Biashara Tabora- Mtaji Milioni 14

Biashara Tabora- Mtaji Milioni 14

Danny Massawe

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2012
Posts
1,297
Reaction score
758
Salaam wadau!

Naandika kwa kifupi ili nieleweke na nisiwachoshe. Naomba wenye uzoefu na Tabora wanisaidie.

Mimi ni mtumishi ambaye nimeamishiwa huu mkoa kutoka Arusha, huko nilikuwa nafanya kazi ya Serikali lakini pia nilikiwa nafanya biashara ya duka ili kuweza ku boost uchumi wangu.

Sasa nimefika hapa nimeuza lile duka kule Arusha nikapata milioni 14 ambayo ndio mtaji nilionao ambao natafuta fursa ya kuwekeza.

Sipendi kufanya biashara kama niliyokuwa nafanya Arusha maana ni mazingira tofauti, hivyo nipo kwenye utafiti wa kuangalia niwekeze kwenye nini maana sitaki kukurupuka.

Naomba wenye uzoefu na huu mkoa mnisaidie. Ahsanteni na Mola awaepushe na corona popote mlipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wekeza kwenye ufugaji wa nyuki mkuu.tafuta pori weka mizinga yakutosha rina asali mangi.

Sent using Jamii Forums mobile app
ni wazo zuri lakini kabla ya hapo ajishughulishe na kuuza asali na nta ili aanze kuzoea mazingira polepole.

Mimi sio mwenyeji wa kule ila kuna ndugu zangu wapo kule wananiambia kule asali inalipa huwa kwa mfano wananunua kwa elfu 40 kwa dumu la lita 20 halafu wanahifadhi ndani kwa miezi kama mitatu halafu wanakuja kuuza kwa elfu 80 au zaidi kutegemea na jinsi soko lilivyo.
Kwa hyo unanunua kwa wingi wa mtaji wako na kunakuwa na mawakala wanazikusanya kwa wingi na kuzipeleka kwa matajiri kama akina MO.

Na Nta pia mtindo ni huo huo watu wanatoboa.
Kwa hiyo kama una hizo milioni ulizonazo chukua kidogo tu kama milioni 4 tu uanze kuifanya hiyo biashara na kuizoea pole pole hela zilizobaki weka benki zitakuja kutumika mbeleni kwa ajili ya kuongezea mtaji polepole.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa ushauri, Naomba mawasiliano na mtu ambaye yupo vijijini ambae anaweza nitafutia mzigo

Back
Top Bottom