n00b
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 1,015
- 2,680
Watu wengi hujikuta wakiwa wanahangaika wataanzaje biashara bila kuwa na kiasi kikubwa cha pesa. Wakati huohuo, wengine wana pesa lakini hawana ujuzi wa msingi wa kuweza kupata zaidi ya kiasi walicho nacho.
Baadhi ya nilizoorodhesha hapa chini, ni biashara ambazo zinahitaji msingi (pesa) kidogo au hata bila pesa zinaweza kuanza kukuingizia kipato. Naamini wengine mnaweza kuongezea:
Natambua kuna watu waliosomea fani mbalimbali, tusaidiane kuwaelimisha wengine juu ya kutumia elimu zao bila kutegemea kipato kikubwa lakini baadae wakanufaika na elimu zao bila kusubiri kuajiriwa na serikali ama makampuni makubwa.
Baadhi ya nilizoorodhesha hapa chini, ni biashara ambazo zinahitaji msingi (pesa) kidogo au hata bila pesa zinaweza kuanza kukuingizia kipato. Naamini wengine mnaweza kuongezea:
- Kuosha magari (Car Wash)
- Blogging
- Urembaji wa keki (Cake decorating)
- Utengenezaji mishumaa
- Mama Ntilie (Catering)
- Kutembeza vyakula maofisini (Mobile food vendor)
- Kazi ya usafi maofisini (kama mkiwa mmejikusanya kama kikundi)
- Computer troubleshooting (kwa graduates wa IT, Computer technicians)
- Event coordinator
- Kutumbuiza kwenye matukio kama DJ (Event DJing)
- Exercise/Sports instructor (wengi wanahitaji huduma hii)
- Utengenezaji wa fenicha
- Utunzaji wa bustani (Gardening, Landscaping etc)
- Usafishaji wa nyumba mtaani (House cleaning)
- Interior decorating (naona wengine hadi wanajiita 'interior designers')
- Kusaidia watu kubeba mizigo wakitoka kwenye manunuzi (Personal shopping assistant)
- Uuzaji wa nafaka/mazao toka kwa wakulima mikoani (wanahitaji kiunganishi na wateja wa mijini)
- Usahihishaji wa lugha/maandishi kwenye ofisi mbalimbali pamoja na vyombo vya habari (Proofreading)
- Kuwa MC kwenye matukio mbalimbali (Unatakiwa kusoma vitabu vya Public speaking zaidi)
- Kutengeneza sabuni (Soap making)
- Kufundisha (Teaching); hapa namaanisha kila mtu ana kitu anafahamu ambacho anaweza kuwa mwalimu mzuri
- Website design (kama ulisomea mambo ya graphics n.k)
- Software developer (kama umesomea software engineering n.k)
- Wedding planner/Event Cordinator
Natambua kuna watu waliosomea fani mbalimbali, tusaidiane kuwaelimisha wengine juu ya kutumia elimu zao bila kutegemea kipato kikubwa lakini baadae wakanufaika na elimu zao bila kusubiri kuajiriwa na serikali ama makampuni makubwa.
Watu wengi huko mtaani nikiwaulizaga ni kwanini yeye ni maskini ananiambia kwamba kama agepata milioni 150 angeanzisha biashara ya maana. Lakini utamkuta amekaa sehemu hiyo hiyo moja kila siku mchana kutwa akilalamikia serikali kwa nini haimpi ajira. Ajui kwamba ajira sio serikalini tu. Serikali ina ajira zake. Serikali inaajiri asilimia ndogo sana ya positions zake na ajira zinazobaki zinapatikana kwenye sekta binafsi ambayo ni makampuni binafsi na kujiajiri.
Ieleweke kwamba hata matajiri wemhi duniani walianza na mitaji midogo sana, muulize Mengi na Bakhresa watakuambia. Inachotakiwa ni kujiamini na kujibana ili uukuze mtaji na pia tujifunze kuacha kufikiria watu wengine watatufikiriaje tukianza na mitaji modogo. Kuwa na mafanikio ni tofauti na kuwa tajiri, so unaweza ukaanza na mtaji mdogo kabisa na kuukuza ukawa tajiri kabisa. Siku hizi kila biashara inalipa na sio lazima uwe umepitia chuo kikuu kufanikiwa kimaisha. Waulize matajiri wa mabasi watakuambia.
