Biashara na malipo ya kodi (TRA)

Biashara na malipo ya kodi (TRA)

Simple on looking

Senior Member
Joined
May 27, 2014
Posts
100
Reaction score
34
Habari zenu Wakuu nataka kuanzisha biashara ila sina elimu yoyote kuhusiana na namna ya ulipaji wa kodi ya mapato. Kwa wenye uelewa naomba kuelimishwa kuhusiana na ulipaji wa kodi ya mapato.

Miongoni mwa maswali ninayo jiuliza ni:-
1. Ni biashara gani inayokupasa upate leseni ya biashara na ulipie kodi ya mapato?
2. Je, Unahitaji Kua na mtaji kiasi gani ili upate leseni ya biashara?
3. Kodi ya mapato inalipwaje?
4. Ni lazima leseni ya biashara kutoka TRA uipate sehemu (mf. Mkoa) unayotaraji kuanzisha biashara?.

Naomba kufahamishwa hayo na mengineyo yanayohusika na biashara na ulipaji wa kodi ya mapato.

Shukrani.[emoji120]
 
Simple on looking

Salama Mkuu

Kwanza naona unachanganya masuala ya leseni na ulipaji kodi TRA (no. 4 ktk andiko lako)
Leseni na ulipaji kodi vinatolewa ktk mamlaka mbili tofauti, yaani namba maalumu ya utambulisho wa mlipa kodi ie TIN inatolewa TRA wakati leseni ya biashara inatolewa ktk ngazi ya manispaa au wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji. Fahamu hili

1. Ulipaji kodi (TRA)
Si biashara zote zinastahili kulipa kodi. Biashara yenye mauzo chini ya milioni 4, hii kisheria haitakiwi kulipa kodi. Hivyo basi angalia biashara yako ina mauzo kama au chini ya mil 4?
Unatakiwa kusajili kwanza namba maalum ya mlipa kodi (TIN) ktk odisi zilizo jirani na eneo unalofungua biashara.

2. Awamu za kulipa kodi
Kwa mwaka kodi ya mapato hulipwa ktk awamu nne ie Machi 31, Juni 30, Septemba 30 na Disemba 31. Hizo tarehe maana yake mwisho wa kulipa kwa kila awamu

3. Leseni ya biashara
Hii hupatikana kutokana na makundi. Ambapo leseni za kundi A hutolewa wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji na kundi B hutolewa Manispaa.
Kuwa na leseni kwa biashara yako itategemea, lkn kwa biashara ndogo sana, au za kuhama hama kama machinga huhitaji kuwa na leseni

Kwa kifupi ni hayo, jipime
 
Afrolink-Tz Consult Ltd

Mkuu naona umwnchanganya hapo unaposema biashara ya chini ya 4M haitakiwi kulipia Kodi..sasa mimi nabiashara yenye thamani kama 1M na sina leseni wala sijalipa kodi ndio nilikuwa najiandaa kuanza fanya taratibu..sijaelewa inakuaje hapo
 
Anamaanisha mauzo yote kwa mwaka yakiwa chini ya 4M ndio haulipi kodi sio anamaanisha mtaji ulionao.
 
sasa ikiwa mauzo kwa mwaka mzima utapimaje hayo mauzo bila kufanya kwanza iyo biashara kama miaka miwili kuipima.
Utakadiria tu. Kwa wastani. Mfano siku nzuri unaweza uza kiasi gani na mbaya kiasi gani, halafu fanya wastani wake. Baada ya hapo zidisha kwa siku 26 thwn kwa miezi 12 kwa wepesi, utajua mauzo kwa matarajio yako

Mfano: tuseme mauzo kwa mwaka ulijikadiria ni mil 3.6/mwaka. Ss biashara ikawa vema hadi ktk miezi 9 tu ya mwaka umefikia mil 4.5. Inabidi uwe mwaminifu kajaze fomu ya makadirio ya kodi ulipe 150k ya kodi kisheria (note mauzo kati ya mil 4 hadi 7.5 kodi ni 150k)

Na kama ulijikadiria mauzo juu, lkn biashara imekuwa sio kwa mwaka, andika barua kuonyesha hili na kumbukumbu uattach. Hii ina maana kodi yk uliyolipa itasogezwa mbele muda ujao
 
Serikali iwape ahueni wafanyabiashara wadogo, wafanye mapato kuanzia hata million 20 ndo waanze kulipa kodi.
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Back
Top Bottom