Biashara mbaya kati ya necta na serikali

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Kumekuwa na hujuma za makusudi kati ya NECTA na serikali juu ya urudiaji wa mtiani Private candidate, watainiwa wengi sana wa PC wanapewa mtiani mgumu sana ukilinganisha na SC , hivyo sasa serikali kama kawaida yake hutumia mwanya huu kujipatia kipato kila mwaka kwani idadi inayorudia mtiani ni kubwa sana na wote 90% huwa hawapati alama zinazotakiwa. Serikali kwa kupitia NECTA imetangaza kwamba ili mtu ajiunge na Unesi daraja la juu diploma nilazima awe na alama za d kwenye somo la kemia na biology, ikumbukwe kwamba zamani manesi wengi walikuwa wanachukuliwa kama walimu kwa ufaulu wa div 26-28, katika vyuo vyao husoma masomo yote ya sayansi kwa miaka minne na kupata cheti na leseni ya ualali wa kuitwa msomi mtabibu, sasa nesi huyu aliyeitumikia serikali miaka kumi, leo hii anataka kusoma wewe unadai ni lazima awe na D ya sayansi, hivi kweli atatoka? Kingine ni kwamba kila mwaka wanabadili mitaala je waliosoma zamani wataweza mitiani hii? Serikali hupata mapato kupitia PC kwa kuwa watainiwa wengi hujaza form wakiwa wamechelewa kutoka na kutokuwa na habari NECTA hupiga faini kwa asilimia 20% .
Maajabu ya mtiani wa mwaka 2012 ni kwamba waliokuwa wamerudia kutafuta c na kusafisha cheti kwa kufanya mitiani yote ndio wamepata zero vipindi vyote. Mfano Tegeta Centre ni shule mojawapo ambayo wanafunzi wake wa PC huwa wanafanya vizuri lakini mwaka huu ni mswaki, hivi nao hawa watu wazima wamechora Messi huku wakiwa wanajua kuwa wamepoteza muda na pesa? Kawambwa ni wakuondoka tu asijitetee, kama kweli kwa nini mwanafunzi huyu asifatiliwe akaadhibiwa.
 
PC kwa kweli wananyanyaswa sana as if sio wanafunzi!
 
nasikia mwaka jana kuna baadhi ya mitihani ilikuwa both school candidates and privates!
 
Naunga mkono hoja kuwa PC wananyanyaswa sana mkuu, mwaka huu serkali ni lazima infind wayout ktk kukomesha swala hili la hujuma.
 
inauma sana kusoma form four miaka 10 ukiambulia zero huku kwingine ulikuwa unatafuta c moja tu lakini kila mwaka unalamba mswaki, jiulize hivi kweli PC wote ni wajiinga kiasi cha kutumia hela nyingi kila mwaka kutafuta credit, kweli NECTA haitaki wasomi lakini hii inalazimishwa na serikali kwamba ikizalisha wengi watenda shule zipi wakati hakuna shule za kutosha.
 
Tulishaambiwa tukiwa shuleni, tusicheze tukafeli tukadhani tutapasi tukirudia mtihani kama PC, Walimu walituambia tufute hizo ndoto, kwa sababu usahihishaji wa mitihani hiyo ni tofauti na usahihishaji wa mitihani ya wanafunzi wakawaida.
Lakini hata hivyo wapo waliorudia mtihani wa A-level na wakapata C tatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…