Kumi4
Senior Member
- Nov 4, 2021
- 101
- 106
Sijui niseme vipi ila kiukweli Biashara sio kitu cha kila mtu, kuna vivumbi vya kila mtindo viko humo ndani, nisiwachoshe niwape misiba yangu miwili mitatu kwanza:-
Mwaka 2021 kibarua changu kiliingia mbolea na kashikashi zikastawi kama hazina akili nzuri sasa bana ukilinganisha na mshahara wenyewe ulivyo ni wa mbuzi nikajikuta mpaka narudi mtaa sijajiweka sawa ile kiviile, nilijipiga piga nikanunua mashine ya juice ya miwa na kutengeneza banda la chuma la kisasa la futi 6 kwa 7 nikalitega mahali.
Nina mwanangu mmoja yeye hakuwahi kubahatika kuajiriwa so akaniomba awe anazugazuga pale nikasema fresh nikajikuna kuna nitafuta laini za Nini pesa nikaweka na kamataji uchwara kama 300,000 tu hivi. Location ilikuwa ni sokoni mjini Mbagala pale. Basi yule mwamba akawa anauza vifurushi tu mwezi ukiisha faida inakuja 10,000 na sio mbali saana na hapo (Ikfahamike kuwa hapo mashine ya juice iko tu ndani maana ilikosa mtu wa kuiendesha).
Gharama za uendeshaji zikawa kubwa pamoja na kwamba tulikuwa hatulipi kodi ni ushuru tu poale sokoni 500 kwa siku. Mwamba akaja akakacha baada ya msingi kwenda kwa jamii. Nikasema fresh.
Sasa basi ndio nikaingia mtaani rasmi na kuamua kuifufua mashine ya juice 'niutesti' upepo. Nilipoanza tu raia ninaokaa nao home wakawa wananisihi kuwa nisikae kimama maana lile ni eneo la soko na kama mnavyojua biashara kwenye masoko zinahitaji UTU UZIMA, mi nikasema fresh najilipua hivyo hivyo, eeh! Shule hapa ndipo ilipoanzia, enewei ngoja niwahishe futari kwanza kwa mama Saidi nikipoa narudi tena kujazia.