Biashara hizi zaweza kuanzishwa bila kuwa na mtaji (pesa) mkubwa au bila mtaji kabisa

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
1,015
Reaction score
2,680
Watu wengi hujikuta wakiwa wanahangaika wataanzaje biashara bila kuwa na kiasi kikubwa cha pesa. Wakati huohuo, wengine wana pesa lakini hawana ujuzi wa msingi wa kuweza kupata zaidi ya kiasi walicho nacho.

Baadhi ya nilizoorodhesha hapa chini, ni biashara ambazo zinahitaji msingi (pesa) kidogo au hata bila pesa zinaweza kuanza kukuingizia kipato. Naamini wengine mnaweza kuongezea:

  1. Kuosha magari (Car Wash)
  2. Blogging
  3. Urembaji wa keki (Cake decorating)
  4. Utengenezaji mishumaa
  5. Mama Ntilie (Catering)
  6. Kutembeza vyakula maofisini (Mobile food vendor)
  7. Kazi ya usafi maofisini (kama mkiwa mmejikusanya kama kikundi)
  8. Computer troubleshooting (kwa graduates wa IT, Computer technicians)
  9. Event coordinator
  10. Kutumbuiza kwenye matukio kama DJ (Event DJing)
  11. Exercise/Sports instructor (wengi wanahitaji huduma hii)
  12. Utengenezaji wa fenicha
  13. Utunzaji wa bustani (Gardening, Landscaping etc)
  14. Usafishaji wa nyumba mtaani (House cleaning)
  15. Interior decorating (naona wengine hadi wanajiita 'interior designers')
  16. Kusaidia watu kubeba mizigo wakitoka kwenye manunuzi (Personal shopping assistant)
  17. Uuzaji wa nafaka/mazao toka kwa wakulima mikoani (wanahitaji kiunganishi na wateja wa mijini)
  18. Usahihishaji wa lugha/maandishi kwenye ofisi mbalimbali pamoja na vyombo vya habari (Proofreading)
  19. Kuwa MC kwenye matukio mbalimbali (Unatakiwa kusoma vitabu vya Public speaking zaidi)
  20. Kutengeneza sabuni (Soap making)
  21. Kufundisha (Teaching); hapa namaanisha kila mtu ana kitu anafahamu ambacho anaweza kuwa mwalimu mzuri
  22. Website design (kama ulisomea mambo ya graphics n.k)
  23. Software developer (kama umesomea software engineering n.k)
  24. Wedding planner/Event Cordinator

Natambua kuna watu waliosomea fani mbalimbali, tusaidiane kuwaelimisha wengine juu ya kutumia elimu zao bila kutegemea kipato kikubwa lakini baadae wakanufaika na elimu zao bila kusubiri kuajiriwa na serikali ama makampuni makubwa.

Bado mtaji unahitajika. Wazo lenyewe ni mtaji tosha achilia mbali eneo na soko
 
Kwenye Catering ni balaa inabidi uwe na msingi wa kutosha labda kuosha magari ndio unahitaji ndoo ya buku na maji ya sh 500 kuosha gari zima.......Thou kuna ideas nzuri sana umetoa za bizna.
 
Kwenye Catering ni balaa inabidi uwe na msingi wa kutosha labda kuosha magari ndio unahitaji ndoo ya buku na maji ya sh 500 kuosha gari zima.......Thou kuna ideas nzuri sana umetoa za bizna.

Pia ukitaka kufanya Car wash ya kisasa inabidi uwe na mtaji mkubwa, kuosha magari kwa ndoo ni kupoteza muda.
 
Labda huelewi MTAJI ni nini.

Huwezi kuwa seremala kama huna ujuzi wa fani hiyo, na huwezi kufanya proofreading kama hukusoma. Kweli zipo fani zisizohitaji mamilioni lkn bado zina changamoto zake.
 
kweli kabisa biashara ni utayari wa mtu na jinsi gani amejitoa kufanya kazi hiyo.
 
kweli kabisa biashara ni utayari wa mtu na jinsi gani amejitoa kufanya kazi hiyo.

