round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 933
- 3,051
Hawa motivational speakers ni watu wanaokula kwa kuuza matumaini yaliyovuka uhalisia kwa watu wanaojitafuta au kukata tamaa.
Unapoingia kwenye biashara kwenye nchi kama Tanzania umeingia kwenye competition ua kikatili sababu mazingira yamejaa rushwa, siasa, ndumba, sheria legevu, n.k. usipokuwa makini UNALALA NJAA !
Nimeshuhudia vijana wengi wakiingia kwenye biashara kwa matumaini makubwa na upepo waliojazwa na motivational speakers, Biashara ni competition ya kikatili mno, Ili moja apate lazima mwengine akose, Mwezanzako anatoboa pale wateja wako wakiacha kuja kwako wanaenda kwake !! Nimeshaona watu wakilala njaa, Nimeona watu waliofanikiwa kibiashara miaka kadhaa wanafirisika wanaanza kupanda bajaji au kutwanga mguu, watu wanachizika kwa msongo wa mawazo, n.k.
Upo ka location kanakuingizia pesa, watu wanakuchora hata mwezi hauishi nao wanafungua biashara kama yako pembeni yako COPY PASTE tena wanaweza kuingia kwa kuuza kwa bei rahisi kukuzidi, taratibu wateja wanaanza kukuhahama.
Umeagiza mzigo kwa kujumua elf 8 kwa piece unaenda kuuza reja reja elfu 10 kwa piece, Mwengine mzigo huo huo anauingiza kwa magendo au kwakutoa rushwa halipii kodi anauza elfu 7 kwa piece, wewe ukiuza hio bei ni hasara.
Unapata wazo jipya la biashara, unatafuta benki ya kukukopa, mfadhili au mshirika. kabla hujajua, wanakulaghai na kufungua biashara yao kwa kutumia wazo lako, sheria zimelegea kukulinda mwenye wazo.
Unafuata taratibu zote halali za biashara, unalipa kodi zote, lakini wenzako wanatoa rushwa ama wana watu wao wa kuwasaidia kukwepa kodi. Mwisho wa siku, wanauza kwa bei rahisi na wanakufanya ushindwe kuendelea.
Unapata dili la kusambaza bidhaa kwa kampuni fulani, unakopa fedha ili uweze kuwaletea mzigo. Baada ya kusambaza, wanagoma kulipa au wanachelewesha malipo, huku wewe unakimbizana na maafisa wa benki .
Unawaajiri watu, unawafundisha mbinu zako za biashara, unawaamini. Baada ya muda, wanakusaliti na kufungua biashara kama yako, wakichukua wateja wako kwa kutumia ujuzi uliowafundisha.
Umepanga eneo lenye kodi ya laki 2 biashara inakua, mwenye nyumba anaona unapata pesa, ghafla anakwambia kodi imepanda mpaka laki 5 au anakuondoa ili akodishe kwa mwingine kwa bei ya juu zaidi.