wanafunzi) , hiyo ya manukato, pedi na vyupi
nimeipenda
mkuu hapa ni kuzungusha mwenyewe mwanzo mwisho ni kukatia mbali mshipa wa aibu!
Ahsante kiongozi
 
wakuu chuo kipo DAR
 
M-pesa itakufaa. Unaweza pia kuajiri kijana kukuzungushia matunda yaliyokatwakatwa na kuwekwa kwenye containers nzuri.
 
mkuu hiyo biashara unauzoefu nayo
plz nisaidie namna gani naweza isimamia

Hiyo biashara ngumu kupata faida kama husimamii mwenyewe. Kwakuwa wewe utakua busy unampa mtaji kijana, kwa siku anakupa kiwango unacho ona kitaleta faida ndani ya muda flani.. Eg, unalipia frem, nakununua mambo yote yanayohitajika kwa siku ya kwanza, then after two days of studying the situation, unakuwa ushajua umtoze sh. ngapi kwa siku msimamizi wako.
 
kwa mtaji huo hakikisha, unaazsha biashara ya vocha, pipi na vitu vidogo vidogo wanavyopenda wanafunzi utapata faida balaa, na hata kama huna kipindi asubuhi wewe njoo ujisomee hapo chuoni na hakikisha unavaa apron za kampuni za simu ili wenzio wakufahamu, tena usibakishe pesa wewe nunua vocha za kutosha utapata faida mpaka unaweza acha chuo kama fedha inakuchanganya.

ukifanikiwa urejeshe feedback please!



mkuu hiyo biashara unauzoefu nayo
plz nisaidie namna gani naweza isimamia
 
mkuu hiyo biashara unauzoefu nayo
plz nisaidie namna gani naweza isimamia

Kwahiyo kijana anakulipa kiasi fulani kwa siku, anajipatia chake pia as long as working capital iko pale pale..
 
duka la vipodozi umefunga tena?
 
M-pesa itakufaa. Unaweza pia kuajiri kijana kukuzungushia matunda yaliyokatwakatwa na kuwekwa kwenye containers nzuri.

mkuu umenifungua akili
nikifanikiwa kupataa oda za watu wa maofisini inaweza kunilipa hii
ahsante sana kiongozi ushauri wako nitaufanyia kazi
 

hapo nimekusoma mkuu
niko naandika hapa ili nichanganue vizur
 
ndio mkuu
nipo chuo cha bandari hapa
Great! Mi enzi hizo za chuo ni kununua majeans na raba nyeupe tu. Najutia kipindi changu kile why sikuamka mapema ningekuwa mbali sana. Komaa na hizo nguo za kike (only) zitakutoa kwa mtaji huo. Ungekuwa na kama 2M ningekushauri utafute kasehemu hapo chuo uuze viepe yaani watoto wa chuo huwaambii kwenye hio kitu. Nimekaa Mabibo hostel (2005-2008) yaani kulikuwa na wagogo std 7 wanauza viepe pale wanapiga hela ndefu hadi dada zetu wakusoma wanashoboka....
 

sawa mkuu ni biashara lkn unaelewa retrn ya hiyo biashara?
Vocha ya elfu 5 faida 200
 
Kwahiyo kijana anakulipa kiasi fulani kwa siku, anajipatia chake pia as long as working capital iko pale pale..

unamaanisha kama biashara ya bodaboda vile yaani kama ni elfu 10 , ni kila siku ...haijalishi mauzo duni au yako over?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…