Biashara ipi itafaa zaidi kwa Toyota hiace? Tanga city

Biashara ipi itafaa zaidi kwa Toyota hiace? Tanga city

wa kihesa

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2018
Posts
206
Reaction score
207
Salam Salam wapigania Uchumi.
Nina Toyota hiace(dungu) ipo Tanga mjini. Nafikiria niisajili ifanye moja Kati ya kazi (routes) zifuatazo;
1. Kufanya town route(daladala)
2. Kufanya routes za nje kidogo ya mji..at least umbali usiozidi 70km.
3. Kufanya routes za mbali zaidi ya 70km.
4. Nyinginezo.
Naamini wapo wazoefu wa haya mambo humu.
Nakaribisha maoni na ushauri.
Gari ni yangu mwenyewe.
KARIBUNI SANA
 
Mkuu ipige ruti ndefu hata ya Horohoro kama gari lako zima au jipya au za fupi basi ipige stand ya zamani to Pongwe itakuwa safi Sana
 
Me ni mwenyeji wa Tanga kwa ruti za ndani Tanga beach pesa ipo pia Mabokweni /Amboni pesa ipo ni njia ya Horohoro
 
Mkuu nichukue tukaenze routes ya horo horo mbna Safi Sana
 
Mkuu ipige ruti ndefu hata ya Horohoro kama gari lako zima au jipya au za fupi basi ipige stand ya zamani to Pongwe itakuwa safi Sana
Hizo ruti zimekaa vizuri. Ngoja niendelee kuzidadavua. Shukrani Mkuu.
 
Me ni mwenyeji wa Tanga kwa ruti za ndani Tanga beach pesa ipo pia Mabokweni /Amboni pesa ipo ni njia ya Horohoro
Hii ya kwenda tanga beach unaweza ielezea zaidi? Naona wengi wanaikimbilia. Mi nazipenda routes zenye challenge ila ziwe na watu.
 
Hii ya kwenda tanga beach unaweza ielezea zaidi? Naona wengi wanaikimbilia. Mi nazipenda routes zenye challenge ila ziwe na watu.
Tanga beach uzuri wake inabeba watu waishio donge ambapo gari za donge pia zinapita sasa tanga beach inapita donge hadi huko tanga beach kwenyewe na watu wa donge uoendelea kali za tanga hii kutokana hazilali/kusimama hovyo kama wafanyavyo donge ..ila routes zenye challenge nzuri horohoro nzuri Sana pia ina watu wengi hasa wafanyabishara hizi gari zinabeba hadi mizigo kutoka mjini pia ni hela ambapo dala dala za ndani mizigo mingi hawachajiwi abiria hawalipi ila siyo horo horo kule kuzuri sana .
 
Back
Top Bottom