Mkuu kweli inabidi mtu uwe tayari kufanya kazi hiyo, hebu angalia hii biashara mpya inayochipukia kwa kasi mijini; Niliona bango moja pale maili moja Kibaha limeandikwa hivi, " kuuliza njia ni Tsh 500/ na kupelekwa Tsh 1000/". Sijashangaa nikaona bango kama hilo tena pale Sinza. Nikawauliza vijana wa mjini, wakasema hiyo sasa hivi ni kazi rasmi, mpoooooh
 
Kufundisha ni moja ya kipengele ambayo inaongoza kwa kutohitaji mtaji kabisa ama kidogo sana. Ila ni vizuri katika kitengo chochote unacho ona upo fiti ukakiboresha kwa kujisomea ama kufanya practices tegemeana na nature ya huo ujuzi wako.
 
Kazi ya usafi maofisini (kama mkiwa mmejikusanya kama kikundi)

huitaji mtaji wala watu wengi, if you got the deal unaweza ajiri watu for day payment
 
Kufundisha ni moja ya kipengele ambayo inaongoza kwa kutohitaji mtaji kabisa ama kidogo sana. Ila ni vizuri katika kitengo chochote unacho ona upo fiti ukakiboresha kwa kujisomea ama kufanya practices tegemeana na nature ya huo ujuzi wako.

Kuna wakati nilipata kazi ya kumfundisha mtoto wa jirani yangu mambo fulani, nilikuwa napata malipo zaidi ya ujira wa Mhindi wangu, mwisho kale kadarasa kakapanuka sana, almanusra niache kibarua kwa Mhindi.
 
Hapo ndipo udhaifu wetu upo kwa weengi.... 'UTHUBUTU!' Malila hebu fikiria, darasa lilipanuka hadi likazidi pato la ujira lakini bado uliogopa kuendeleza kwa kuboresha na ku invest katika hicho chanzo chako cha pesa nzuri kwa woga wa kushindwa. Tunataka 'saftey' ya kutokuwa na risks na gurantee ya pesa ya mshahara tukisahau kuwa wakati wowote hiyo kazi inaweza kuisha na tukasahau kuwa biashara yako yaweza fika mbali saana na hata kupelekea wewe kuajiri pia...

Kwa hiyo Malila uliacha kufudisha?
 
Sijaacha kufundisha na sitaacha, ila nilibadili mbinu ya ufundishaji. Sigawi samaki ila nafundisha kuvua samaki. Narudia tena kwa msisitizo, kufundisha kunalipa mara kumi zaidi ya mshahara wa Mhindi wangu. Darasa langu ni kubwa sana na linakuwa kila siku, sihitaji matangazo.

Kama unaweza kufundisha, fanya hii kazi,itakulipa.
 
Malila kama hutajali toa mwongozo unaokuwezesha ili wengi tuweze kunufaika... BTW naomba kujua unadhani kuna uwezekano kuwa hio kazi kwa mhindi ipo hati hati ya kuweza iacha sababu ya hii kazi yako ulioanza kama mzaha?
 
ashaDii Wewe nawe unao ujuzi wako mzuri kama mwandishi,mtangazaji,au mpelelezi. Unaongoe maneno laini yanayoweza kumtoa nyoka pangoni.
 
ashaDii Wewe nawe unao ujuzi wako mzuri kama mwandishi,mtangazaji,au mpelelezi. Unaongoe maneno laini yanayoweza kumtoa nyoka pangoni.

ha ha ha! Umenifurahisha saana... Basi nitaboresha ujuzi namie nifundishe. Lol, I am humbled.
 
ha ha ha! Umenifurahisha saana... Basi nitaboresha ujuzi namie nifundishe. Lol, I am humbled.

umeonaee? Haya endeleeni kumwaga data watu tumechoka na huu mkosi wa umaskini.malila mie na mwaminia sana hata mie ni mwanafunzi wake japo sina uhakika kama darasa analonifundisha ndilo analowafundisha wengine.
 
Mbona sasa unamwaga unamwaga mchele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…