Biashara na mahusiano hayatanitesa kweli?

Biashara na mahusiano hayatanitesa kweli?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Wakuu habari?

Mchepuko wangu alinipa wazo moja la biashara, na katika kulitathmini likanishawishi na kunipa matumaini, kwa sababu kama nitalitekeleza kwa ufasaha, linaweza kutengeneza matawi hapa na pale na mwisho wa siku kipato kitaonekana.

Bahati nzuri katika wazo hilo, yuko tayari kulisimamia, na pia ana timu ya kumsaidia kufanya hiyo kazi; kwa upande wangu natakiwa kufungua ofisi tu.

Bahati nzuri tuliafikiana nifungue mimi ofisi na isomeke kwa majina yangu (eqn x co.ltd), yeye awe kama muajiriwa tu, ila faida tuwe tunagawana nusu kwa nusu. Na itamlazimu wakati mwingine kwenda mikoa mingine kwa ajili ya ufunguzi wa ofisi; kwa mazingira hayo atakuwa kama ''operation manager''

Kutokana na hii mikakati kabambe, nimeamua kumzawadia ujauzito ili aweze kufanya kazi kwa uaminifu zaidi, akijua anapambania mali ya baba wa mtoto wake.

Hofu yangu ni kwa huko baadaye, hatoweza kuleta timbwili timbwili kwa bi mkubwa (waifu matirio wangu)?

Ingawa kwa sasa anasema ananiheshimu mimi pamoja na familia yangu, na hatoleta tatizo.

Wazoefu, nipeni maushauri; hii biashara na mahusiano hayata nitesa kweli?

Je, nifanyeje?​
 
Angalia wenzio wanaojua nini maana ya biashara..
FB_IMG_17043131758584302.jpg
 
Hakuna kuteswa wala kuteseka, biashara ibaki kuwa biashara na mahusiano yakabi kuwa mahusiano, hapo ni kuweka msimamo na sheria kali sana.

Yawezekana vijana wa mjini mnaendekeza sana hao binti wavaa vipedo ila, biashara haipaswi kuingiliwa naye hata robo ya chembe ya mchele.
 
Unaweza kuficha ila siku ukifa tu msibani kila kitu kitajulikana ,maiti yako mkeo atatamani aichape viboko
Faida nitakayokuwa naipata, mke wangu pia atakuwa anaipata, pia atajua ni ofisi ya mume wake, kwa kuwa kila kitu kitakuwa kwenye usajili wangu; na yeye atakuwa upande wa ushauri kuhusu mambo ya fedha.
Ingawa mchepuko ataonekana ni mwajiriwa tu, ila atakuwa na mtoto na mimi.​
 
Bahati nzuri yeye atakuwa kama muajiriwa, pia nitajaribu kuweka vijana wa upande wangu katika kupunguza 'risk'
Mapenzi ni maagano kwahiyo usitegemee kuwa wewe utakuwa na sauti kuliko huyo mchepuko kwenye biashara.
Kama alikukuta na hiyo biashara basi atakuwa muajiriwa ila kama mnaanzisha wote hakuna hicho kitu kuwa atakuwa km muajiriwa😁😁😁😁😁
 
Back
Top Bottom