Biashara Leo: Tumia Sheria ya mara 2, mara 3 kwenye mipango yako ya Biashara

Biashara Leo: Tumia Sheria ya mara 2, mara 3 kwenye mipango yako ya Biashara

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,915
Reaction score
3,422
Pamoja na uwezo mkubwa ambao tunao, pamoja na maarifa mengi tunayoweza kujikusanyia bado hakuna mtu anayeweza kuitabiri kesho kwa asilimia 100. Hakuna.

Hakuna anayejua ni nini kitakachotokea kesho kwenye maisha yake au biashara yake. Lakini hii haituzii kuweka na kufanyia kazi mipango yetu kwenye maisha na biashara zetu.

Kwa kuwa hatuna uhakika na kesho yetu, mara nyingi sana tumekuwa tunaweka mipango lakini tunashindwa kuitekeleza kwa wakati. Tunajua kabisa ni kitu gani tunataka na tunakiwekea mipango mizuri lakini tunashindwa kukifikia.

Mara nyingi hali hii huwaumiza watu wengi na wengine huchukulia kama wameshindwa au hawawezi biashara.


Leo nataka nikuambie usiumie tena na hali hii, haitokei kwako mwenyewe na huwezi kuthibiti kesho yako. Unaweka mipango leo lakini hujui nini kitatokea kesho. Hivyo kujilaumu hakuwezi kukusaidia. leo nakushiriksiha sheria moja muhimu itakayokuwezesha kuondokana na hali hii ya kushindwa kufikia mipango yako kwa wakati.

Sheria hii inaitwa MARA MBILI, MARA TATU. Sheria hii ina maana kwamba katika mipango yako yote ya fedha weka MARA MBILI. Kwa mfano kama umesema biashara unaotaka kufanya unahitaji shilingi milioni 10 basi tafuta milioni 20. Hii ni kwa sababu kwamba mahitaji yako ya fedha yatakuwa makubwa kuliko ulivyopanga.

Pia katika mpango wa muda fanya MARA TATU. Kama unafikiri bashara yako itakuwa imesimama baada ya miezi miwili weka miezi sita. Kama unafikiri mzigo ulioagiza utafika ndani ya siku moja weka siku 3. Hii itakuondolea usumbufu pale jambo linaposhindwa kukamilika kwa wakati.


Sio mara zote utahitaji fedha mara mbili na sio wakati wote muda utakuwa mara tatu. Ila tuna uhakika kwamba utahitaji fedha zaidi ya ulizapanga sasa na utahitaji muda zaidi ya uliotenga sasa. kwa kujiwekea nafasi kubwa ya fedha na muda kunakufanya ufanye biashara yako kwa uhuru sana na kuepuka kuwa na msongo wa mawazo kila mara ambapo mambo hayajakwenda kama ulivyopanga.

Biashara yenyewe tu tayari ni ngumu, usitake kuongeza ugumu wake kwa mipango yako mwenyewe. Iweke mipango yako kwa nafasi ya kukutosha wewe kuifanya kwa ufanisi na ukiw aumetulia.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.


Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa.

Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.
 
Huwa naheshimu sana mawazo yako kaka,,ingawa natathmini pale nilipoanguka ila kwa Mbinu hizo ntajaribu for the second Time
 
You mean every action should have emergency plan.
 
Huwa naheshimu sana mawazo yako kaka,,ingawa natathmini pale nilipoanguka ila kwa Mbinu hizo ntajaribu for the second Time

Mkuu John, kung'uta vumbi songa mbele. Utamu wa mission ya aina yeyote ile haupo kwenye kurusha ngumi pekee bali pia kwenye uwezo wa kuendelea na game hata baada ya kupigwa ngumi za uhakika. Waulize wote walifanikiwa,watakuonesha makovu makubwa ya majeraha. Vita mbele kwa mbele mkuu don't give up the fight.
 
natamani na mie nichangie hivi sheria hizi ni kinga kwa mipango yote ya maendeleo ya mparanganaji yeyote.
 
Back
Top Bottom