Ngoja nikufafanulie kwa mfano,
Pamoja kwamba mimi niko kwa Mhindi, lakini nafuga, nina wale kuku wenye viguu vifupi lakini wanataga mayai mengi sana ya kienyeji na wewe unataka kuanza kufuga kuku wa kienyeji kwa ajili ya mayai. Mimi nitakupeleka shambani/bandani kwangu, nitakuonyesha namna ya kuku huyu anavyotunzwa, namna ya kuweka kiota cha kutagia mayai, nitakuonyesha namna ya kutumia madawa ya kienyeji nk Sitakuchaji kitu, kisha tunaagana.
Sasa kama unamaanisha na somo limekuingia, step itakayofuata ni utekelezaji kwako,hapa ndipo mimi ninapoanza kupata malipo yangu kwa haki kwa bei halali, ama utataka nikuuzie mbegu ya kuku wale ambao hawapatikani sasa hivi au utasema nikutafutie. Wanafunzi wengine wenye nguvu nawaelekeza walipo hawa kuku wakafuate wenyewe, lakini wanaporudi kutoka huko wanabeba na kuku wangu, kumbuka wengi huwa waungwana hawanichaji gharama za usafirishaji, kwa hiyo hawa wanafunzi wangu wenye nguvu kidogo nawajulisha kuwa mzigo wenu umefika, wanakuja wanalipia mzigo ( cash au wanakopa). Mzunguko huu unaendelea na unapanuka. Siku nyingine naletewa mzigo bure kabisa kama asante kwa elimu.
Hata usiku huu kuna mwanafunzi wangu mwingine anasaidia wengine na mimi ananisaidia kupunguza gharama za project.
Kupitia maelezo haya umefanikiwa kupata kitu?