Biashara Leo: Biashara yako ni matatizo ya watu

Biashara Leo: Biashara yako ni matatizo ya watu

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,915
Reaction score
3,422
Mbinu bora kabisa itakayokuwezesha wewe kufanya biashara yako wka mafanikio ni kubadili mtazamo wako katika biashara unayofanya.

Tulishakubaliana kwamba lengo la biashara sio kupata faida bali kutengeneza wateja wa kudumu.

Sasa leo tutajifunza mbinu nyingine muhimu ambayo ni kubadili jinsi unavyoichukulia biashara yako. Usiichukulie biashara yako kama tu ni kuuza na kununua bali chukulia biashara hiyo kama kutatua matatizo ya watu.

Kama unauza chakula basi jua kwamba unatatua tatizo la njaa. Kama unauza magari basi jua unatatua tatizo la usafiri. Kama unauza vitu vya ndani basi unatatua tatizo la malazi na kadhalika.

Ni nini faida ya kufanya biashara kwa mtazamo wa kutatua matatizo? Hii itakuwezesha wewe kuweza kujenga mahusiano mazuri na wateja wako. Kama unatatua tatizo la njaa, utampatia mteja kile ambacho kweli kutamuondolea njaa yake. Kama unatatua tatizo la usafiri basi utampatia mteja wako gari au usafiri utakaoweza kumuondolea tatizo hilo. Kadhalika kwenye tatizo la malazi, utampatia mteja bidhaa au huduma zitakazomfanya afurahie malazi yake.

Kwa mtazamo huu utakuwa unakazana kutoa bidhaa au huduma ambayo ni bora sana kwa mteja wako na mteja ataendelea kufanya biasahara na wewe kwa muda mrefu. Na pia atakuwa tayari kuwaambia wateja wengine kuhusu biashara yako, na hivyo utakuwa umevuka changamoto hii ya Kwa Nini Watu Hawawaambii Wengine Kuhusu Biashara Yako.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa.

Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.
 
An entrepreneur is the person who solves other people's problems at profit
 
Watz kwa theory tu, tuko vizuri sana! Sasa twende practical, hata Mwalimu wa biashara hola!
 
Marikita Amani, Salam kwako. Unaelimisha vizuri, Ushauri. Naamini wewe n mtaalam aw mambo ya Biashara kutokana na jinsi unavyoandika, ingekuwa n Vema zaidi Kama ungekuwa unaandika kimpangilio aw kimaelezo na kwa topic, mfano, kwa jinsi gani wazo la biashara linakuja kichwani, how you see it . Visionaries it, nurture it, how you start, when, how, now and then, how you proceed from there, how you overcome the left over on how and then. Hii itasaidia for the start over to get the really picture on how they ll start.

Another thing, umesema business is not all about making profit, it's about retaining your customer and those retained customers becomes your premium clients then you make profit out of that. Sasa wewe kwa nn unaweka mawasiliano yake hapo.ili tukutafute tupate huruma yako and eventually we gonna have to pay you. Right?, what if unajikita tu katika kutoa elimu for all. Bila kuweka any contact, eventually watu watasoma harafu watakutafuta automatically, and they ll become your clients with no efforts of convincing.

N Ushauri tu brother
 
Habari mkuu,

Asante kwa ushauri mzuri. Kuhusu kuweka contacts sijui nikujibu nini maana umejijibu mwenyewe. Umesema nitoe vitu vizuri halafu automatically watu watanitafuta, sasa watanitafutaje? Njia rahisi ya kunipata ni kwa namba hizo za simu. Ukisema kutumia pm ninaweza nisiipate instantly.

Sijajua kwa nini mimi kuweka namba ya simu kunakupa wewe tatizo, lakini kuweka elimu hakukupi tatizo. Labda ni mtazamo wako. Lakibi nimekuwa nafanya hivi kwa wale ambao wanahitaji msaada zaidi wajue pa kuupata.

Hata darasani mwalimu akifundisha kuna wanafunzi ambao wanaelewa mara moja, wengine mpaka wapate na tuition, sasa wanahitaji kujua kama tuition ipo.
 
Sawa mkuu,
Kama nilivyokuwa nimesema, ni Ushauri tuu, najua utayafanyia kazi Yale ambayo unaona yanafaa japo systematically na kwa uchache,
All the best.
 
Back
Top Bottom