Biashara msimu wa sikukuu. Zipi biashara za kufanya

Biashara msimu wa sikukuu. Zipi biashara za kufanya

Kibenje KK

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2016
Posts
270
Reaction score
391
Kila Mmoja anafahamu kuwa msimu wa siku watu hununua mahitaji mbalimbali. Naomba tusaidiane. Ni biasahra gani ya msimu huu wa siku mtu anaweza kufanya?
 
Vinywaji mtambuka tuu..

Bia konyag ulanzi mbege dadii kimpumu komoni pingu namba kitoko nk
 
Upo sehemu gani kama upo mkoani nunua nguo za watoto dar uza mkoani
 
Biashara ya nafaka hasa mchele grade one. Sikukuu mtu atajitahidi ale mchele mzuri.

Kuku wa kienyeji. Unaweza kutoa Singida na vijijini kisha ukaleta Dar es Salaam. Imezoelewa siku bila kuku haiendi. Unaweza anza chukua oda mapema

Biashara ya nguo. Hapa zaidi nguo spesho za watoto. Unaweza kuuza nguo za vijana pia na wanawake.

Biashara ya usafiri. Kupeleka watu mikoani, unaweza ongea na wenye Costa ambazo hazina kazi ukafatilia kibali cha kupeleka watu mkoani.

Fanya biasahra ya kufungasha zawadi. Hapa ni wewe na ubunifu wako tu. Unaweza chukua box ukafunga vizuri ndani ukaweka zawadi mbali mfano saa, cheni, perfume nk. Unaweza weka option ya mtu kuchagua zawadi wlza kuweka. Msimu wa sikukuu watu huwapa wapendwa wao zawadi.
 
Back
Top Bottom