Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli 100% nimepata mawazo ya biashara tena mazuri mno na ila mtaji sasa ndo mtihaniUnajua watu wengi haswa mswahili, anakwambia ili ufanye biashara lazima kwanza uwe na wazo, hili kwangu ni BIG NO mtaji kwanza wazo baadaye hivi hujawahi kuwa na wazo miaka kadhaa iliyopita na ukaja kufeli kwasababu hukuwa na mtaji. Tuache nadharia za kwenye makaratasi tuende kwenye uhalisia.
Hujawahi jiuliza kwanini aliyesoma BBA wengi wao huwa hawafanti biashara ila wanataka waajiriwe?
Kwangu biashara ni mtaji wazo ni ujinga, ni sawa kuwa na wazo kwenda kuwekeza sayari ya JUPITER wakati unajua hilo haliwezekani kutokana na mtaji
Unajua watu wengi haswa mswahili, anakwambia ili ufanye biashara lazima kwanza uwe na wazo, hili kwangu ni BIG NO mtaji kwanza wazo baadaye hivi hujawahi kuwa na wazo miaka kadhaa iliyopita na ukaja kufeli kwasababu hukuwa na mtaji. Tuache nadharia za kwenye makaratasi tuende kwenye uhalisia.
Hujawahi jiuliza kwanini aliyesoma BBA wengi wao huwa hawafanti biashara ila wanataka waajiriwe?
Kwangu biashara ni mtaji wazo ni ujinga, ni sawa kuwa na wazo kwenda kuwekeza sayari ya JUPITER wakati unajua hilo haliwezekani kutokana na mtaji
Dalali anakuwa na mtaji gani?bila mtaji hakuna biashara !
Kuanzisha biashara bila mtaji ni moja ya mambo ambayo kila mtanzania anatamani yangewezekana.
Nina amini inawezekana tu ukiweza kutafsiri maana ya neno mtaji.
(Kwa mtazamo wangu,) Mtaji ni msukumo ambao Mjasiriamalicanahitaji ili kubadilisha wazo lake.kiwa biashara. Kuna aina nyingi za "Mtaji" ila ule ambao umekuwa ukionekana wa lazima, Pesa, ndio umekuwa ukirudisha maendeleo ya watu nyuma.
Aina Tatu za "Mtaji"
Start Up Capital( Pesa)Recquired Skills( Ujuzi)Psycological Motivation(Motisha)
Mtaji wa tatu( Motisha), kila mjasiriamali anao; Pale unapo pata wazo la biashara na kufahamu kuwa lina faida, kitu utakachofikiria kama hatua inayofuata ni mtaji(Pesa). Ukifisha fikiria hivyo tayari umepata Una motisha ya kufanya kile unachoona ni fursa( Wazo lako).
Kosa kubwa ambalo huwa tumezoea kufanya na kutoliona kama kosa ni : Baada ya kupata wazo la biashara na Motisha, Huwa tunakimbilia kufikiria kuwa kitu.kilichobaki ili wazo letu la biashara lifanikiwe ni mtaji wa Pesa, na kuruka kitu muhimu.....Ujuzi.
Mfano: Labda nimekuja na wazo la kuanza kufuga kuku wa kienyeji Large Scale.
Sasa nimeanza kufanya research kuangalia Success Stories Mtandaoni(Youtube, Google, TED) na kugundua watu kweli wanatengeneza pesa na biashara hii, ntakuwa nimepata Motisha ya Kusonga mbele( Mtaji wa kwanza) baada ya hapo ntaanza kufikiria kuhusu mtaji( Na nikiwa nao) Ntaanza kufuga kuku kwa sababu watu wengine kama mimi wanapata faida.
Hili ndilo kosa kubwa kuliko mengine yote, Nimekimbilia kuanza biashara kabla ya kujua wale niliosikia wamefanikiwa walitumia mbinu gani; Sijajua kama ilikuwa ni kwa bahati, Ujuzi fulani au tu hata hakuna ujuzi unahitajika.
Baada ya mda mfupi ntaanza kusambaza habari kuwa Ufugaji wa kuku haulipi...Kumbe ninaonhea jambo ambalo hata silifahamu.
Nachojaribu kukwambia ni kuwa, Mtaji wa Pesa sio lazima likija swala la kuanzisha biashara yenye mafanikio.....ni UJUZI
Kwanini Unapaswa kuwa na ujuzi kuhusu biashara(wazo) Husika?
Kwenye mambo ambayo yana tatiza au kukatisha tamaa ni kwamba kwenye dunia ya sasa, Hakuna mtu aliyefanikiwa atakupa muongozo sahihi kama aliotumia ili kufanikiwa.Na inawezekana hato kupa kabisa...
Sasa jambo hili tumeliona kama ndio jamno sahihi linwlopaswa kufanywa hivyo yule atakayetaka kukusaidia umuone kama Anakuchukulia kama fursa. Hii ni Logic ambayo imekuwa kwa sasa na uwezi kuipinga kwa maneno maana na hata wale wano ipa nguvu hawafahamu wanaongea nini.
Hali hii imefanya hata yule anayetaka kukusaidia kutofanya hivyo maana Business Model yake itachafuka kwa kuonwa kama Scammer( Kuwa anakuchukulia wewe kama fursa yenyewe)
Kuwa na Ujuzi kuhusiana na Idea yako itakupa nguvu za kuipinga ' Sauti ya Upande wa Pili' Kwa kuwa utakuwa unafahamu unafanya nini.
