Zephania kilango
New Member
- Aug 6, 2014
- 1
- 1
1.BIASHARA.
2.MAFANIKIO KATIKA MAISHA.
3.HITIMISHO
1.0.BIASHARA.
Kuna aina mbalimbali za biashara na aina ya ufanyaji biashara zinazoweza kukukuza kiuchumu. Katika andiko hili litakuonyesha ni nini ufanye ili biashara yako iwe na mafanikio makubwa.
1.1. Kupata soko la biashara yako.
Watu wengi sana wanashindwa kujua umuhimu wa kuandaa soko kwa ajili ya biashara yake, kabla ya kuanza biashara hakikisha kuna uhitaji mkubwa katika soko la bidhaa yako hii itakusaidia sana kunufaika kibiashara.
1.2. Kuhakikisha kuna upatikanaji wa urahisi wa bidhaa yako.
Ili kuweza kufanya biashara kwa rahisi zaidi unatakiwa kuhakikisha kuna upatikanaji mkubwa wa bidhaa yako ambayo itakusukuma kuweza kufanya biashara bila ya kupoteza wateja na kupoteza muda.
1.3. Kuandaa njia bora ya kusafirisha bidhaa yako.
Ili uweze kuwa na biashara nzuri na yenye uwakika unatakiwa kujua utawezaje kusafirisha bidhaa zako kutoka unapozipata mpaka kufika sokoni.
1.4. Faida na hasara ya biashara yako.
Bila ya kuogopa hasara unatakiwa ufahamu nini faida katika biashara yako na nini hasara katika biashara yako ambavyo vinaweza kukupa picha nzuri katika maisha yako ya kila siku.
1.5. Aina ya biashara unayotaka kuifanya.
Aina ya biashara ni moja ya jambo muhimu mno wakati wa ufanyaji biashara, unapofanya biashara yako ni vyema ukaangalia biashara gani ninayokwenda kufanya, je watu wanaipenda, je bidhaa zangu zinakaa mda gani sokoni bila kuharibika, je bidhaa ninazopeleka sokoni hazijapitwa na wakati, je biashara ninayoifanya haiweze kuletewa kikwazo na maisha yangu ama shughuli zangu za kila siku( hapa ngoja nikupe mfano kuna watu wanaanza biashara bila kuzungumza na wenza wao unakuta mke kaanzisha biashara ya baa na anataka yeye kuwa meneja hii kama mwanaume hatokubali inaweza mpa shida sana, au kuna mtu anaanzisha biashara dodoma wakati yeye makazi yake ni daresalaam hili pia linaweza mpa shida na hasara kubwa).
2.0.MAFANIKIO KATIKA MAISHA.
Katika maisha kuna mambo mengi sana ya kufanya ili kuhakikisha tuna maisha bora na yenye mafanikio mambo hayo ni;
2.1.Kuwa na nidhamu ya fedha.
Katika maisha nidhamu ya fedha inahitajika mno ili kuweza kujihakikishia maisha bora wakati wote jamii inapaswa kuwa na nidhamu ya fedha kuhakikisha unafanya matumizi ya pesa pale inapobidi na kuacha kufanya matumizi makubwa ya fedha kwa siku, wiki, mwezi na mwaka.
2.2. Kupunguza au kuacha matumizi yasiyokuwa ya lazima( hanasa).
Watu wengi katika jamii hufanya matumizi yasiyokuwa ya lazima kama vile ulevi,kununua wanawake na kutumia pesa kwa fujo wapo wengi hudhani hanasa ni kuwa mlevi na kununua wanawake tu ila sio hilo tu hata kama ulitakiwa kula chakula cha elfu nane kwa siku wewe ukanunua cha laki moja kwa siku hyo ni hanasa uliweza kula cha elfu kumi na ukala chakula kilichokutosha na kukufaa ukizidisha hapo hiyo pia nia hanasa.
2.3. Kushiriki shughuli za kijamii.
Hii pia uleta mafanikio katika maisha maana hii huongeza ushirikiano wako wewe na jamii katika mambo mablimbali kama vikao, misiba, sherehe, shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa shule na hospitali. Hii husaidia sana kukukuza kiuchumi na maisha kiujumla.
2.4. Kusambaza ujuzi wako kwa wengine.
Katika maisha unatakiwa uwe tayari kutoa ujuzi wako kwa wengine ili uweze kusonga mbele hii pia itakusaidia na wewe kupata ujuzi kutoka kwa wengine.
2.5. Kuwa na uthubutu, kuwa tayari kujaribu haijalishi utafikia wapi.
Hapa ndipo watu wengi katika maisha wanashindwa kupatumia vizuri watu wengi huwa na mawazo ya biashara, mawazo ya kufanya ambayo yange wakwamua kimaisha ila wanashindwa kuthubutu kujaribu kufanya kwa kuogopa kushindwa.
2.6. Kujikinga na maradhi.
kuhakikisha unajikinga na maradhi ambayo yanaweza kupunguza utendaji wako kazi na kukufanya ukatumia fedha kubwa kwenye matibabu, maradhi hayo ni kama ukovi 19, ukimwi, kipindupindu, malaria na magonjwa mengine ya zinaa.
3.0. Hitimisho.
Katika kuhitimisha ni muhimu kufahamu kuwa watu wengi hufanya biashara ili kuhakikisha wanafanikiwa kimaisha jitahidi kujikita katika biashara halali au shuhuli halali karika maisha hii itakuhakikishia mafanikio yenye uwakika na kuacha biashara haramu kama uuzaji wa madawa ya kulevya, biashara bila leseni, kukwepa kulipa kodi na kuuza miili na vilevi ambavyo havijadhibitishwa hii itakurudisha nyuma sana.
Imeandikwa na Zephania kilango.

Upvote
3