Nimeamini ndiyo maana wafanyabiashara huwa ninawaona wachoyo hawatoi kumi yao. Biashara ina tuvimambo fulani fulani huwezi kuvikuta kwenye kuajiriwa.
Aisee,biashara si jambo jepesi, yaani kujiajiri kwa kifupi fikiria kuamka saa 9 usiku kufata samaki Feri. Halafu kupeleka uji usiku wa manane Sterio kuwauzia wanaoshusha mzigo, mlioajiriwa heshimuni wafanyabiashara aisee.
Waliojiajiri muwaite tu wachawi
maana wanayofanya ni miujiza, kwenye ajira huwezi kuta. Yaani wewe saa 10 tu mchana upo njiani au ushafika home, hadi kesho saa 2 au moja na nusu asubuhi.
Kwenye biashara hakuna kulala na ukilala unapiga tu mahesabu kichwani.