Biashara gani unayoweza fanya yenye uwezo wa kuingiza milion 300 kwa mwaka kwa kutumia mtaji wa bilion 1?

Je, ni biashara gani unayo weza fanya yenye uwezo wa kuingiza milion 300 kwa mwaka kwa kutumia mtaji wa bilion 1?
Dawa za hospitali za binadamu.

Tatufa kanda yako katika nchi hii, ambako ushindani sio mkubwa sana. Fungua Pharmacy, uza kwa jumla, wasambazie wenye maduka ya dawa, vi-discount vya hapa na pale.

Ikiwezekana unafungua na maduka ya dawa baridi za binadamu katika maeneo yenye tija, unakuwa unajisambazia.
 
Nunua shamba la heka 20
Zungusha uzio
Chimba kisima
Jenga mabanda
Fuga nguruwe wa kisasa
Ni kama broiler
Jenga kijumba cha vyumba kadhaa
Kwaajili ya wafanyakazi kadhaa
Watakaoishi hapo shamba
Nguruwe wa kisasa hukuwa haraka na wana soko pia kuanzia mbegu mpaka kwa wachinjaji
Panda mazao hapo shambani kwaajili ya chakula cha nguruwe na kingine utakuwa unanunua
Nunua nguruwe ambao wamefikia kupandwa
Ukianza na nguruwe 100 siyo mbaya

Ambao kila nguruwe unaweza kununua kwa milioni na nusu
mpaka milioni mbili

Nguruwe anakaa na mimba miezi minne kasoro
Nguruwe mmoja anaweza kuzaa watoto zaidi ya kumi
Kwa hiyo before mwaka kuisha utakuwa na nguruwe zaidi ya elfu1
Unaweza kuuza mbegu yani wakiwa bado wadogo kama miezi 3 hivi wakimaliza kunyonya unawaweka sokoni
Wa kisasa wanakuwa haraka hawali sana
Wakienyeji wanakula sana na wanakuwa kidogo
Nguruwe wa kisasa wa miezi mitatu ni kama wa miezi sita kienyeji kwahiyo kienyeji ni hasara
Nguruwe wa miezi mitatu unaweza kumuuza hata laki nne na kuendelea
Nguruwe wa kufaa kula ni kuanzia miezi6 na kuendelea
Pia katika wafanyakazi wako ajiri mtaalamu/daktari wa kilimo/ ufugaji
Awe ndiyo kiongozi wa hawa wafanyakazi wengine utakao kuwa nao ili mambo yaende vizuri
Unaweza kutumia nusu au chini ya nusu ya hiyo hela kwenye hizo vurugu zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…