Biashara ipi kati ya hizi mbili inalipa zaidi kati ya Fusso Tippa Vs Coaster ya Kubebea abiria

Biashara ipi kati ya hizi mbili inalipa zaidi kati ya Fusso Tippa Vs Coaster ya Kubebea abiria

Ndugu yangu ana Tipper naona linampa pesa ila kupata trip yeye ni kazi aliniambia alipata tabu sana mwisho wa siku alikuja kupata connection yupo Tanga mjini pale ....Anachukua mchanga na mawe kuna sehemu inaitwa maweni kiomoni kila trip analaza 90k - 100k halafu anazunguka town pale akitoka nje kidogo labda pongwe hata chaji zinaongezeka ..

Pia anaangalia back haul ya kushusha mzigo na kurudi ,mfano sehemu kama Machui ,Tongoni njia ya pangani barabara ni mbovu anachaji pesa ndefu kidogo..

Pia nimeona trip za town risk ni ndogo haswa ajali za barabara ,umbali sio mrefu kwa sana ...Kikubwa utambue mazingira ya biashara kwamba unaweza kosa wateja sometime siku umepiga trip mpaka 6 au 5 sio mbaya unaweza kukosa kabisa.

Sambamba na hilo pia ununuzi wa tipper liwe roho ngumu na jipya sio haya yenye viraka ,then fuata sheria na taratibu zote ... Mwanzoni usitegemee sna faida ya haraka kwani utakuja kata tamaa ...

Tusidanganywe hakuna mkoa watu wamelala kila sehemu watu wanajenga daily ...Pata connection wengine wanaenda kuulizia mchanga machimboni mpaka gari huko huko basi unaweza chonga na wadau then unawapa dili za kujaza na kupakua mchanga ndio maisha.
 
In

Kumbe umesikia Kwa Ndugu zako , Subiri ukiokota Hela. Na wewe ujaribu hiyo biashara.
Unajuwa Bei ya Coaster
Bei ya Fuso?
Halafu unakuja kumpa mjinga Moja anaanza kulewa na kufuata Malaya wa Kutumia nao Hela za Gari zako?
Kama Mtu hana muda wa kusimamia mwenyewe achana nae , fanya issue zingine, Bora ujikite kwenye Ardhi , nunua ekari zako mbili maeneo ya Kibaha , subiri mwaka Moja au miwili unaanza kukata viwanja, ekari Moja , then unasuburi Tena unauzw. Kidogo kidogo , utapata fedha nzuri ,
Ndio maana nikakuambia wewe haujawahi kufanya biashara hiyo ila ni bingwa wa maneno mengi yasiyokuwa na maana,najua bei za magari kwasababu mimi biashara zangu zinahusisha na kusafirishwa na hayo malori,hapa mtwara kuna madogo kibao walianza na fuso moja baada ya muda saivi wana magari mpaka 10 kwahiyo punguza ujuaji kwasababu kila biashara ili ifanikiwe inahitaji usimamizi mzuri
 
Ukitaka kufa mapema na uongee peke yako barabarani miliki chombo cha usafiri bila usimamizi mzuri

Dereva anaiba,fundi anaiba,konda anaiba, trafiki wanataka pesa

Mi niliwahi lala na viatu siku .....kwanza ukiona simu ya dereva....mapigo yanabadilika kabisa

Mi najiulizaga wanaomiliki mabasi na malori hivi cjui hawana mioyo?
😆😆😆wewe ni muongo sana bila shaka hata pikipiki haujawahi kumiliki
 
Ndio maana nikakuambia wewe haujawahi kufanya biashara hiyo ila ni bingwa wa maneno mengi yasiyokuwa na maana,najua bei za magari kwasababu mimi biashara zangu zinahusisha na kusafirishwa na hayo malori,hapa mtwara kuna madogo kibao walianza na fuso moja baada ya muda saivi wana magari mpaka 10 kwahiyo punguza ujuaji kwasababu kila biashara ili ifanikiwe inahitaji usimamizi mzuri
Biashara yoyote ya Kitanzania inahitaji USIMAMIZI MKALI WA KARIBU, ubunifu na connection.
Biashara za usafiri wa aina yoyote inahitaji USIMAMIZI MKALI MNO. Hao unaoona wametoka kwenye tipa 1 mpaka 10 maana yake wanausimamizi mkali mno. Usiwachukulie poa.
 
