Biashara ipi ya kuwekeza kipindi hiki kwa mtaji wa milioni 30 -50?

Biashara ipi ya kuwekeza kipindi hiki kwa mtaji wa milioni 30 -50?

Turiani msimu wa kilimo unaanzaga mwezi wa ngapi. Na ekari moja wanalima shiling ngap
Mawazo mazuri sana ila yote yanahitaji uwepo wake..haswa no3 ila angeweza kukuza mtaji wake kidogo awe na kama 60m achukue trekta mpya kabisa na jembe lake aingie ata Turiani apo Moro uhakka wa kulaza atleast 18m kila msimu wa kulima
 
Inategemea aina ya biashara sasa...ndio maana kama mimi nikapendekeza Carwash haitaji ujuzi nini kusimamia, ila mfano ayo mambo ya Video photograph kama sio mjuzi uwelewi.

Binafsi niki accumulate kihasi kikibwa kazini najua wapi pa kuepeleka na mpka wa kuisimamia...mpaka muda wa kuacha kazi kifikie nini niache nime plan vyote.
Nadhani ca
Mwambie aje nimuuzie uwanja Chamazi ajenge nyumba apangishe hatojuta bei mzuri tu mil 7 itakayo baki nitampa idea ya biashara ya kufanya nnayotaka kuifanya mimi
Mkuu faida ya real estate ni ndogo sana labda uwe na mtaji wa mabilioni....fikiria nyumba ambayo mtu anajenga kwa gharama ya mil 150 akikodisha hiyo pesa itarudi baada ya muda gani...akipangisha kwa laki 6 au hata 1m kwa mwezi itachukua miaka zaidi ya 10 kurudisha uwekezaji...hii inawafaa watu wanaotaka kutunza tu mtaji lakini sio baishara ya faida ya kutoka kabisa.
 
Hivi kamera zinabei sana ? Au ni zile mac computer? Shukrani kwa mchango
Mimi pia ukiachana na taaluma yangu pia ni Expert wa GRAPHICS & DESIGNING Kwa Computer zenye uwezo na ubora za Graphcs ni ghali sana minimum price ina 900K - M 's inategemea especially for Mac

Pia kwa upande wa Photography Camera nzuri nazo ziko ivyo iyo ni M kadhaa
 
Hahahqhaha eti unatafta partner kwa 40m..nakupa 7mths utakuwa huna hata 200!partiner?😁😁!yaan 40m isimamie mwwnyew kbs..usione watu wanahamia maporini mkuu...binafsi mm hata ndg simwamini kqenye biashara...!

kweli tumepishana
Ni kweli lakini kama lengo ni kufika mbali huwezi kukua ukiwa mwenyewe ndio maana tz hakuna biashara nyingi kubwa sababu kila mtu anataka kufanya mwenyewe. Lazima kushirikiana ili kufika mbali. Changamoto nikupata mtu mwaminifu....
 
Ni kweli lakini kama lengo ni kufika mbali huwezi kukua ukiwa mwenyewe ndio maana tz hakuna biashara nyingi kubwa sababu kila mtu anataka kufanya mwenyewe. Lazima kushirikiana ili kufika mbali. Changamoto nikupata mtu mwaminifu....

Mimi bora nipambane alone aisee...sio kushare na watu
 
Achukue baadhi ya hizi ....

1.Aje Dodoma afungue kiwanda cha kufyatua na kuuza tofali,hii biashara inalipa sana watu wanajenga balaa kwa Dodoma,hapa anaweza kuweka na ki min shop cha hard ware.location zipo nyingi sana za kufanya hii biashara.

2.Aje Dodoma afungue kiwanda kdg cha kusaga na kupaki unga wa mahindi,asee hapa pesa ataikimbia mahitaji ni makubwa sana,waliopo wanaofanya hii biashara hawakidhi mahitaji ya wateja kwamba mda mwingi unga haupo mitaani.location zipo za kutosha nawez kwemwelekeza bure kabisa.

3.Anunue tractor la kilimo alipeleke Manyara,hapa pesa ni nyingi sana na ya uhakika.location za kupeleka tractor kwa Manyara zipo nyingi sana na pesa zipo nyingi sana.
Mkuu naomba nikutafute private hizi ideas zote ninazo na lengo na location nilizowaza ni the same. Kama ulikua kwenye akili yangu
 
Mkuu naomba nikutafute private hizi ideas zote ninazo na lengo na location nilizowaza ni the same. Kama ulikua kwenye akili yangu
Karibu sana mkuu..ideas zipo nyingi zingine zikuziweka hapa jukwaani kwa kuchoka kuandika.
 
Kwa ushauri wangu ningependekeza namba tatu kufungua studio ya kupiga picha na mambo yanayohusiana na hayo. Kwa Sasa biashara za mambo ya graphics designing, wedding photography, photoprinting ndo vinasoko Sana na biashara ya studio ya picha ni marachache Sana kula hasara ila changamoto ni gharama za vifaa watu wazoefu wapo hivyo napendekeza no. 3
Kwani mkuu vifaa ni ghali sana?
Pitapita mtandaoni naona gharama kubwa ni pc Apple iMac Retina display 4k ambayo inafika $1,300 au zaidi
Camera pia nadhani zinafika $2,000 au zaidi...

Hivyo nadhani 20m inaweza kutosha? Wazoefu wa hizi kazi wanaptikanaje? Huwa wanalipwaje kwa kazi au asilimia ya mapato?
 
