Biashara hii kutoka mbeya kuja dodoma ikoje?

milionea wa kesho

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2015
Posts
328
Reaction score
631
Wakubwa nafikiria kuanza biashara ya mazao kutoka mbeya kuja dodoma. Nawaza nianze na mchele, maharagwe na viazi vya chipsi.

naomba summary ya bei za mazao hayo kwa mikoa ya mbeya na dodoma na pia changamoto zake zikoje.

Natarajia kuanza na mtaji wa 2M.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikondo ni iringa naisi... wafanya biashara wakubwa wa viazi mbeya huwa wanajumua uko

Sent using Jamii Forums mobile app
Kikondo sio iringa ni mbeya vijijini karibu na mbuga za kitulo nilishawahi kufika huko usafiri ni changamoto Sana bora uchukue sehemu inaitwa tokela IPO wilaya ya rungwe, lakn ujue hyo 2m inatosha nauli pekee kutoka Mby mpk dom
 
Kikondo sio iringa ni mbeya vijijini karibu na mbuga za kitulo nilishawahi kufika huko usafiri ni changamoto Sana bora uchukue sehemu inaitwa tokela IPO wilaya ya rungwe, lakn ujue hyo 2m inatosha nauli pekee kutoka Mby mpk dom
Mkuu kweli viazi vingi vinapatikana bara bara ya Tukuyu na hasa hapo Ntokela ila mtaji unasema wa mazao Million mbili haitoshi hata akianza kwa kuchukua gunia chache akapakia kwa maroli tupu yanayotoka Malawi mpaka Iringa na Iringa akaunga lingine mpaka Dodoma haitawezekana au kuchanganya mzigo kwa wafanyabiashara wengine wanaopeleka Dodoma...
 
Ntokela na sio Tokela

Usafir ni changamoto kiaje?

Na Mara ya mwisho kufika kitulo ni lini mkuu.

Kikondo sio iringa ni mbeya vijijini karibu na mbuga za kitulo nilishawahi kufika huko usafiri ni changamoto Sana bora uchukue sehemu inaitwa tokela IPO wilaya ya rungwe, lakn ujue hyo 2m inatosha nauli pekee kutoka Mby mpk dom
 
maybe kwa ushauri huu anaweza akajaribu
 
Hivyo viazi vinavyopatikana kikondo kwa sehem kubwa vinatoka mashambani maeneo ya matamba,kinyika,mwambwalo,mpangala, ila kama ataweza aende mashamban kabisa akipata mzigo afaulishie pale chimara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anamkatisha tamaa tu. Gunia moja huko ntokela ni elfu 15. Hivyo anaweza nunua viazi vya 1.5m na hiyo 500k akatumia kwa usafiri huu wa kuunga kwa gari za transit zikiwa zinarudi.

Bei ya kuuzia gunia moja kwa haraka ni 45-50k. Akijipanga soon anatoboa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikondo ipo wilaya ya Mbeya vijijini jirani na kata ya ilungu. Unaweza kuchukua viaz Kikondo au wilaya ya Ilungu yaani vijiji vya Ifupa, Mashese, Ngole n.k. Usafiri si lazima upite njia ya Isyonje bali unaweza pitia Wilaya ya Mbarali kijiji cha Mswiswi kuna Barabara ya Vumbi nzuri tu ya kwenda huko kote shida ni milima tu.
 
Kwenye biashara mtu muhimu sana ni mnunuzi..,mkuu nafikiri anza kwanza sokoni ukiwa na uhakika na soko waweza maliza changamoto nyingi zikiwemo za usafiri au mtaji mdgo kwa maana kupewa kiazi uuze ndo uje ulipe(mali kauli) na kama mbeya ni mbali pia Njombe kuna viazi vingi sana na barabara nzuri waweza enda huko cha msingi Dodoma kuwe na uhitaji mkubwa wa kiazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…