Biashara ndogondogo nyingi zinafanywa na watu wasio makini katika fedha

fixed_fangs

Member
Joined
Oct 30, 2016
Posts
73
Reaction score
85
Nimeshuhudia mara kadhaa wahudumu wa hizi biashara ndogondogo, ambazo hufanywa na watu wengi, hususan akina mama - hufanya makosa ya kimahesabu sana hasa kwenye kurudisha chenji!

Leo asubuhi, kwa mfano, nimenunua mihogo ya 400/= kwa mama mtaani na kumpa buku. Chenji ananipa sarafu alfu na mia nne! Nikamrudishia alizonizidishia. Sasa, hapo nilikuwa mteja peke yangu, je kungekuwa na foleni?
Na hii si mara yangu ya kwanza kushuhudia "hii kitu" kwa watu na nyakati tofauti tofauti hapa jijini.

Nadhani iko shida ya uelewa na umakini katika hizi shughuli hasa ukizingatia wanazozifanya ni watu wenye weledi mdogo kwenye "basics" tu za biashara. Labda ndiyo maana biashara nyingi ndogo hazidumu na mwisho wa siku tunasema kuna "mkono wa mtu" kumbe tuna"jiloga" wenyewe!

Je umewahi kutana na mfanano wa kitu kama hiki? Na nini kifanyike kuwasaidia hawa watu?

Ni hayo tu.
 
Nafkiri ni bahati mbaya tu inatokeaga,
Mtu hawezi fanya biashara kama hta mahesabu madogo ya kurudisha chenchi yana msumbua.
 
hata wenye biashara kubwa huwa inatokea wanakosea kurudisha chenji.
Vipi angekurudishia chenji pungufu ungemuchukuliaje?
 
Pamoja na umakini lakini na elimu japo kidogo short course inahitajika Matharani jinsi ya kumjali mteja na stock mgt! Huwa nashangaa kuona Mtu anagombana na wateja [emoji87][emoji87][emoji87] ulimwengu huu wenye ushindani unaanzaje kumgombeza mteja? Acha yeye akugombeze lakini siyo Wewe mtoa huduma ndo uwake! Siyo Siri huwa nawaonea huruma sana! Yani Mtu hajui thamani ya mteja yeye anaona kumpoteza siyo shida! Kuna mafundi Bomba wangapi wako vijiweni wanatafuta kazi Wewe unampata halafu unashindwa kuchukuliana nae [emoji87][emoji87][emoji87]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…