Mkuu hizi coster tunazoona zinapiga kazi mjini wamiliki wake hawanufaiki nazo? na mnapozungumzia usimamizi mzuri, mnamaanisha mmiliki ndie akawe kondakta au dereva?
Usimamizi ni km nani anaenda na gari kwa fundi unakuta kifaa hakijaisha kikifunguliwa anauziwa mwingine

Gari mwisho saa ngapi? Na inalala wapi?

Gari route zake kwaanzia saa ngap mpaka saa ngap inanya kazi

Km tu ukienda kariakoo usiku mpaka costa za staff serikalini unakuta inapiga route za tandika..kwa wizi

Sembuse ya mtu binafsi
 
Biashara yoyote ya Kitanzania inahitaji USIMAMIZI MKALI WA KARIBU, ubunifu na connection.
Biashara za usafiri wa aina yoyote inahitaji USIMAMIZI MKALI MNO. Hao unaoona wametoka kwenye tipa 1 mpaka 10 maana yake wanausimamizi mkali mno. Usiwachukulie poa.
Kuna mahala nimekuambia nawachukulia poa? Hakuna biashara isiyohitaji usimamizi hapa duniani
 
Ndio maana nikakuambia wewe haujawahi kufanya biashara hiyo ila ni bingwa wa maneno mengi yasiyokuwa na maana,najua bei za magari kwasababu mimi biashara zangu zinahusisha na kusafirishwa na hayo malori,hapa mtwara kuna madogo kibao walianza na fuso moja baada ya muda saivi wana magari mpaka 10 kwahiyo punguza ujuaji kwasababu kila biashara ili ifanikiwe inahitaji usimamizi mzuri

Mtwara inaonekana biashara ya tipper ni nzuri,ila kwa dar ni ngumu kufikisha gari 10 bila kutuoa kwenye vyanzo vingine.canter Tani 2 bei yake 50m ,hesabu elfu 50,fuso bajaji tan 4 bei Kati ya (75-80m) hesabu elfu 80 hadi laki,isuzu tani 10 bei yake 120m hesabu laki 2.5,mende na faw tan15 bei (130-150) hesabu laki 3,semi tan 30 hesabu laki 5.bado vitu kama service,tairi,bima,latra na TRA ni vya tajiri.hapo kufika break even sio chini ya miaka 2hadi 3
 
Mwaka 2017 kuna jamaa alianza na DCM leo yuko vizuri sana ana TATA 2.
N.B.
Yeye mwenyewe yupo mlangoni anakusanya nauli.
 
Nikushauri tu humu hamna wamiriki wa hayo magari ko auwezi kupata ushauri wa uakika kwenye jambo lako ungefanya kumfuata mmiriki wa izo gari unaemjua uonane nae akupe ushauri wa kweli ila humu watu wanafanya kuona zinapita barabarani wanadhan ndo pesa zinaingia tu.

Binafsi simiriki hata boda nikimiriki nitakushauri
 
Wewe uko wapi na biashar hiyo una mpango wa kuweka wapi?
 
Wakuu nataka kufanya biashara mbili kati ya hizi niwe na fusso tipa la kubebea mchanga, kokoto, vifusi na n.k au niwe na coaster kwa ajili ya kubebea abiria kutoka wilaya moja kwenda nyingine au kutoa mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine.

Naomba wazoefu hizo biashara moja wapo mnipe muongozo mzuri ili nione kipi kitanifaa kati hizo biashara mbili.

Niko hapa nasubiria muongozo wenu wakuu
Kaka samahani naweza kupata bei ya beef fillet
 
Back
Top Bottom