Kuwa makini...
Kipindi unachagua chanzo cha kujifunza zaidi kuhusu wazo lako la biashara, fahamu kuwa wapo pia watu amabao wamejifunza juzi na wanataka kukifanyanwanajua kumbe hawafahamu hivyo kukupoteza itakuwa rahisi mno.
Internet ni ka dunia yetu ;Ina watu ka hawa tulionao sasa hivi....wajuaji na wajanja ambao wnataka kuji Credit kwa mambo ya wengine ili kukupoteza "Two-Faced Logic Validators" Kwa hiyo ukiichagua kama sehemu ya kujifunzia ilo wazo lako...kuwa makini na anayejaribu kukufunza. Fanya research na wakati wote jaribu kubaini kama anajaribu kukuuzia kitu.
Ujuzi ni jambo pekee linaweza kuipa biashara yako nguvu na sio pesa!
Baada ya kuyasema hayo...Zifuatazo ni aina za biashara unazoweza bila mtaji
1. Business Plan Biding( Kuuza wazo/Mpango wa Biashara)
Kama mimi, najua wengi wetu kila siku tunapata Idea mpya za biadhara...Ila nyingine zinahitaji mtaji mkubwa kuliko tunao weza kuwa nao, Labda hata sio mwingi au mkubwa ila tu hatuna pesa za kuanzia.
Kuuza wazo la biashara (Na mpango wake) ni kitu unachoweza kufanya.
Weka hii akilini kabla ya kuendela: Hakuna wazo jipya!
Na ili kuuza wazo la biashara utahitaji uwe na Ujuzi kuhusu wazo lako maana utabidi kuandaa mpango thabiti wa Biashara.
Unaweza soma jinsi ya kuandika Mpango wa Biashara mtandaoni. (Kwenye Blog yangu nimefundisha pia!)
Ukimaliza kuandaa mpango wako wa biashara utafutie hati miliki( Copy Right) Kisha Uza Mpango wako. Ukimwambia mtu akagoma kuununua kisha ikabainika luwa ameanza kuutumia, unaweza kumfungulia mashtaka maana wewe ndiye mmiliki halali wa mpango wako( Kwa sababu ya Haki Miliki)
Hapa sitokwambia umuuzie nani maana utakuwa unawafahamu ni akina nani wanao uwezo wa kumidu Mpango wako.
2.Two Sided Mini-Market Place( Kuwa Mtafiti wa Bidhaa)
Hii model ndiyo rahisi zaidi kwenye list yangu na Inapanuka.
Moja ya makampuni makubwa duniani, Google wanatumia Model hii na wanaingiza pesa nyingi bila kufanya kitu kikubwa.
Mfano, Ukiangalia Youtube; ni Tovuti ya pili maarufu duniani na Google hawafanyi kitu ili kuifanya iwe hivyo.
Waliandaa Platform ambako wanaweza wakakufanya Uweke Video kibao( Kwa kutumia Adsense, utalipwa), Kumfanya Mtu aangalie Video( Kwa kuwa wewe umeziweka) na kumfanya Mtu mwingine aweke Matangazo kwenye Video zako ( Kwa kuwa kuna wa kuyaangalia)...
Kwenye process nzima wewe hufanyi kitu. sasa kufanya kitu kama hiyo at Small Scale Inawezekana.
najua unaweza kuwa unamfahamu mtu fulani anayehitaji kitu fulani na pia bado unamfahamu mwenye nacho. Kwa hiyo kazi yako nikum Direct anayehitaji kitu fulani kwa Mwenye nacho...na In return akupe kamisheni kwa kumletea mteja!
Kiurahisi iko hivi;
Mimi naitwa Frank na najua Ben anahitaji Laptop ya Laki Nne.Pia Nafahamu kuwa John ana laptop anauza kwa Laki Tatu na Nusu.Kazi yangu itakuwa kumfanya John amuuzie Ben Laptop kwa Laki Nne kisha Kunipatia ile Hamsini itakayo bakiKiufupi wewe Unaambiwa utafute bidhaa kwa bei fulani, Na kumtafuta anaye uzabidhaa husika kwa bei pungufu.Kama umefunguka Usisahau Kulike na Kutoa maswali/ maoni.
Soma zaidi: Biashara Mbili Unazoweza Kuanzisha Bila Mtaji | TechTania
Ni hatua gani za kufuatwa ili kupata copyright ya wazo la biashara.na gharama zake zikoje
Unaelewa maana ya mtaji?!Dalali anakuwa na mtaji gani?
Hii ni kweli kabisaUnajua watu wengi haswa mswahili, anakwambia ili ufanye biashara lazima kwanza uwe na wazo, hili kwangu ni BIG NO mtaji kwanza wazo baadaye hivi hujawahi kuwa na wazo miaka kadhaa iliyopita na ukaja kufeli kwasababu hukuwa na mtaji. Tuache nadharia za kwenye makaratasi tuende kwenye uhalisia.
Hujawahi jiuliza kwanini aliyesoma BBA wengi wao huwa hawafanti biashara ila wanataka waajiriwe?
Kwangu biashara ni mtaji wazo ni ujinga, ni sawa kuwa na wazo kwenda kuwekeza sayari ya JUPITER wakati unajua hilo haliwezekani kutokana na mtaji