nicholaus mbwambo
JF-Expert Member
- Apr 19, 2018
- 287
- 233
Biashara nzuri ni ile unayoifanya kwa moyo bila kushinikizwa na faida wala makundi ya rafiki yaani kuiga kutoka kwa marafiki.
Vijana wengi hasa wahitimu sio kama hatuwezi kufanya biashara, la hasha na wala sio kama hatuna mitaji hapana shida ni kuwa na mawazo ya biashara hasa biashara ndogo ndogo ,narudia tena kuwa na wazo la biashara hasa biashara ndogo ndogo,
Katika mzunguko wa biashara ni rahisi sana kuua biashara yenye mtaji mkubwa kuliko mtaji mdogo maana uendeshaji wake ni tofauti.
Vijana wengi tuna mawazo ya biashara tena zenye faida lakini shida ni muamko wa kufanya baishara hizo yaani roho ya uthubutu ya kufanya ni biashara hasa kwa kufananisha na elimu tulizonazo.
Biashara nyingi hasa za vijana kama mimi zinafeli kutokana kukosa urithi wa kufanya biashara. Siku hizi tunapenda online business yaani tulale home tutegemee biashara ikue.
Ni kweli lakini swali la kujiuliza ni wateja wangapi wanaokuingzia kipato kupitia online marketing?
Matumaini ya wengi ni kuwa marafiki tulionao ndio wateja wetu wa kwanza wakati sio maana. Utafiti uliofanywa na Kitengo cha Masoko Marekani 2010 walisema biashara nyingi zinakufa kwasababu ya uhusiano wa karibu na marafiki.
Wengi tunashindwa kuanzisha biashara kwa sababu ya muda na hasa kukosa muda wa uvumilivu pia kukosa nidhamu katika mitaji na mauzo tunayoyapata.
Vijana wengi tunaamini kufanya biashara ni tafsiri ya kukosa ajira au kutokuwa na elimu ndo maana hata tukifanya biashara fikra zetu zinadumaa kwa kufanya biashara bila ujuzi na ufanisi wa kuikuza.
Nilibahatika kukutana na kijana mwenzangu mmoja akiniomba ushauri kuwa afanye biashara gani swali rahisi na ushauri wangu mkubwa nilimjibu kwa haraka na kwa kutofikiria kwa kumwambia afanye biashara ya kuuza maandazi, Ilihali akili yangu ilinituma kumpima imani na utayari wake wa kufanya biashara hasa ndogo ndogo.
Alinijibu hawezi uza kwasababu haiendani na elimu yake. Najua na nina imani wengi wetu tuna mawazo mengi ya biashara yawezekana ni mapya kwa eneo husika au sura za watu au mengine, lakini hatujui kwanini roho hazipendi na bado hazijafunguka kufanya biashara.
Majibu ni mawili moja bado tuna mawazo yaliyofungwa, na pili kuwaza baishara ni faida na si vinginevyo.
Malengo makuu matano ya mafanikio katika maisha ya binadamu:
1. Kiafya
2. Kiroho
3. Kifamilia
4. Kibiashara/Uwekezaji au Fedha
5. Kazi
Jiwekee malengo kwa mpangilio unaohisi wewe ni sahihi kufanikisha na ni muhmu kwa maisha yako.
Kila lengo ni muhimu lakini kuna la muhimu zaidi, then yagawanye malengo hayo makuu wa kila moja katika makundi matano yaani malengo madogo madogo then anza kufanya na kujituma katika malengo uliyojiwekea.
Kila lengo ni muhmu kwa mafanikio. Pia katika maisha ifike wakati jifunze kuwa na marafiki chanya.
Simaanishi uwe na maadui au uanze kuringa na majigambo la hasha, bali chagua marafiki wenye kuleta chachu ya mafanikio, yaani marafiki ambao wapo tayari kukuambia ukweli hasa pale unapokosea na kwenda tofauti hasa ule ukweli unao au utakao kuuma na ikiwezekana utengeneze jeraha moyoni mwako na marafiki hao wawe changamoto ya mafanikio yako.
Pia na muhimu, kwa kuzingatia na kuheshimu imani na dini za kila mtu katika maisha yako, kumbuka kutoa "zaka" kwa imani na kwa kuweka nia na kutaja maombi yako makuu hasa hayo matano kwa chochote unachokipata katika biashara yako, kazi yako,n.k kwa imani.
Maisha yako yatabadilika.
Itaendelea