Biashara Msumbiji

Biashara Msumbiji

Wao hizo ndoo wanazifanyia nini noaja zina value kiasi hicho?

Mtu akiwa nazo ndani anaonekana ana maisha mazuri. Wanaweka maji na kutunzia bidhaa za mashambani. Pia wengine wanawindia wanyama kama sungura nk wakiweka chakula wakiingiza kichwa hawatoki. Pia kwa aliyeshangaa mayai 40 hicho ni kidogo mno. Mavago kuku ni wengi kama pikipiki za Mwanza au kule Songea hawaoni hasara kabisa. Pia wengi wamelala.
 
mkuu inamaana nikitaka kununua hao kuku?..yaani badala ya ndoo, niwape hela!
Ahsante sana
 
wakuu kuna huu uzi , hapa wadau wamejaribu kutupa kitu kuhusu fursa nchini msumbiji INGIA HAPA
 
Tatizo mitikash yao si dili tz,vijana weng wanatoka kwa kwenda migodin na si issue nyingine
 
Kama utakwenda Msumbiji fika kijiji cha Mavago jirani na Tunduru. Chukua ndoo za mafuta zilizotumika za kutosha. Kule hawatazinunua kwa hela ila mtabadilishana na kuku wa kienyeji wakubwa hujawahi kuwaona. Pia utaweza badilishana na mayai ya kienyeji. Mfano ndoo 1 ya lita kumi utaweza pata mayai 40 ya kuku wa kienyeji.

Hao ndugu wanaongea LUGHA gani, pia Km itawezekana unaweza kujua umbali wakutoka TUNDURU hadi hapo mavago? Gharama zikoje km hutajali,,,!
 
Hao ndugu wanaongea LUGHA gani, pia Km itawezekana unaweza kujua umbali wakutoka TUNDURU hadi hapo mavago? Gharama zikoje km hutajali,,,!

kama unaweza kimakonde mtaelewana, kireno, kiswahili wachache.
 
poa ndugu thanx wacha niichungulie hapo link ya majigo
 
mkuu ile nchi ni ya watanzania, wako wengi kweli...si lilongwe wala mzuzu,ila kule vfaa vya ujenzi ni hela!
Pia kule baiskeli ni kama bodaboda au daladala
ukiuza vfaa vya baiskeli unaweza piga hela pia!

Nashukuru kwa mchango wako, maana ndio nimeajiriwa sasa hvi huku Kyela nipo maeneo ya boda na Malawi, ninahitaji kufanya nao biashara, vp kuhusu biashara ya mazao kama mchele, mahindi, maharagwe, alizeti n.k?
 
mkuu DZUDZUKU malawi kwenye suala la kilimo cha mazao ya chakula wako vizuri kwenye mahindi , maana ndio zao lao kuu la chakula
kwenye viungo vya chakula mfano nyanya , vitunguu maji/saumu nk hawalimi kwa wingi
tatizo kule ni thaman hela yao inashuka kila wiki, hii inaweza kuwa changamoto kwa biashara toka Nje, pia kule kuna mageti mengi hivyo ujiandae kwa ukaguzi wa mizigo na paspot barabarani
mkuu unawewza ukaenda na kufanya kautafiti kwani mimi nimeondoka huko mwaka juzi, hivyo kunaweza kuwa na mabadiriko ktk mambo mengi hasa baada ya kuingia kwa raisi mwanamke madarakani bi Joyce Banda
nisamehe mkuu sim yang ina uwezo mdogo wa kupost maneno mengi
kama kuna swali unaweza kuniuliza tafadhari!
 
