Biashara utumwa ndani ya U.S.A katika sura mpya?!

Biashara utumwa ndani ya U.S.A katika sura mpya?!

Rapherl

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Posts
3,504
Reaction score
2,256
Wanajamii,

Kanye West juzi katambulisha nyimbo mpya "New Slave" kutoka albamu ya Yeezus itatoka June 18,katika nyimbo hiyo kuna Bars kama;

Meanwhile the DEA/
Teamed up wit the CCA/
They tryna to lock N****s up/
They tryna to make new slaves/
See that's a private owned prison/
Get your piece today

CCA ni Correction Corperation of America,anasema hizo Prison Industrial system na DEA wanashirikiana katika kukamata na kuwafunga watu weusi wa Amerika,kwamba imekuwa ni biashara inayofanywa na hawa watu ili kupata "Cheap labor" ndo maana wengi wanapewa "double digits sentence"akitoka uko ameshazalisha vya kutosha!

Pia Yeez kaliongea kwenye "Crack Music",Immortal Technique-Peruvian Cocaine,na Raptivist wengine kama KRS-One,Cunninlyngnists,Dead Prez-Thats War na Know your Enemy,Lupe fiasco,X-Clan,Talib Kweli,Killer Mike kwenye nyimbo "Reagan" ya 2012 anasema;

Thanks to Reagonomics,prisons turned to profits/
Because free labor is the cornerstone of U.S economics/
Cause Slavery is abolished unless you are in Prison/
You think am b****ing then read the 13th Ammendment/
Involuntary servitude and Slavery it prohibits/
That's why they giving drug offenders time in double digits

Imekuwa ikisemwa muda mrefu kwamba biashara ya usafirishaji madawa ya kulevywa inafadhiliwa na Marekani kupitia shirika lake la kijasusi CIA tukiangalia kama ile "Watch Tower missions" ambayo CIA na MOSSAD kwa kushirikana na Colonel Manuel Noriega mpaka alipokuja kuuawa walikuwa wanafanya usafirishaji wa madawa kutoka Bogota to Panama to U.S,kuna ops kama"Golden Triangle of southeast Asia and Pakistan", hizi pesa zilienda kuweka kwenye mabenki Panama,Switzerland na US

The Huffington Post kwenye article ya tarehe 18 April 2013 yenye kichwa:The drug war and mass incarceration by numbers wanasema idadi ya watu waliofungwa mpaka mwaka 2010 ni milioni 2.2 na idadi hiyo NUSU yake(50perc) ni AFRICAN-AMERICAN!

Chat waliotoa American Civil Liberities Union inaonyesha idadi ya Wafungwa wa kesi za madawa inazidi kuongezeka kila mwaka,japo inasemekana idadi kubwa ya Wauzaji na watumiaji wa madawa hayo ni White people!

--Je,ni kweli Serikali ya Marekani na Magereza wanafaidika na hii "cheap labor"?,ni aina mpya ya Slavery kutoka kwa individual Slaveholders to Governments na Collectives nyingine zenye authority to lock people up(refer 13 ammendment)?!

--Kama CIA ndo wanashiriki katika hii Biashara na Serikali inatumia zaidi ya $51 bilion kwa mwaka,walipakodi wa Marekani wametumia zaidi ya $1 trilion kupambana na madawa ya kulevya yanayoingizwa na shirika lao la kijasusi!,ni kweli kuna kupambana na madawa ya kulevya au wanapambana na jamii ya watu weusi ili tu waende Magerezani kuwazalishia?

Ni kwanini asilimia kubwa ya wanaofungwa kwa Kesi hizo ni Watu weusi??!

Nawasilisha nimeshindwa kuweka link ila nitajitahidi niziweke
 
Huwa najiuliza,watu weusi tumeukosea nini ulimwengu huu?majibu mengi napata lakini swali bado linaendelea kubaki kichwani!
 
Sasa kama vibaka, shoplifting, ukahaba, uuaji, cocaine, bangi etc mnaoongoza kwa maasi hayo yote ni weusi kwa nini msifungwe hali mkijua in America nobody is above the law?
 
ni utumwa tu hakuna chochote hapo kwanini wao wanafanya biashara hizo lakini haoni wakifungwa wanatuonea tu sisi watu weusi laikini Mungu yuko atawafichua na wao pia
Sasa kama vibaka, shoplifting, ukahaba, uuaji, cocaine, bangi etc mnaoongoza kwa maasi hayo yote ni weusi kwa nini msifungwe hali mkijua in America nobody is above the law?
 
Sasa kama vibaka, shoplifting, ukahaba, uuaji, cocaine, bangi etc mnaoongoza kwa maasi hayo yote ni weusi kwa nini msifungwe hali mkijua in America nobody is above the law?

wazungu vibaka pia wapo,vivyo hvyo kwa changudoa na drug users,sema wao wana akili nyingi wanafahamu kukwepa mkono wa sheria,black people wao huwa wanafanya uhalifu then wanakamatwa kiurahisi
 
Ukiwa mtu mweusi Marekani una probability kubwa ya kwenda jela kuliko kufika college, katika kila watu weusi 9, mmoja yupo jela...bado unataka kuniambia ni coincidence? White people of Wall street are the biggest users of illegal drugs in the world lkn hawaguswi, mateja weusi ndo wanaofungwa kwa kupewa double digit sentences. The Amerucan correction system is there to ensure availability of cheap labour in the capitalist syatem. Period!
 
Back
Top Bottom