Biashara, Nyumba au Gari?

Biashara, Nyumba au Gari?

Majaribu2013

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
952
Reaction score
1,049
Habari za Muda Huu Mkuu?
Kumekuwa na mijadala mingi sana katika jamii hasa kwa vijana wanaopambani kutafuta maisha. Jambo lenyewe liko hivi:-

Mara nyingi vijana wanapoanza kuona mwezi {pesa} zinakuwa ndogo kiasi kwamba hazitoshelezi kufanya mambo yote tajwa hapo juu. Shida inakuja hapa je kama kijana kapata let say Million zake 20, aanze na lipi? Ajenge nyumba? Aanze biashara? au anunue gari?
Karibuni ubaoni kwa mawazo mbalimbali.
 
biashara ndo kipaumbele, na faida kwenye biashara inaleta vyote hivyo
 
Biashara ipi kwa mfano maana zipo biashara za kukupa nyumba, gari nk, pia zipo biashara za kufanya upunguze ukali wa maisha yani unapata pesa ya kula, kulipa kodi ukisema uifanyie mambo makubwa hiyo biashara inayumba kwaiyo mnaposema biashara muangalie biashara ipi
 
Kwanza uyo kijana lazima afahamu mil 20 si pesa nyingi sana ni ya kawaida sana.
Ningemshauri kama ifuatavyo:
Aendelee kuweka bidii kwenye hiyo kazi iliyompatia mil 20 asikimbilie kujenga kwa sababu mil 20 kama hana kipato cha uhakika hatatimiza lengo la kujenga.
Asikimbilie kwenye kuiwekeza mil 20 kwenye biashara kwa sababu biashara haina gurantee 100% atumie kiasi kidogo tu labla mil 4 kufanya biashara ndogondogo.Atafute viwanja 2 anunue kwa ajili ya kiwanja kimoja kujengea baadae na kingine anaweza kukiuza akaongezea kwenye ujenzi.

Aachane na mawazo ya kununua gari kabisa mpaka awe na vyanzo vya uhakika vya kumuingizia pesa ili gari lisigeuke kuwa liability.

Note:kwangu ni ulimbukeni kwa kijana anayeanza maisha kukimbilia kununua gari.kujijenga kiuchumi kwanza ni muhimu sana.
 
Ningekua mimi ndo kijana mwenye millioni 20 huu ushauri ningeufatisha hadi nukta
 
Mi nashauri kuanza na biashara kwani ikienda vzr ndyo itakayofanya hayo mengine yote kama ni gari au nyumba, ila kama ni mimi nimepata hizo M 20 ningetafuta kiwanja hata cha M 5 or 7 for future afu hizo pesa zingine ningechukua kiasi mfano m 6 naweka kwenye biashara ili nione uelekeo wake na kama itaenda vzr basi ntaongezea hiyo nyingine as a working capital. Hivo ntakua sehemu nzuri na nikipata faida kiasi najengea, nanunua gari nyingine naongezea kwenye hiyo biashara ili izidi kukua. At the end ntakua na biashara, nyumba, gari habari ya vyuma kukaza ntakua naskia kwa wengine tuu
 
Kwanza uyo kijana lazima afahamu mil 20 si pesa nyingi sana ni ya kawaida sana.
Ningemshauri kama ifuatavyo:
Aendelee kuweka bidii kwenye hiyo kazi iliyompatia mil 20 asikimbilie kujenga kwa sababu mil 20 kama hana kipato cha uhakika hatatimiza lengo la kujenga.
Asikimbilie kwenye kuiwekeza mil 20 kwenye biashara kwa sababu biashara haina gurantee 100% atumie kiasi kidogo tu labla mil 4 kufanya biashara ndogondogo.Atafute viwanja 2 anunue kwa ajili ya kiwanja kimoja kujengea baadae na kingine anaweza kukiuza akaongezea kwenye ujenzi.

Aachane na mawazo ya kununua gari kabisa mpaka awe na vyanzo vya uhakika vya kumuingizia pesa ili gari lisigeuke kuwa liability.

Note:kwangu ni ulimbukeni kwa kijana anayeanza maisha kukimbilia kununua gari.kujijenga kiuchumi kwanza ni muhimu sana.
Unaonekana una mawazo ya kizamani sana. Kuwa na gari sio ulimbukeni. Hasa kwa miji kama Dar. Labda uwe unakaa mkoani
 
Vizuri akausikiliza moyo wake unasema nn na pia yeye alizitafuta za kufanyia nn kama ni za machimboni awe makini zaidi mana hizo zinakatikaga kiutani utani kwenye biashara afanye utafiti wa kutosha na asiingie na pesa yote aanzie chini 2m atafutie uzoefu pia akumbuke miluzi mingi inampoteza mbwa
 
Mkuu izo pesa kwanza tungefaham chimbuko lake tungejua tuanzie....Kama Umepewa mkopo so kuna marejesho na riba....kama umepewa na ndugu/familia basi ahueni yako....kama umebet au kuiba dah hapa kuna kahatari....Iko hivi Kama ulipewa na ndugu basi idea ya biashara iko vyema zaidi..Naamanisha Pesa inatakiwa izalishe na kama utajenga basi nyumba iwe ya biashara(kupangisha frem/Chumba,gesti).Kama utanunua gar basi pia liwe la biashara (tax,noah nk)....Kinachotakiwa ni pesa iendelee kuwepo katika namn ya mtaji au mali ili izalishe zaidi ukizingatia hutopewa/ipata tena kwa namna iyo ya awali....Kama imetoka kwenye biashara basi iyoiyo iendeleze ama kufungua matawi.Pesa ukisha ipatia mzunguko/biashara basi faida itakuletea hayo mengine...
 
Jenga nyumba ya kupangisha biashara kwa sasa hapa nchini NI KICHOMI AMBACHO HAKIJAPATA DAWA
 
Back
Top Bottom