iMind hata mimi yamenikuta nimejitahidi karibu mwaka na nusu sasa ila kwa sasa nimemwaga manyanga yaani nimeshindwa kwanza wafanyakazi pasua kichwa unamtumia nauli anakaa miezi miwili anadai kuondoka anaondoka anaacha sehemu ya biashara imefungwa mpaka ukija kufungua tena wateja washasahau khs uwo wizi ndio usiseme mpaka najiuliza wenzangu wanaweza vipi mbona mimi nashindwa kabisa jamani nao pia wanategemea wafanyakazi kama mimi jamani mwenye maujuzi atujuze na sisi nimeshindwa biashara ndogondogo ingawa nilikua na fursa nzuri sana mtaani kwangu ila naona nimeshindwa kabisa
Sasa Dada yangu Sharifa kwenye biashara kuna sehem mbili za kuangalia.
Tatizo la muajiriwa na muajiri.
Sasa maelezo yako hapo juu ni kwamba muajiriwa hana tatizo ila wewe muajiri ndio tatizo na ndio janga.
Sasa dawa ya tatizo lako unayo mwenyewe.
Inakuwaje biashara inayokulipa vizuri mtaani kwako halafu usema inakushinda kwa kudai wafanyakazi pasua kichwa.
Mbona wakati walipokuwa wakifanya biashara hadi wewe kugundua inakulipa hukusema asante kwao na badala yake ukala bata peke yako.
Kama biashara yako inakulipa vizuri kama umevyosema basi ajiri watu wawili hasa kipindi huyo anapokuwa anaeda likizo au anaumwa.Watu watu kibao unaweza kuajiri kwa muda wa mwezi,ni bora umlipe pesa nyingi lakini sehem ya biashara iwe wazi.
Na pia tujifunze kutoa motisha kwa wafanyakazi wako,kama mfanyakazi utampa motisha nzuri wakati wa kurudi likizo basi anaweza hata mwezi usifike akarudi kazini.Kuna wafanyakazi wangapi humu wapo likizo lakini wanaenda kazini hata kupiga story kulingana na mazingira ya kazi na muajiri wake.
Nakumbuka mie wakati naenda nyumbani kuoa,muajiri wangu alinipa Ticket ya ndege kwenda na kurudi na wife.
Sasa lengo sikwamba ananipa offer bila malengo,la, lengo lake ni kwamba nikitumia usafiri wa train ni siku mbili,na pia lazima ni book kwa wiki kadhaa ndio nipate.Sasa akajua kwamba kama akinipa bonus hiyo lazima nitakuwa na hashuo la ndege na nitarudi mapema.Na kweli trip hiyo ndio ilikuwa ya Kwanza wa Wife kupanda ndege.Ikanipa maujiko kweli.Mtaani wakajua Bakhressa nimeenda kuoa.Mwisho wa Reli tena,siunajua tena .Mme kaja kwa ndege na karudi na mkewe kwa ndege.
Sasa hapo iliniwezesha kurudi ndani ya wiki moja tu na kuanza kazi kama kawaida kwa amani na furaha,na kumshukuru sana boss kwa kunipatia tickets za ndege kwenda na kurudi,lakini hapo ujue ni kwamba nafasi yangu ni muhim sana na ilikuwa ni msimu wa kazi.Sasa alijua kabisa kwamba lazima acheze na rasilimani mtu.Is very technical
Sasa kama wewe sehem inalipa unashindwa ku pick staff mwingine?yaani jinsi watu wanavyohaha kutafuta ajira kesho tu ukitangaza unawapata.
Na hii inaoneysha kwamba hata mfanyakazi wako alikuwa akiumwa basi unafunga biashara,
Kwa ufupi tangu nazaliwa ndio naona na kusikia biashara hiyo yako inafungwa mtu akienda likizo.
Sasa kwa maelezo yako hapo juu,tatizo ni wewe mwenyewe na sio muajiriwa wako.