mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,778
- 7,145
Kumekuwa na hujuma za makusudi kati ya NECTA na serikali juu ya urudiaji wa mtiani Private candidate, watainiwa wengi sana wa PC wanapewa mtiani mgumu sana ukilinganisha na SC , hivyo sasa serikali kama kawaida yake hutumia mwanya huu kujipatia kipato kila mwaka kwani idadi inayorudia mtiani ni kubwa sana na wote 90% huwa hawapati alama zinazotakiwa. Serikali kwa kupitia NECTA imetangaza kwamba ili mtu ajiunge na Unesi daraja la juu diploma nilazima awe na alama za d kwenye somo la kemia na biology, ikumbukwe kwamba zamani manesi wengi walikuwa wanachukuliwa kama walimu kwa ufaulu wa div 26-28, katika vyuo vyao husoma masomo yote ya sayansi kwa miaka minne na kupata cheti na leseni ya ualali wa kuitwa msomi mtabibu, sasa nesi huyu aliyeitumikia serikali miaka kumi, leo hii anataka kusoma wewe unadai ni lazima awe na D ya sayansi, hivi kweli atatoka? Kingine ni kwamba kila mwaka wanabadili mitaala je waliosoma zamani wataweza mitiani hii? Serikali hupata mapato kupitia PC kwa kuwa watainiwa wengi hujaza form wakiwa wamechelewa kutoka na kutokuwa na habari NECTA hupiga faini kwa asilimia 20% .
Maajabu ya mtiani wa mwaka 2012 ni kwamba waliokuwa wamerudia kutafuta c na kusafisha cheti kwa kufanya mitiani yote ndio wamepata zero vipindi vyote. Mfano Tegeta Centre ni shule mojawapo ambayo wanafunzi wake wa PC huwa wanafanya vizuri lakini mwaka huu ni mswaki, hivi nao hawa watu wazima wamechora Messi huku wakiwa wanajua kuwa wamepoteza muda na pesa? Kawambwa ni wakuondoka tu asijitetee, kama kweli kwa nini mwanafunzi huyu asifatiliwe akaadhibiwa.