Biashara na mahusiano hayatanitesa kweli?

Biashara na mahusiano hayatanitesa kweli?

Wakuu habari?

Mchepuko wangu alinipa wazo moja la biashara, na katika kulitathmini likanishawishi na kunipa matumaini, kwa sababu kama nitalitekeleza kwa ufasaha, linaweza kutengeneza matawi hapa na pale na mwisho wa siku kipato kitaonekana.

Bahati nzuri katika wazo hilo, yuko tayari kulisimamia, na pia ana timu ya kumsaidia kufanya hiyo kazi; kwa upande wangu natakiwa kufungua ofisi tu.

Bahati nzuri tuliafikiana nifungue mimi ofisi na isomeke kwa majina yangu (eqn x co.ltd), yeye awe kama muajiriwa tu, ila faida tuwe tunagawana nusu kwa nusu. Na itamlazimu wakati mwingine kwenda mikoa mingine kwa ajili ya ufunguzi wa ofisi; kwa mazingira hayo atakuwa kama ''operation manager''

Kutokana na hii mikakati kabambe, nimeamua kumzawadia ujauzito ili aweze kufanya kazi kwa uaminifu zaidi, akijua anapambania mali ya baba wa mtoto wake.

Hofu yangu ni kwa huko baadaye, hatoweza kuleta timbwili timbwili kwa bi mkubwa (waifu matirio wangu)?

Ingawa kwa sasa anasema ananiheshimu mimi pamoja na familia yangu, na hatoleta tatizo.

Wazoefu, nipeni maushauri; hii biashara na mahusiano hayata nitesa kweli?

Je, nifanyeje?​
😅😅😅😅 Scenerio yako na yangu ni pacha wasio fanana. Mimi mchepuko kanipa busness idea, na kuniongezea mtaji juu. Sema yeye hajihusishi nayo kila kitu naendasha mimi fully. Na hahitaji anything in return zaidi ya mimi kuendelea kuwa nae kimahusiano. Ni mke wa mtu na mimi nina mke. Sijajua hii safari itatamatika vipi. Wacha tuone.
 
Huwa naiheshimu hii ID ya huyu bwana. Ila sometimes yes sometimes No. Acha nipite, niepushe fedheha
Sema neno mkuu, elimu haina mwisho, maisha ni haya haya; utajisikiaje pale una miaka 70+ halafu una watoto 20+ wamepanda hewani wanakuzunguka baba yao halafu wote ni wafanyabiashara; utajisikiaje?​
 
Hakuna kuteswa wala kuteseka, biashara ibaki kuwa biashara na mahusiano yakabi kuwa mahusiano, hapo ni kuweka msimamo na sheria kali sana.

Yawezekana vijana wa mjini mnaendekeza sana hao binti wavaa vipedo ila, biashara haipaswi kuingiliwa naye hata robo ya chembe ya mchele.
Nitajaribu kuweka mifumo ya kudhibiti mapato na matumizi
 
Mapenzi ni maagano kwahiyo usitegemee kuwa wewe utakuwa na sauti kuliko huyo mchepuko kwenye biashara.
Kama alikukuta na hiyo biashara basi atakuwa muajiriwa ila kama mnaanzisha wote hakuna hicho kitu kuwa atakuwa km muajiriwa😁😁😁😁😁
Kuna mkataba nitamsainisha; ingawa kwangu muhimu zaidi ni pesa, kama hatosumbua hapo hakuna shida.
 
😅😅😅😅 Scenerio yako na yangu ni pacha wasio fanana. Mimi mchepuko kanipa busness idea, na kuniongezea mtaji juu. Sema yeye hajihusishi nayo kila kitu naendasha mimi fully. Na hahitaji anything in return zaidi ya mimi kuendelea kuwa nae kimahusiano. Ni mke wa mtu na mimi nina mke. Sijajua hii safari itatamatika vipi. Wacha tuone.
Hapo ni pagumu 😀
 
Wale wa kataa ndoa wapo sahihi. Wasikilizwe
 
Mwanamke akishapata pesa hamtaelewana tena

pitia ule uzi wa davis mosha utajifunza, mke wake alikuwa muhasibu kwenye kampuni yake, aliiba billions of money

akaanza kuliwa na mganga na kufikia hatua ya kutaka kumuwekea sumu mume wake
Bahati nzuri hiki ninachokianzisha kitakuwa chini ya mimi na mke wangu, ila huyu mchepuko ataonekana muajiriwa ingawa atakuwa anajilipa vizuri kutokana na faida inayopatikana.
Kwangu nimeona ni fursa kwa sababu ana muda wa kusimamia na kuhakikisha pesa inapatikana.
Muhimu zaidi mi naona, ni bora kuweka mifumo ya kumdhibiti pale atakapotamani kudokoa dokoa​
 
Back
Top Bottom