USHAURI:...
milioni 8 ni ndogo kama huna business plan nzuri na ni nyingi ukifanya Vise versa...
Kwa kuwa unataka kuwekeza kwenye vyombo vya moto, nunua Bajaj... Usinunue hivi Bajaj zenyewe zenye jina hilo hilo Bajaj, nunua inayoitwa TVS KING. Ina nguvu na Injini yake inavumilia angalau kuliko hiyo 4 stroke ya Bajaj...
Hesabu yake kwa siku huwa ni kuanzia 15 hadi 20 kulingana na makubaliano na dreva . So kwa wiki ni 100,5000 hadi 140,000. Hapo ni kufanya kazi Jumatatu hadi Jumapili... Ili kutunza chombo inashauriwa angalau kila baada ya wiki mbili kumwaga Oil.
Na kila jumapili chombo ipumzike na dreva pia apumzike maana kazi inachosha hii.
Pia kwenye service mnaweza kukubaliana... Kwamba kifaa kilicho chini ya 10000 iwe juu ya dreva, ikizidi hapo juu ya bosi... Au akawa anakupa hesabu ya siku 5,siku ya sita anatafuta hela ya service na siku ya saba ni mapumziko! Bajaj (TVS King) itakaa mpaka ichoke hela yako isharudi.
Na Bajaj ni uhakika maana lazima abiria wapande tu mjini hapa, na ukiwa na dreva mzuri mwaminifu utaipenda Bajaj.
Ni hayo tu!!
CHAGUZI ZA HESABU.
1. 15,000/day x 6days =90,000x4weeks= 360,000 (month).
2. 18,000/day x 6days =108,000x4weeks=432,000(month)
3. 20,000/day x 6days =120,000x4weeks =480,000 (Month).