Kwani mkuu vifaa ni ghali sana?
Pitapita mtandaoni naona gharama kubwa ni pc Apple iMac Retina display 4k ambayo inafika $1,300 au zaidi
Camera pia nadhani zinafika $2,000 au zaidi...
Hivyo nadhani 20m inaweza kutosha?
Wazoefu wa hizi kazi wanaptikanaje? Huwa wanalipwaje kwa kazi au asilimia ya mapato?
Million ishirini inatosha kabisa na kuhusu wazoefu nilimaanisha wale ambao wamekwishafanya kazi katika studio mbalimbali hao unaweza kuwatumia endapo utakua unastudio teali wapo wengi tu ambao wapo tayari kufanya kazi katika studio mpya.
 
HIVI KWANINI UKIWA NA MTAJI UNAKUA HAUNA AKILI YA KUFIKIRIA BIASHARA YA KUANZISHA
 
Aende china akafunge mzigo wa spare za pikipiki alete bongo atafte chimbo lake afungue gerage ndogo ya pikipiki awauzie kwa rejareja huku akitengeneza hizo pikipiki. Kama vipi pia awe anasupply kwenye maduka madogomadogo kwa jumla io ni moja tu nimempa..kama yupo seriouss anicheki mm ndio niwe huyo mtu wa kusimamia miradi yake nina idea kama zote ila tu pesa sinaaa. Mi 40 tutarudisha chap tu aisee daaah
Usimdanganye mwenzio, million 40 ni ndogo mno kufunga mzgo wa spare za pikipiki China au kuuza jumla.
 
Kama ana access ya kupata 40millions kama capital ya biashara anashindwa nini kuachana na hiyo kumtumikia bwana akaingia mtaani akapambana kivyake?

Hapa ndipo naposhindwa kuwaelewa watu wanaosema wamesoma,imani yangu na uzoefu wangu kwa mtaji huo kwa mwezi anaweza kujitengenezea faida nzuri tu kama akitulia kwenye biashara.
Nlikua nataka kusema kama wewe.

Kuna mda huwa siwaelewi kabisa hawa vijana wanaojiita WASOMI.
 
40m kwenda China ? Inabidi ufanye utafiti wa kutosha..la sivyo utaenda mara moja tu na mtaji utakata...gharama ya kwenda na kurudi si chini ya 3m...bado hujatoa mzigo bandarini....frem hujakodi ...leseni.. TRA ..kumbuka sio lahisi kuuza mzigo wote ukaisha lazima katikati kabla mzigo haujaisha uende tena.

hapo ndio utangundua mtaji ni mdogo...labda uwe unchukua oder kwa wenye maduka mzigo ukifika unauza tu. Au subiri wale wanao shusha conterner chukua mzigo na ww uza..wengi ndio wanafanya hivyo kkoo.
 
Biashara inahitaji usimizi wa hali ya juu kutoka kwa muhusika...kama huna muda wa kukaa kwenye biashara ni bora hiyo hela uiweke bank au ujenge la sivyo utaipoteza...sio rahisi sana kuanza biashara ikakuwa ili hali ww ukiwa umeajiriwa sehemu nyingine...hapo ni kama una-beti...na wengi wamepotezea mitaji eneo hilo...msemo wa anza biashara kwanza ndio uache kazi inawapoteza sana waajiriwa wengi ... na kikubwa hapo ni uoga na kutojiamini ... 40m kwa biashara ni mtaji mzuri kwa kuanzia...fanya utafiti wa kutosha alafu fanya maamuzi magumu...acha kazi
 
We ndugu Duksi hebu niambie kwanza kazini unalipwa shilingi ngapi kwa mwezi+ukiongeza na zile ambazo sio za mshahara lakini unazipata kupitia kazi, then ndo nikushauri partneship au quiting the job.

Kwenye partneship kuna kupata faida, kumaintain mtaji tu, au kupoteza na mtaji wako, so nitaona hapa kama itatokea umepoteza ule mtaji na huyo partner wako utaupata kupitia ajira yako baada ya muda gani?
 
We ndugu Duksi hebu niambie kwanza kazini unalipwa shilingi ngapi kwa mwezi+ukiongeza na zile ambazo sio za mshahara lakini unazipata kupitia kazi, then ndo nikushauri partneship au quiting the job.

Kwenye partneship kuna kupata faida, kumaintain mtaji tu, au kupoteza na mtaji wako, so nitaona hapa kama itatokea umepoteza ule mtaji na huyo partner wako utaupata kupitia ajira yako baada ya muda gani?
Nadhani mdau anaeuliza hili hataki kuacha ajira kwasasa. Nijuavyo jamaa analipwa vizuri tu kwahiyo sidhani kama anaweza kuacha kazi anachotaka ni kutanua wigo wa kipato...wahenga husema usiweke mayai yote kwenye kapu moja.
 
hyo namba 2 imenitouch...nimekuDM bro

Sent from my SM-J320F using JamiiForums mobile app
Mkuu una details zozote za hizo mashine kama bei, wauzaji....?

Biashara ili ikuwe inahitaji sana partnership, tatizo lililopo watzania hatujawa na waaminifu kihivyo ktk biashara. Mtu anakuaminisha kwa kukushikia visenti vyako vidogovidogo, siku vikijaa, lahaullah, humuoni tena alipokaa amehama usiku mwingi na laini za simu kavunja mazima.
 
Mradi wa kuzoa taka mtaani.....
Nipe dili kama jamaa atakubali hili wazo.
 
Back
Top Bottom