Biashara ikianza kuwa ngumu unaanza kujikosoa, "hivi ni mimi niliesema ajira ya kupokea mshahara kila mwezi na posho za kila wiki ni utumwa ?"

Mwaka mgumu huu...
Me Jana kijana wangu, ananiambia Kwa trend inavyoonesha hapa hatutoboi , biashara ngumuu... Tuwaze nje ya box!
Na kweli wateja wamekuwa wakusua sua...huku matumizi makubwaa
Kodi na malipo kila pembe.
 
Ni kweli tabu mitaji ni midogo unajitahidi angalau uajiri na upate atakayekuibia kidogo wakati ukijipanga na mengine.
wife ukimueka wakati mwingine ndo linaweza kuwa balaa tu atalisimamia kwa chips na tusker 2 baridi mambo yatakuwa zaidi ya yaleyale.
 
[emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Biashara ya Tanzania kwa sasa jifunze kutokomea sehemu penye kuhitaji ili wakija wenzako we ushaweka mizizi. leo hii unaenda kufanya biashara mijini labda kuwa na mitaji na ujanja
Vipi sehemu kama kariakoo, pale wateja si wako wengi hata kama ndio unaanza biashara
 
Unakuta mtu anapitia stress lakini anaigiza million kwa mwezi lakini wewe upo comfortable kuingiza laki 3 after makato
 
Maisha yote huwezi kuepuka utumwa, labda utaepuka utumwa wa aina fulani tu.

Unaweza kuepuka utumwa wa kufanya kazi chini ya bosi wako, ukafungua biashara, ukaenda kuwa mtumwa wa wateja wako na maafisa wa TRA.

Tajiri mkubwa sana duniani Elon Musk alikuwa na majumba kibao, kayauza karibu yote kwa sababu alijikuta anakuwa kama mtumwa wa mali.

Siku hizi analala mpaka ofisini, kawa mtumwa wa kazi.

Hivyo, usilenge kuepuka utumwa, chagua utumwa utakaoweza kuuvumilia au kuupenda tu.
 
Unakuta mtu anapitia stress lakini anaigiza million kwa mwezi lakini wewe upo comfortable kuingiza laki 3 after makato
Ni kweli mtumishi anaweza akawa anapokea laki 3 baada ya makato na asiwe na stress, yena hapo unakuta kaajiriwa kwa cheti cha certificate (kipo chini ya diploma)

ni tofauti na Mtu kakopa milioni 100 biashara iningiza milioni 1 kwa mwezi, ukianza kutoa makato ya frem, mishahara, kodi, ulinzi, vibali, n.k. anabakiwa na negative / hasara
 
Ni kweli mtumishi anaweza akawa anapokea laki 3 baada ya makato, ni tofauti na Mtu kakopa milioni 100 biashara iningiza milioni 1 kwa mwezi, ukianza kutoa makato ya frem, mishahara, kodi, ulinzi, vibali, n.k. anabakiwa na negative / hasara
Kwaiyo mtumishi hakopi?
 
Kwaiyo mtumishi hakopi?
umeshasema mshahara baada ya makato.

cha ajabu kwa mfanyabiashara umeandika kiupendeleo kwamba anaingiza milioni 1 huku ukisahau makato, hapo unakuta frem laki 5, mshhara na chakula cha msaidizi laki 3, anabaki na laki 2, ... na hapo hana marejesho ya mkopo
 
Million mbili baada ya kutoa huo ushenzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…