Biashara Msumbiji

jirani27

Member
Joined
Apr 15, 2014
Posts
56
Reaction score
15
naamin huku nitapata majibu kwa kuhitaji kufanya biashara na msumbiji. tafadhari yeyote mwenye taarifa na ujuzi wa biashara kati yetu watanzania na nchi ya msumbiji naombeni nizifahamu wadau. nahitaji kufanya nao biashara kutokana na location nilipo njombe. nitashukuru kwa michango yenu
 
Ningekushauri uende mji mmoja unaita Tete, kwa vile upo Njombe pitia boda la Kyela hadi Blantyre, pale utapita boda inaitwa Mwanza, ni jirani sana na Tete ni mwezo wa kama saa mbili.

Biashara kubwa pale Tete ni chakula kama Mchele, Unga na Maharage inalipa sana. Ukitanga kupanua biashara, nenda mji mmoja unaitwa Chimoyo maarufu sana kwa kulima ndizi na Wazimbabwe wapo wengi sana hapo, unatoka Chitanda kabla ya kufika njia panda ya kwenda Beira napo biashara hiyo inalipa sana, kwa sababu Msumbiji chakula ni tatizo, wao ni mikate mikate na wao. Nina uzoefu sana na nchi hizi za kusini mwa Jangwa la sahahara nimekaa karibia nyingi.
 

well said mkuu,mm mwenyewe nimekaa sna msumbiji biashara ya chakula haswa maharage inalipa sna.
 
asante sana kakamkubwa..bigbro..na geba2013, msaada zaidi na kutoka msumbiji kuleta tanzania ipi hasa itanifaa, hii ya kupeleka chakula huko itahitaj niwe na kitu cha kurud nacho bongo, biashara ipi itafaa kutoka msumbiji kuja tanzania?
 
Biashara ya kurudi nayo bongo ni meno ya ndovu kule yako mengi sana wateja bongo kibao
 
Huyu anayetaka ushauri ana msingi kiac gani?than nitamshauri ,BEM VINDO EM MOCAMBIQUE,(NAO E PARA QUEM QUER E PARA QUEM PODE)
 
asante sana kakamkubwa..bigbro..na geba2013, msaada zaidi na kutoka msumbiji kuleta tanzania ipi hasa itanifaa, hii ya kupeleka chakula huko itahitaj niwe na kitu cha kurud nacho bongo, biashara ipi itafaa kutoka msumbiji kuja tanzania?

Kaka, biashara ya kurudi nayo Bongo ni ngumu, labda uje na viatu vya ngozi ya mamba vingi inatengenezwa Ureno, bastola ambazo zote zinatoka Afrika Kusini, ila ukikamatwa nayo ni noma, ile nchi iko tofauati sana!
 
du.......ngoja nijipange niende Mozambique kutembea
 
Huyu anayetaka ushauri ana msingi kiac gani?than nitamshauri ,BEM VINDO EM MOCAMBIQUE,(NAO E PARA QUEM QUER E PARA QUEM PODE)

Mimi nina lori(semi trailer) vipi biashara ya usafirishaji huko mozambique?
 
Kama utakwenda Msumbiji fika kijiji cha Mavago jirani na Tunduru. Chukua ndoo za mafuta zilizotumika za kutosha. Kule hawatazinunua kwa hela ila mtabadilishana na kuku wa kienyeji wakubwa hujawahi kuwaona. Pia utaweza badilishana na mayai ya kienyeji. Mfano ndoo 1 ya lita kumi utaweza pata mayai 40 ya kuku wa kienyeji.
 

mkuu haya mapya sasa dah!
Sijaamini bado....ndo moja mayai 40?! .....hii miujiza...sibishi kwa sababu sijawahi kufika huko ila nashindwa kuamini!
 

Wao hizo ndoo wanazifanyia nini noaja zina value kiasi hicho?
 
Mimi nina lori(semi trailer) vipi biashara ya usafirishaji huko mozambique?
hapo utapiga bao...watanzania pale ndio wasafirishaji wakuu jaribu hilo hutapoteza ila wanapigana fitna sana yuko maningnise na kampuni nyingine nimeisahau jina wote ni watanzania...mina nafanya gemstone kule..na watu wa kule wamelala haswa haswa miji yao hii ya pembezoni..mtipweshi ,pemba,nakala,msimbwa,nampula haya na shimoyo huko kumejaa watanzania na wanafanya vizuri
 
mkuu haya mapya sasa dah!
Sijaamini bado....ndo moja mayai 40?! .....hii miujiza...sibishi kwa sababu sijawahi kufika huko ila nashindwa kuamini!
Biashara iyo siijui ila kwa msumbiji watu wamelala mno mno tena watanzania wanajichumia pale kama hawa akili vizuri tena kwa biashara tofauti tofauti ...ninauzoefu napo msumbiji
 

Vp kuhusu Malawi?
Nipo Kyela.
 
Vp kuhusu Malawi?
Nipo Kyela.

mkuu ile nchi ni ya watanzania, wako wengi kweli...si lilongwe wala mzuzu,ila kule vfaa vya ujenzi ni hela!
Pia kule baiskeli ni kama bodaboda au daladala
ukiuza vfaa vya baiskeli unaweza piga hela pia!
 
thanx sana kwa ushauri, nadhan its time ya kuvuka boda now kwa tz biashara nshaifaham vya kutosha. pia nilitaman biashara na uganda kutokana na maelezo ya money stunna, bt kutokana na location nliyopo na kwa ushaur wenu, ts time for the nearest country, thats msumbiji, malawi na zambia ntakuja. pia naomben wenye ujuz na ushaur zaid kwa msumbiji, pia zambia na malaw in future.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…