Simple on looking
Salama Mkuu
Kwanza naona unachanganya masuala ya leseni na ulipaji kodi TRA (no. 4 ktk andiko lako)
Leseni na ulipaji kodi vinatolewa ktk mamlaka mbili tofauti, yaani namba maalumu ya utambulisho wa mlipa kodi ie TIN inatolewa TRA wakati leseni ya biashara inatolewa ktk ngazi ya manispaa au wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji. Fahamu hili
1. Ulipaji kodi (TRA)
Si biashara zote zinastahili kulipa kodi. Biashara yenye mauzo chini ya milioni 4, hii kisheria haitakiwi kulipa kodi. Hivyo basi angalia biashara yako ina mauzo kama au chini ya mil 4?
Unatakiwa kusajili kwanza namba maalum ya mlipa kodi (TIN) ktk odisi zilizo jirani na eneo unalofungua biashara.
2. Awamu za kulipa kodi
Kwa mwaka kodi ya mapato hulipwa ktk awamu nne ie Machi 31, Juni 30, Septemba 30 na Disemba 31. Hizo tarehe maana yake mwisho wa kulipa kwa kila awamu
3. Leseni ya biashara
Hii hupatikana kutokana na makundi. Ambapo leseni za kundi A hutolewa wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji na kundi B hutolewa Manispaa.
Kuwa na leseni kwa biashara yako itategemea, lkn kwa biashara ndogo sana, au za kuhama hama kama machinga huhitaji kuwa na leseni
Kwa kifupi ni hayo, jipime