ha ha ha! Umenifurahisha saana... Basi nitaboresha ujuzi namie nifundishe. Lol, I am humbled.
udalali mtaji mdomo na ujanja kujuana na watu.
Malila kama hutajali toa mwongozo unaokuwezesha ili wengi tuweze kunufaika... BTW naomba kujua unadhani kuna uwezekano kuwa hio kazi kwa mhindi ipo hati hati ya kuweza iacha sababu ya hii kazi yako ulioanza kama mzaha?
Nitachangia kidogo,
Niliiangalia jamii inayonizunguka nikagundua mahitaji muhimu kwa jamii yangu, na nikaona mimi naweza kutoa majibu ya mahitaji haya. Jamii yangu ilipungukiwa mtu anayemaanisha, Nikasimama nikawaambia marafiki zangu kuwa tufanye hivi ili na sisi tujikomboe na hili tatizo la kiuchumi. Nilianza na watu wa kawaida aka wakeshahoi, waliponielewa, mimi nikapanda daraja na wao wakasogea mbele, kwa hiyo wote tukasogea. Mimi nilitoa mafundisho bure, kwa moyo halafu bila kuwapotezea muda wao kwa longo longo nyingi na tulikubaliana kuwa tufanye kwa vitendo zaidi.
Ili nifanikiwe sikutaka kutumia matatizo ya jamii kujinufaisha,nilitaka wote tufanikiwe. Ni dhambi kuficha maarifa uliyonayo kwa sababu kanuni ya Mungu ni kwamba, toa kwanza ili upokee zaidi. Natumia lugha rahisi sana kufundisha ili kila mtu aweze kunielewa,sifundishi kitu ambacho mimi sijafanya. Sipendi kumilikiwa na daraja fulani la jamii, mimi ni wa watu wote.
Ngoja nirudi kwa mhindi wangu, tutaonana baadae.
Asante Malila kwa haya maelezo... Ingawa nimeshindwa kukupata. Naomba tuwe realistic kidogo. Katika jamii ya leo ni wachache ambao wanaweza tumia mda wao mwingi kwa kitu ambacho akiwaingizii pato lolote.
Ulizungumza katika post ya awali kuwa inakuingizia pato kubwa na kuna faida zaidi, hii post naona unazungumza kana kwamba hio service unayotowa ni buree kabisa. Naomba kuelewesha mana umeniacha njia panda.
Nilivyouliza namna na njia ulizotumia nikajua hapa sasa napata muongozo wa toka ulipo anza hadi ulipofika, ikiwezekana na kukua kwa pato kwa asilimia. Take note; hapa walengwa sana ni wale ambao maisha ni magumu, hawana kipato na saa ingine hawana hope ya kuweza fanya lolote ili kuhimili maisha yao kwa chochote watacho pata.
una kitu flani ila bado sijajua ni nini!!..sijui niseme ni mwalimu sijui mwanasaikolojia sijui mwezeshaji i dont real know...point yangu ya msingi una kitu flan,jifanyie study then uimalishe hicho kitu..
Ivi umeshawai kuandika chochote may be kitabu au article ukaitoa sehemu??
Ngoja nikufafanulie kwa mfano,
Pamoja kwamba mimi niko kwa Mhindi, lakini nafuga, nina wale kuku wenye viguu vifupi lakini wanataga mayai mengi sana ya kienyeji na wewe unataka kuanza kufuga kuku wa kienyeji kwa ajili ya mayai. Mimi nitakupeleka shambani/bandani kwangu, nitakuonyesha namna ya kuku huyu anavyotunzwa, namna ya kuweka kiota cha kutagia mayai, nitakuonyesha namna ya kutumia madawa ya kienyeji nk Sitakuchaji kitu, kisha tunaagana.
Sasa kama unamaanisha na somo limekuingia, step itakayofuata ni utekelezaji kwako,hapa ndipo mimi ninapoanza kupata malipo yangu kwa haki kwa bei halali, ama utataka nikuuzie mbegu ya kuku wale ambao hawapatikani sasa hivi au utasema nikutafutie. Wanafunzi wengine wenye nguvu nawaelekeza walipo hawa kuku wakafuate wenyewe, lakini wanaporudi kutoka huko wanabeba na kuku wangu, kumbuka wengi huwa waungwana hawanichaji gharama za usafirishaji, kwa hiyo hawa wanafunzi wangu wenye nguvu kidogo nawajulisha kuwa mzigo wenu umefika, wanakuja wanalipia mzigo ( cash au wanakopa). Mzunguko huu unaendelea na unapanuka. Siku nyingine naletewa mzigo bure kabisa kama asante kwa elimu.
Hata usiku huu kuna mwanafunzi wangu mwingine anasaidia wengine na mimi ananisaidia kupunguza gharama za project.
Kupitia maelezo haya umefanikiwa kupata kitu?
Baby steps Malila… Baby steps.
Nakupata taratiibu… Naomba nikiri kuwa umenichanganya kabisaaaa! Umenifanya nianze tena kusoma post zangu. Nikajisemea rohoni huyu Malila anajua kuwa amehama hoja? Awali tulikuwa tukizungumzia ‘Ualimu' tena basi ulisema toka mapema kuna mtoto wa jirani ulianza nae; usingetaja kuwa ni mtoto moja kwa moja kwa maelezo ya post hii ningechukulia kuwa ndio elimu ulikuwa ukitoa kwa watu wazima.
Hata hivyo nishukuru kwa hii taarifa ya ufugaji… Naona nijiwekee taratibu ya kuweza hili maana ninavyo amini mimi nitachinja kuku woote wataisha tu! Hahaha
Ufugaji siwezi, hasa wa kuku. Ila Inshaallah, Mwenye Mungu akiniwezesha nataka nijiingize katika kilimo na kama ufugaji labda wa ng'ombe.
Asante kwa darasa… Kwa maelezo haya nimefanikiwa kupata kitu. Pamoja Saana.
Ualimu uko aina nyingi sana, huyu mtoto nilikuwa namfundisha hesabu, akaita marafiki zake,wakati huo nilikuwa bado sina majukumu, wale watoto walifanya vizuri ktk masomo yao. Mzazi mmoja aliniita na kuniambia kuwa naweza kuwa mwalimu mzuri, hakuishia hapo tu, alinipa kitu kizuri sana. Nimejikuta naendeleza tabia ya kufundisha ktk maeneo mengi yanayonizunguka na inanilipa vizuri.
Mwanzoni nilikwambia kuwa mimi nafundisha kuvua samaki sio kugawa samaki, kwa hiyo darasa ninalotumia ni lazima liwe na nyenzo halisi halafu liwe langu mwenyewe. Hata leo kama ningerudi shule ningesomea Ualimu ili iwe taalumu yangu rasmi.
Safi saana inapendeza... Wanasema 'Knowledge is power' hujafikiria kusomea ualimu hata kwa njia ya 'Open University?' inaweza kuwa ya tija na manufaa huko mbele.
All in all inaonekana mwenzetu unajua nini unataka, nini ufanye na wapi unaelekea. Which is really good na ni wachache wenye bahati ya kuwa nayo. Kila la Kheri...
Kazi ya usafi maofisini (kama mkiwa mmejikusanya kama kikundi)
huitaji mtaji wala watu wengi, if you got the deal unaweza ajiri watu for day payment
yeee menPia ukitaka kufanya Car wash ya kisasa inabidi uwe na mtaji mkubwa, kuosha magari kwa ndoo ni kupoteza muda.
Asante sana!!!
.................
Nimejifunza kitu....