Ukichagua idea moja kati ya hizo alizoorothesha huyo jamaa hapo juu ukaweka effort na kuacha kuangalia ishu za watu wengine na kufanya biashara yako na kujibana, then mtaji wako utakuwa na pia kuacha kufikiria kuwa tajiri fasta, kwasababu eventually utakuwa tajiri baada ya muda flani kama ukijituma sana. Kama wengine wamekuwa na mafanikio kwa nini nawe usiwe?
Kuna njia kadhaa za kutafuta mtaji wa kuanzia biashara:
1. Kupitia kukopa kwa ndugu, rafiki na jamaa
2. Kukopa benki (ambapo kwasasa ktk nchi yetu mfumo wake si mzuri sana, ila ukiishaianzisha wanaweza kukupa maana mabenki wanatoa mikopo kwa biashara zilizoanza tayari)
3. Kama tayari biashara yako imeshaanza, unaweza uza hisa watu watoe hela ili wawe na asilimia flani za umiliki
4. Anza na biashara zisizohitaji mitaji kabisa
Jinsi ya kuanzisha biashara yenye mafanikio:
Mimi nasomea biashara na tunafundishwa kwamba kuna aina mbalimbali za mifumo ya biasha, aidha uanzishe mwenyewe au na partner n.k. Sasa tunaambiwa kwamba ukianzisha na partner unakuwa na mafanikio zaidi kuliko ukianzisha mwenyewe, mfano makampuni yotemakubwa duniani wameanzisha ma partners: google, microsoft, oracle, apple, n.k. Faida ya upartner ni kuchangia ujuzi na resources. Mfano wewe una elimu flani mwenzako ana hela, au yeye ana ujuzi wewe una connections na watu flani flani. Pia partnerships tax zake si kubwa. Sema partners lazima muwe mnaaminiana sana hata kama mko wengi.
Ideas zisizohitaji pesa nyingi:
1. kinyozi
2. kuuza matofali (veta wana mashine za kufyatulia matofali za bei rahisi kabisa)
3. Kibanda cha chipsi, ice cream, vocha, n.k
4. Duka dogo la reja reja
Anza kidogo then unakua baada ya muda flani. Usiogope kuanza na mtaji mdogo, maana ndo matajiri walianza hivyo na baada ya biashara zao kukua kidogo, ndo wanatokea watu wanawekeza kwenye biashara yako.
Siri nyingine ni kwamba kama utaamua kuandikia biashara yako kuwa kampuni, ukienda brela kuna aina kadhaa za makampuni mfano sole propriatorship (uliyoianzisha wewe mwenyewe), partnerships n.k. Hakunaga investor anayewekeza kwenye sole proprietoship. Ndo maana hata benki hawatoi mikopo kwenye vibiashara vya mtu mmoja mmoja kwasababu sole proprietorships (kampuni iliyoanzishwa na mtu mmoja mmoja) hairusiwi kuuza shares. So anzisha na partner ili muda wowote kama mnata kuongeza capital yenu mtu yeyote anajiunga nanyi na kwekeza kiasi cha pesa.
Ntakupa mfano wa facebook.
Mark zakabegi alipokuwa anaanzisha facebook alikuwa na ujuzi wa programming tu, hana hela wala nini. Ikabidi aanzishe partnership na rafiki zake eduardo na mwingine. Eduardo aliwekeza 15,000 dollars ndo ikafanya hata wawe na ofisi badala ya bwenini walikoianzishia facebook. So kampuni yao ikawa partnership. Baada ya muda kampuni ikawa imekua ndo akatokea jamaa mmoja akawekeza 500,000 dollar akapewa asilimia kadhaa ya shares na ndo hapo facebook ilipopaa kimafanikio. So usiogope kuanza na partner.
Cheers