Job K
JF-Expert Member
- Oct 4, 2010
- 9,314
- 7,149
Kama upo serious tutafutane ,nakupm namba yangu
Mkuu mwaga data hapa hapa jamvini ili wengi tufaidike!! Achana na mambo ya PM kama mnataka kutongozana na akina Madame B!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama upo serious tutafutane ,nakupm namba yangu
Hivi mkuu inachukua muda gani tangu umeagiza mzigo mpaka unaupata? Na vipi kuhusu vifaa vya ujenzi? Hivi watu wanavifuata China, Hong Kong au Dubai?
Tayari huyo ameshachezea kitu Ban!! Unacheza na PAINKILLER nini??!!
YAP! Watu wanajadili vitu vya msingi yeye analeta masikhara!! Ukute lenyewe hata biashara ya kuuza ubuyu haliwezi!! Mijitu mingine hovyo kabisa. Ila mkuu kuna darsa moja kuhusu biashara ya kufuata nguo Uganda umelitoa kwa ufasaha sana BIG UP SANA MKUU!! Hebu aidia na kwenye hili mkuu.Vizuri sana maana jamaa nimefatilia sana comments zake hapendi maendeleo na anaponda kila kitu.
Huyo apewe ban ya maisha kabisa
Hapo kwenye red mkuu, ni wapi ambako vifaa vyake vina ubora na bei nzuri? Maana usije mtu ukawa umeagiza mzigo halafu unafika hapa unaambiwa vifaa havina ubora, hivyo vinakanyagwakanyagwa na katapira!! Na hapo kwenye ubora huwa inakuwaje ukishaifikisha hapa nchini? Hawa jamaa wa TBS kuna popote wanaingia hapo mkuu?Mkuu,
Kuhusu muda inategemea na aina ya bidhaa na mfumo wa usafiri ambao utapenda kuutumia.
Kwa mfano bidhaa zinazosafirishwa kwa ndege huchukua siku tatu za kazi hadi nne (Kulingana na route ya ndege za mizigo kwa wiki husika)
Ukitumia usafiri wa maji (Meli) pia utapata makadirio kulingana na siku ya kupakia lakini Mara nyingi huchukua siku 40 hadi 50 hadi kukabidhiwa mzigo wako.
Vifaa vya ujenzi (Hasa vya finishing) vinapatikana kote China na Dubai. Tofauti hapo ni bei, quality na quantity. Hata hivyo kwa China sasa maeneo kama Hong Kong na Guangzhou yamekuwa ni masoko mchanganyiko bila kuchagua kama awali kwa mfano Guangzhou walikuwa na soko kubwa la electronics na viatu huku Hong Kong wakiwa na soko la nguo na vifaa vingine vya pamba.
Hapo kwenye red mkuu, ni wapi ambako vifaa vyake vina ubora na bei nzuri? Maana usije mtu ukawa umeagiza mzigo halafu unafika hapa unaambiwa vifaa havina ubora, hivyo vinakanyagwakanyagwa na katapira!! Na hapo kwenye ubora huwa inakuwaje ukishaifikisha hapa nchini? Hawa jamaa wa TBS kuna popote wanaingia hapo mkuu?
Ubarikiwe mkuu!!Nina experience kidogo na China. Kuna madaraja ya bidhaa zozote za ujenzi, wapo wafanyabiashara ambao hawana uzoefu wa kuchagua madaraja ya bidhaa hivyo hujikuta wakinunua bidhaa zisizo na viwango vinavyokubalika na TBS na kuishia kuteketezwa kwa mali zao.
Utaratibu wa TBS bandarini upo wazi na wanashirikiana kwa karibu sana na TRA na TICS/ Airport. Wana vipimo vyao ambavyo huwa ni lazima wajiridhishe juu ya ubora wake kabla hawajakuruhusu kupeleka sokoni. Hata hivyo, sababu ambazo zimekuwa zikisababisha baadhi ya wafanyabiashara kuingiza bidhaa zisizo na ubora ni pamoja na; 1. Kutokuwa na ujuzi wa kutambua madaraja ya bidhaa, 2. Kupenda kununua bidhaa kwa bei ndogo zaidi ili kujipatia faida nyingi, 3. Kubambikwa na baadhi ya makampuni na au madalali wasio waaminifu juu ya ubora husika.
Kumbe wakatisha tamaa wamekuwemo JF tokea "zamani"😀Vizuri sana maana jamaa nimefatilia sana comments zake hapendi maendeleo na anaponda kila kitu.
Huyo apewe ban ya maisha kabisa