Biashara itakayokupa faida ya bilioni 1 kwa mwaka

Biashara itakayokupa faida ya bilioni 1 kwa mwaka

Fanyeni biashara ya mafuta. Capital ni kubwa lakini return pia ni kubwa.
 
Sasa mkuu unataka business plan tufanye sisi wewe ukakamatie mshiko pekee. Hebu kuwa serious,
 
Mkuu ipo biashara ya miezi kadhaa2 iyo Bilioni unaikamata fasta, mwambie uyo mzee aende wizara ya Madini akaonane na waziri, alaf akate kibali au vibali vyote, aongee na waziri amwambie wizara impe sehem maeneo ya mwadui pale, au aombe makanikia yaliyoachwa na Williamson, ajenge plant ya kuoshea, akifanikiwa hilo la kupewa yale makanikia ndani ya miezi mitatu yeye ni Bilionea, nina imani hatajutia kuna jamaa yangu alipiga mifuko ya Azam5 hpo saiv anaendesha V8

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usipate Shida Afungue Kiwanda Cha Alizeti Cha Kisasa Singida. Mafuta Ya Alizeti Soko Lake Ni La Uhakika Cha Muhimu Upate Mashine Za Kisasa Zenye Uwezo Wa Kukamua Vizur Na Cost Za Investment Sio Kubwa Sana Na Ukimaliza Kukamua Mashudu Unapeleka Kuuza Kenya Yana Soko Zuri Sana
 
Usipate Shida Afungue Kiwanda Cha Alizeti Cha Kisasa Singida. Mafuta Ya Alizeti Soko Lake Ni La Uhakika Cha Muhimu Upate Mashine Za Kisasa Zenye Uwezo Wa Kukamua Vizur Na Cost Za Investment Sio Kubwa Sana Na Ukimaliza Kukamua Mashudu Unapeleka Kuuza Kenya Yana Soko Zuri Sana
Nafikiri nahitaj kulijua hili kwa mapana na marefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habar zenu wadau.

Mimi ni mfanyabiashara wa kati, yupo mzee mmoja ni mteja wangu wa muda kidogo...kiasi Cha kuwa rafiki.
Baada ya kuniona namna ninavyofanya biashara yangu...alipenda. akanipa kazi ya kumuandalia mpango wa biashara (Business plan) yenye mtaji usiozid mil 20, ambayo anataka kumfungulia kijana wake. Nilianza kutekeleza agizo lake ingawaje ilinichukua muda kidogo...maana hata mzee mwenyewe sio mtu wa hovyo...hivyo sikutaka kumchagulia kitu Cha hovyo hovyo...nashukuru Mungu niliamaliza na last week nimemkabidhi.

Sasa baada ya kupitia kwa makini, juzi aliniita ofisini kwake kwa ajili ya kunipa mrejesho. Kiukweli aliipenda Sana na akasema hakuamini Kama Nina weza kuwaza nje ya box kiasi kile.
Ila kilichonishangaza, amesema anataka kunipa kazi nyingine kabla hiyo haijafanyiwa utekelezaji. Kidogo alinipa mashaka kuona anaweza kunidhulumu wazo langu akalitumia bila Mimi kunufaika.

Ila aliweka wazi hana lengo la kufanya hivyo ila baada ya kusoma wazo langu amegundua Nina kitu kikubwa zaidi ya hicho.

Ananiambia nifikirie mradi utakaoweze kuzalisha faida ya 1bilioni moja ndani ya miezi 12 (mwaka mmoja). Kiukweli nimewaza na kuwazua bado sijapata, Ni biashara gani hasa inaweza kuzalisha fedha nyingi kiasi hicho ndani ya hicho kipindi hicho kifupi. Yani Mil 83.3 kwa kila mwezi. Ukizingatia hali yetu ya kiuchumi kwa hapa nchini. Naomba tupeane mawazo wadau angalau nipate hata mwanga juu ya hiyo biashara.

Sijui ana malengo gani huyu mzee..ila anaonekana yuko very serious, na business plan ya kwanza amenirudishia ili niondoe hofu juu ya kunidhulumu haki yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ni mtego tu umepewa ila sio lengo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MWAMBIE ABETI MKUU..... Fanya hivi.... Achukue Timu mbili za mpira

Manchester City
Barcelona

Azibetie mwezi mzima timu mbili tuu kwa jumla ya mechi 8 Barcelona mechi 4 city mechi 4 kila mechi aweke over 0.5 goli moja tuu UHAKIKA

Jumla Ni odds 4 awake iyo 20M

JUMLA atapata 80M Kila mwezi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatua moja kati ya hizi changamoto hapa ikiwa unahitaji biashara itakayodumu zaidi ya miaka 100. Suala la kuingiza 1B kwa mwaka itategemea na kiwango cha hela atakachowekeza. TIA

  1. NJAA
  2. UKOSEFU WA AJIRA
  3. MAGONJWA
  4. ELIMU
  5. UMEME/NISHATI
  6. UCHAFU
  7. USAFIRISHAJI
  8. MAKAZI
 
Billioni moja kwa mwaka ni pesa ndogo sana, issue ni kuwa na mtaji wa kutosha kufanya investiment kubwa na kuwa tayari kwa lolote. Mimi kwa experience yangu ya biashara ya famasi anaweza akafanya hivi (Theoretically):
Aanzishe reputable pharmacy chain ambapo kila mkoa atakuwa na famasi babkubwa za rejareja angalau 3; achague mikoa 30 tu ya Tanzania, hivyo jumla atakuwa na famasi 90. Kisha awe na famasi za jumla angalau moja Dar es salaam, Moja Arusha, Moja Mwanza na Moja Mbeya.

Famasi standard za rejareja = Millioni 30 kila moja; Famasi 90 => Billioni 2.7 a.k.a 2,700,000,000/=
Famasi standard za jumla = Millioni 150 kila moja; Famasi 4 => Millioni 600

Miezi sita ya mwanzo mfanye marketing na sales ya nguvu + grace period ya kuvumilia "ngombe wenu waanze kutoa maziwa ya kutosha"; baada ya hapo the rest is history!

Kila famasi moja ya rejareja itakupa faida (net profit) ya angalau Tsh 2,000,000/= kwa mwezi.
Famasi 90 x 2,000,000/= => 180,000,000/= kwa mwezi;
=> 180,000,000/= x 12 = 2,160,000,000/= kwa mwaka.

Kila famasi moja ya jumla itakupa faida (net profit) ya angalau Tsh 10,000,000/= kwa mwezi
Famasi 4 x 10,000,000/= => 40,000,000/= kwa mwezi;
=> 40,000,000/= x 12 = 480,000,000/= kwa mwaka.

Faida ya famasi za jumla + famasi za rejareja = 2,160,000,000/= + 480,000,000/=

= 2,640,000,000/= (Billioni Mbili na Millioni Mia Sita na Arobaini)

Ila ajiandae kwa kisukari, presha, kipandauso, kukosa usingizi, msongo wa mawazo, sonona na kadhalika.

NB:
- Huu sio ushauri wa kitaalam bali ni maoni ya kawaida, na ni nadharia tu kwa 100%; ukitaka kuwekeza ongea na wataalam wako wakushauri
- If you want to win big you gotta play big

Nawasilisha ........
 
Back
Top Bottom