Biashara na mahusiano kati ya Kenya na Tanzania zimeimarika mara mbili zaidi kutoka 2020

Biashara na mahusiano kati ya Kenya na Tanzania zimeimarika mara mbili zaidi kutoka 2020

Tryagain

Member
Joined
Nov 23, 2021
Posts
73
Reaction score
458
Napitia Takwimu kutoka kenya juu ya kuimarika kwa Biashara kati ya Tanzania na Kenya mara mbili zaidi kutoka Mwaka 2020.

Takwimu kutoka nchini Kenya zinaonyesha Biashara kati ya Tanzania na Kenya zimeimarika zaidi. Thamani ya bidhaa zilizosafirishwa kutoka kenya kuja Tanzania zimepanda kwa asilimia 43.39 ongezeko la dola milion 376.6 kulinganisha na Mwaka 2020 Aghalabu bidhaa ambazo Kenya inauza Tanzania ni za kiviwanda kama vile dawa, plastiki na chuma.

Bidhaa zilizosafirishwa kutoka Tanzania zimepanda sawa na ongezeko la asilimia 95.3 kufanya ongezeko la mara mbili kulinganishwa na Mwaka 2020 Kwa mujibu wa Idara ya Takwimu Kenya zinaoneysha kuwa katika kipindi hicho bidhaa zilizouzwa Kenya kutoka Tanzania zilikuwa zenye thamani ya dola milioni 267.47 hii ikitajwa kuwa ni mara ya kwanza Tazania kuongoza katika biashara baina ya nchi mbili.

Kutoka January hadi September 2022 imeongezeka mara mbili kwa dola milioni 499.3

Viwanda vya Kenya hununua kutoka Tanzania nafaka, mbao, mboga chakula cha wa nyama na bidhaa za karatasi.
 
Back
Top Bottom