Biashara Leo: Biashara unayofanya sasa, au utakayoanza sasa, Sio Biashara utakayofanya milele

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,915
Reaction score
3,422
Moja ya changamoto ambazo zinawazuia watu wengi kuingia kwenye biashara au kukuza biashara zao ni kufikiria ni biashara gani sahihi kwao kufanya.
Watu wengi hupoteza muda mwingi wakitafuta wazo bora kabisa la biashara ambalo litawaletea faida kubwa na mafanikio makubwa pia.
Wafanyabiashara wengine huumia sana pale ambapo wazo lao la biashara haliwaletei matokeo waliyotarajia. Hii huwapelekea kukata tamaa na kuona hawawezi kufikia mafanikio kupitia biashara.
Sasa leo nataka nikupe mbinu moja rahisi sana. Mbinu hiyo ni kwmaba usihangaike sana kutafuta wazo la biashara na pia usiumie sana pale ambapo wazo ulilotegemea halijaleta mafanikio uliyotaka.
Kama unaanza biashara anza na wazo lolote ambalo linawezekana kwenye mazingira uliyopo. Angalia chochote ambacho unaweza kufanya na watu wakakulipa hata kama ni kiasi kidogo. Lengo lako kubwa sio kupata faida kubwa kwenye biashara ya kwanza, hakuna uhakika wa hilo, ila lengo lako ni kujifunz akuhusu biashara hiyo na biashara kwa ujumla. Na elimu bora utakayoipata pale utaweza kuitumia kwenye biashara yoyote utakayofanya baada ya hiyo. Hivyo usipoteze muda kufikiria ni biashara gani bora unayoweza kuanza nayo, mabadiliko yanatokea kila siku hivyo fanya kile ambacho kitakupa elimu nzuri kuhusiana na biashara. Kumbuka hakuna elimu bora kama utakayoipata kwa kufanya mwenyewe, utakapopata hasara utajifunz ani jinsi gani yakukwepa hasara baadae.
Kama tayari upo kwenye biashara ila haifanyi vizuri usipoteze muda wako kulalamika kwamba biashara hailipi ay hutaweza kufikia mafanikio. Badala yake angalia ni kitu gani unachoweza kubadili kwenye biashara hiyo ili iweze kuleta faida. Kumbuka biashara yoyote ambayo unafanya, hata iwe ngumu kiasi gani, kuna wenzako wanaifanya na wanapata faida kubwa. Hivyo angalia ni kitu gani wenzako wanafanya kwa utofauti na wewe ukifanye ili uweze kupata faida. Biashara yako haiwezi kubadilika kama wewe hutobadilika. Kama biashara yako ni ngumu na haikupatii faida nina neno moja la kukuambia, BADILIKA. Ukibadilika na kuanza kuibadili biashara yako utaona mabadiliko kwenyekipato chako pia.
SOMA KITABU; JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA na utajifunza mbinu nzuri sana za kujiandaa na mabadiliko kwenye biashara.
Fanyia kazi mbinu hii ya leo na kesho tukutane hapa kwa mbinu nyingine nzuri.
Kwa ushauri zaidi wa kibiashara piga simu 0717396253.
Kila la kheri.
 
Mkuu waweza n pm no y CMU kama utojali
 
Hongera Amani kwa makala zako,na hata ukiwa unahojiwa kwenye Tv na vyombo vingine vya habari huwa napenda unavyotuhamasisha vijana.
Nikija Dar nitakutafuta in person kuna vitu nataka unipe consultation,ready to pay all consultation fees.
Maana naheshim taaluma yako na ninajua Chuo kikuu umelipia ada kubwa sana kwa masomo yako.

Stay blessed
 
Asante sana mkuu.
Karibu sana.
 
Theoretically ni rahisi sana,lakini kwenye utendaji hata maprof. pale UDSM inawashinda,nakuhakikishia ukisoma sana haya mavitabu hutakaa ufanye biashara yoyote!
 
Hapa ndipo watanzania tunapoachwa nyuma. Watu wanafanya biashara kwa mazoea, wakipewa nafasi ya kujifunza njia bora wanakuja na sababu. Mara haiwezekani, mara ni theory.
Kama biashara yako inakusumbua, ni hakika kwamba haiwezi kubadilika kama unaendelea kufanya kile ambacho unafanya kila siku. Sasa kwa nini usijaribu mbinu mpya unazojifunza na ukaokoa biashara yako?
Mtu yeyote ambaye hatafuti maarifa anajiandaa kupotea.
Amua kutafuta maarifa na uyatumie kuboresha biashara yako au amua kupuuza na kufanya kile ambacho umezoea kufanya kila siku. Hakuna atakayekushikia fimbo au kukulazimisha mwisho wa siku wewe ndio utafaidi au kuendelea na biashara iliyo na changamoto nyingi.
 
Mimi huwa nashangaa ina maana watu hawajiulizi kampuni kubwa zenye mafanikio zinaendeshwaje? Hivi zingekuwa zinaendeshwa kwa staili ya duka la Mangi pale mtaani zingefika hapo zilipo? Huko kote kwenye kampuni za maana zenye mafanikio wanaoziongoza ni watu wana elimu za kueleweka kwenye biashara. Angalia vodacom, Google, IBM, Hata Azam. Halafu watu wanataka kujiamisha kuwa biashara ni kufanya kiujanja ujanja tu!!!

Kaka we kata shule kuna watu wanakufuatilia na kuelewa unachosema. Leo nimejifunza kitu kwenye hii makala.
 
Back
Top Bottom