Biashara mpya kusamehewa kodi kwa miezi sita

Biashara mpya kusamehewa kodi kwa miezi sita

Joasi

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
766
Reaction score
674
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imependekeza kusamehe kodi mafanyabiashara au mwekezaji kwa kipindi cha miezi sita pindi anapopewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

Serikali imesema msamaha huo, utaanza kutumika Julai Mosi 2019, ili kumuwezesha mfanyabiashara au mwekezaji kujiandaa na mahitaji yanayotakiwa katika shughuli anazofanya, vilevile kuondoa usumbufu, dhana ya woga wakati wa kuanza biashara ikiwamo mahitaji ya leseni ya biashara na vibali vingine.

Hayo yameelezwa Alhamisi hii na Dkt. Mpango wakati akiwasilisha makadirio na mapato ya Serikali kwa mwaka 2019/20.

“Hatua hii inatofautiana na hali ilivyo sasa ambapo mfanyabiashara anapopewa TIN anaanza kufanyiwa tathimi (tax assessment) ya mapato yake ya biashara na kutakiwa kulipa kodi,” alisema Dkt. Mpango.
 
Hongera serikali ya awamu ya tano, natumai kuna mengi bora yanakuja
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Utekelezaji wa hili suala ukoje wakuu...? Limeshaanza kutekelezeka...?
 
....Samahani Wakuu, Sijaelewa kidogo hapo...'Serikali Inapendekeza...'! Serikali inapendekeza kwa nani? Yenyewe si ndio yenye maamuzi ichukue tu hatua?
Kwani kunaMfanyabiashara anayependa kuanza kukatwa kodi mara tu anapoanza biashara yake?
Kuna mambo mengine Serikali inatakiwa ichukue tu maamuzi kwa faida ya wananchi wake!
Sio kupendekeza! Kwa nani...!
 
Back
Top Bottom