Biashara ilinifunza kwamba ukiweka mbongo dukani itakulazimu uwe makini sana na daftari lasivyo utapukuchuka

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Hili ni moja ya mafundisho muhimu sana niliyowahi kujifunza kwenye biashara na bahati mbaya au nzuri, nililijifunza kwa kulipa ada kwa njia ya hasara. Siku hizi niko makini kupita maelezo. Nafuatilia kila kinachoendelea dukani kwa karibu. Hata kama mteja amenunua bidhaa ya laki mbili halafu akasema atamalizia deni la buku baadae lazima lirekodiwe. Hakuna kitu kidogo kwenye biashara.

Nilikuwa nimetingwa na shughuli zangu nyingine, nikawa naacha duka chini ya uangalizi wa mfanyakazi nikiwa na imani naye.

Nikawa mvivu wa kukagua daftari la hesabu. Wakati mwingine inafika hadi mwezi mzima sijafunga hesabu — nachukua tu hela bila kuangalia vizuri. mwezi ukipita nikitaka kuanza kupiga hesabu nasahau nilipoishia naanza kukisia, nakuwa nimejitengenezea mwenyewe mazingira ya KUPIGWA.

Mizigo ikifika, yeye ndiye anasimamia kushusha na kuingiza kwenye stock.

Kwa kuwa alianza kuona sifatilii sana, na yeye akaanza kuwa mvivu kurekodi baadhi ya madeni na mauzo. Badala yake, alikuwa anakremu tu.

Nikifika dukani nikichukua kiasi pungufu ya mauzo hasemi chochote anajipigia cha juu. Ikitokea kuna short ndio atasema kuna mzigo aliuza anasubiri hela jioni.

Ukirudi kuangalia stock, unahisi kizunguzungu !! Unashindwa kuelewa mzigo ulienda wapi. Kichwa kinataka kulipuka.
 
kwenye biashara "ufuatiliaji" ni kazi pia
 
Biashara yoyote kama unataka kufanya usimuweke mtu kaa mwenyewe kwa nzia manunuzi na kuagiza mzigo na lazima uwe na rekodi ya kila siku umeuza sh ngap na faida sh ngapi Mimi nilko kwenye biashara mwAka wa pili naona Nini nachokifanya
 
Kukaa mwenyewe dukani inafaa ukiwa na duka moja au kama huna shughuli nyingine.

Wengine wana duka zaidi ya moja, wengine ni waajiriwa wamejiongeza kufungua biashara kujiongezea kipato, n.k.
 
N

Ni sawa lakini kama unataka kukua kibiashara au unamalengo ya kufika mbali ukimuweka mtu hayo malengo hayawezi kutimia kama umeajiriwa kaa kwenye kazi yako hio pesa Bora ujenge nyumba za biashara kama loge na nyumba za kupangisha biashara inatakiwa umakin mkubwa sana
 
Nimemweka mtu na biashara inakua huku nikiendelea na shughuli zangu, ni suala la mikakati tu, yule mtu wa dukani anahusika zaidi na kuuza tu (salesmanship), mimi nahusika na kuhakikisha mzigo wanaohitaji wateja upo, wanahudumiwa vizuri na kuwa makini kwenye kufuatilia biashara kwenye upande wa records za mauzo, matumizi na faida.
 
Hili ni moja ya mafundisho muhimu sana niliyowahi kujifunza kwenye biashara na bahati mbaya au nzuri, nililijifunza kwa kulipa ada kwa njia ya hasara. Siku hizi niko makini kupita maelezo. Nafuatilia kila kinachoendelea dukani kwa karibu. Hata kama mteja amenunua bidhaa ya laki mbili halafu akasema atamalizia deni la buku baadae lazima lirekodiwe. Hakuna kitu kidogo kwenye biashara.

Nilikuwa nimetingwa na shughuli zangu nyingine, nikawa naacha duka chini ya uangalizi wa mfanyakazi nikiwa na imani naye.

Nikawa mvivu wa kukagua daftari la hesabu. Wakati mwingine inafika hadi mwezi mzima sijafunga hesabu — nachukua tu hela bila kuangalia vizuri. mwezi ukipita nikitaka kuanza kupiga hesabu nasahau nilipoishia naanza kukisia, nakuwa nimejitengenezea mwenyewe mazingira ya KUPIGWA.

Mizigo ikifika, yeye ndiye anasimamia kushusha na kuingiza kwenye stock.

Kwa kuwa alianza kuona sifatilii sana, na yeye akaanza kuwa mvivu kurekodi baadhi ya madeni na mauzo. Badala yake, alikuwa anakremu tu.

Nikifika dukani nikichukua kiasi pungufu ya mauzo hasemi chochote anajipigia cha juu. Ikitokea kuna short ndio atasema kuna mzigo aliuza anasubiri hela jioni.

Ukirudi kuangalia stock, unahisi kizunguzungu !! Unashindwa kuelewa mzigo ulienda wapi. Kichwa kinataka kulipuka.
Mkuu Pole sana, Karibu tukupatie Mfumo wa Usimamizi wa Bidhaa inapotengenezwa, kununuliwa, kuuzwa au kuwa destroyed. Ni mfumo wa kidijitali wa usimamizi wa biashara. Bofya Link hii https://duka.haofo.or.tz/
 
Nimemweka mtu na biashara inakua huku nikiendelea na shughuli zangu, ni suala la mikakati tu, yule mtu wa dukani anahusika zaidi na kuuza tu (salesmanship), mimi nahusika na kuhakikisha mzigo wanaohitaji wateja upo, wanahudumiwa vizuri na kuwa makini kwenye kufuatilia biashara kwenye upande wa records za mauzo, matumizi na faida.
Hongera sana Kiongozi, Simamia biashara yako kidijitali ukiwa na SHARED DUKA ENTERPRISES PORTAL https://duka.haofo.or.tz/
 
Biashara yoyote kama unataka kufanya usimuweke mtu kaa mwenyewe kwa nzia manunuzi na kuagiza mzigo na lazima uwe na rekodi ya kila siku umeuza sh ngap na faida sh ngapi Mimi nilko kwenye biashara mwAka wa pili naona Nini nachokifanya
Kwamtindo huu huwezi ipanua biashara,maana halisi ya biashara ni kuiacha pesa ikuingizie pesa sio wewe kuweka hela alafu bado unalazimika kukaa kwenye biashara
 
Back
Top Bottom