fixed_fangs
Member
- Oct 30, 2016
- 73
- 85
Nimeshuhudia mara kadhaa wahudumu wa hizi biashara ndogondogo, ambazo hufanywa na watu wengi, hususan akina mama - hufanya makosa ya kimahesabu sana hasa kwenye kurudisha chenji!
Leo asubuhi, kwa mfano, nimenunua mihogo ya 400/= kwa mama mtaani na kumpa buku. Chenji ananipa sarafu alfu na mia nne! Nikamrudishia alizonizidishia. Sasa, hapo nilikuwa mteja peke yangu, je kungekuwa na foleni?
Na hii si mara yangu ya kwanza kushuhudia "hii kitu" kwa watu na nyakati tofauti tofauti hapa jijini.
Nadhani iko shida ya uelewa na umakini katika hizi shughuli hasa ukizingatia wanazozifanya ni watu wenye weledi mdogo kwenye "basics" tu za biashara. Labda ndiyo maana biashara nyingi ndogo hazidumu na mwisho wa siku tunasema kuna "mkono wa mtu" kumbe tuna"jiloga" wenyewe!
Je umewahi kutana na mfanano wa kitu kama hiki? Na nini kifanyike kuwasaidia hawa watu?
Ni hayo tu.