Last edited by a moderator:
sijui kuhusu utaratibu wa kibali cha masuala ya afya
pharmacy , cosmetics na dispencary ni nadra sana sana kupatikana mjini, kwenye makazi ya watu ndo hakuna kabisa kama ilivyo huku , na kama ipo basi ni moja au mbili, hivyo kuwalazim watu kufata hizo huduma mjini
lugha kuu kule ni chichewa, chitumbuka na kizungu, hili nalo ni tatizo kwani sehem nyingine watu hawajui chichewa bali chitumbuka
 
mkuu DZUDZUKU malawi kwenye suala la kilimo cha mazao ya chakula wako vizuri kwenye mahindi , maana ndio zao lao kuu la chakula
kwenye viungo vya chakula mfano nyanya , vitunguu maji/saumu nk hawalimi kwa wingi
tatizo kule ni thaman hela yao inashuka kila wiki, hii inaweza kuwa changamoto kwa biashara toka Nje, pia kule kuna mageti mengi hivyo ujiandae kwa ukaguzi wa mizigo na paspot barabarani
mkuu unawewza ukaenda na kufanya kautafiti kwani mimi nimeondoka huko mwaka juzi, hivyo kunaweza kuwa na mabadiriko ktk mambo mengi hasa baada ya kuingia kwa raisi mwanamke madarakani bi Joyce Banda
nisamehe mkuu sim yang ina uwezo mdogo wa kupost maneno mengi
kama kuna swali unaweza kuniuliza tafadhari!

Nashukuru sana kaka. Majigo
Nilikuwa nafikiria kuwapelekea mchele na mimi nirudi na sukari, unanishaurije kwenye hili?

Kwenye vitunguu nitafanyia kazi na pia kama unaweza kunisaidia sehemu za masoko maeneo ya Malawi kwa biashara tajwa.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru kwa mchango wako, maana ndio nimeajiriwa sasa hvi huku Kyela nipo maeneo ya boda na Malawi, ninahitaji kufanya nao biashara, vp kuhusu biashara ya mazao kama mchele, mahindi, maharagwe, alizeti n.k?

kaka mi nipo tukuyu,tuwasiliane,tunaweza ona tufanyaje kwapamoja..
 
DZUDZUKU sijaizunguka sana malawi kwa sababu nilikwenda kwa maswala yangu binafsi maana bi mkubwa wangu yupo kule
mi natokea boda ya Tz, sijajua utachukua mzigo wa namna gani na utatumia utaratibu gani mpaka kusafirisha eneo unalotarajia kuuzi kwakweli kwa wafanya biashara wa dogo hasa wasio wazoefu ,sukari ya malawi ni kujibebea presha kwani akari wa kila kitengo hiyo ndo imekuwa sehem yao ya kula
wakikamata mzigo wanakutoza hela kubwa ambayo haiendani hata kido na faida utakayoipata baada ya kuuza, lasivyo wanapokonya sukari yote!
 
Last edited by a moderator:
kwa malawi karonga pekee na maeneo ya jirani ndio wazalishaji wakuu wa mchele, tena kipindi cha mavuno watz hushuka mpaka vijijini kufata mpunga na mahindi, wachofanya ni kuexchange vyombo kama sahani , ndoo nk mfanya biashara hurudi na mchele yeye anawapa vyombo
mazao ya chakula yanamlolongo na usumbufu mwingi mpaka kuivusha nchi ya pili, si tz wala Malawi
kwa hali kama hiyo sizani kamabiahara ya mchele itakulipa kule!
 
biashara zinayoingizwa tz kwa wingi toka malawi ni power(pombe kali za packet) pamoja na sukari
wafanya biashara wadogo hubeba mabegi ambayo huwekwa nguo juu kama gersha lakin chinu kunakuwa na mzigo wa maana , wengi wanauzia mbeya kwa wafanya biashara wakubwa wanaosupply dar na maeneo mengine kama arush nk
inahitaji maandalizi na umakini mpaka mzigo ufike tz hasa nje ya kyela
kuepusha usumbufu vijana wa kazi hutumiwa hutumiwa na baadhi ya wafanya biashara kuzisafirisha kwa kutumia baiskeli -wa njia za porini, toka kyela mpaka tukuyu, hapo wanaangalia ustaarabu mwingine ili zifike eneo husika!
 
Back
Top Bottom