Tom Tanzania
New Member
- Sep 12, 2022
- 2
- 6
ELIMU ni suala mtambuka lisilotenganishwa na AJIRA au KUJIAJIRI (Biashara). Hivyo suala la ELIMU linapaswa kutazamwa upya kama uwekezaji usasa ambao ni sharti ulete mafanikio kwenye jamii husika.
Mfumo wa kutoa bidhaa pendwa za MUDA,PESA na USALAMA wa muhusika kwa lengo la kujizolea ujuzi na maarifa ya kuleta mabadiliko ya kijamii,kiuchumi n.k.Kwa wastani kijana mwenye shahada ya chuo kikuu anawekeza muda usiopungua miaka 16.
MSAFIRI WA SHAHADA na maarifa ya kijamii huanza uwekezaji wa rasiliamali pesa siku tu linapopatikana wazo la kuandikishwa shule,kupitia yeye wazazi/walezi wake wanaanza kukatwa tozo za kumgharamia masomo yake kwenye ada,usafiri,umeme,maji,kodi za nyumba,vitendea kazi,chakula n.k hata walezi wasibaki na umiliki wa chochote ila lengo la Elimu litimie
Wakati Serikali na wadau binafsi wanaotoa huduma wanajiinua kupitia uwekezaji wa MSAFIRI WA SHAHADA ili kujipatia maarifa na ujuzi akakomboe jamii.
MHITIMU anapaswa kuvikwa taji la Ushindi kwa heshima na bashasha tele baada ya kushinda vita dhidi ya Adui UJINGA ama kwa kurahisishiwa mazingira ya KUJIAJIRI au KUAJIRIWA. Hii ni motisha kwa WAZAZI/WALEZI wapate matunda ya uwekezaji wa kijana wao kupitia pato lake, Motisha kwa mhitimu na familia yake kufurahia mbivu za uwekezaji wa muda na nafsi yake.
Ushindi kwa jamii kwa kuziishi mbivu za maarifa yatokanayo na elimu ya MSAFIRI,Na Faida kwa Serikali kwa kujihakikishia makusanyo chungu mzima ya kodi,tozo na michango mingine kutoka kwa muhusika kupelekea maendeleo ya kijamii.
Hakuna safari isiyo na magumu, lakini safari ya KUINGIA kwenye AJIRA/KUJIAJIRI na KUZIISHI AJIRA/BIASHARA imekua ni ya kukatisha TAMAA. Zama za kutia shaka katika juhudi za kuwaendeleza kiuchumi WAAJIRIWA ( Wafanyakazi) na WALIOJIAJIRI (Wafanyabiashara) kwa UTANASHATI tatanishi.
UKATILI TANASHATI; Kuna vikwazo vya UMRI wa kupata AJIRA, UKATILI tanashati kwa jina la VIGEZO. Kijana anahitimu mwaka 2015 akiwa na miaka 25,kazi hazitangazwi miaka 5 mfulululizo, mwaka 2022 zinatangazwa akiwa na miaka 30 anahitajika kijana mwenye umri chini ya 30. KIJANA ananyimwa haki yake ya kuomba AJIRA kwa kivuli cha msamiati KIGEZO. Mamlaka zinapaswa kutambua sio UZEMBE wa MHITIMU kufikisha miaka 30 hajajua cha kufanya bali ni zao la mifumo hivyo kumpa kipaumbele MHITIMU wa kale kwa kuvumilia miaka 5 bila kupewa hitaji lake la msingi ni jambo la KUJIVUNIA.
UCHONGANISHI TANASHATI; Kikwazo CHONGANISHI kwa jina la TOZO tishio la WANANCHI kuingia kwenye ulimwengu wa KUJIAJIRI na Kuishi kwenye AJIRA kwa waliokwisha jiajiri/ajiriwa. Ni busara kwa mamlaka kuepuka haraka mfumo huo wa unyang’anyi wa kipato cha wananchi wao wakikiita TOZO kwani hupelekea kufa kwa biashara/mitaji yao hasa pale makusanyo /makato ya tozo yanapofanyika bila kuzingatia mzunguko wa kipato cha mhusika.
Ni vema Mamlaka zidhibiti mfumo wa kuwachonganisha WANANCHI na mamlaka zao kwa kuonekana wanapinga MAELEKEZO YA SERIKALI hali ya kuwa wanatetea mazingira nafuu na WEZESHI kiuchumi.
Bali kuwapa kipaumbele kwa kuwasikiliza sababu za kupinga na madhara chanya ya kuepuka mifumo hiyo inayolalamikiwa ili kujiridhisha njia waipitayo ina usahihi kwa kiasi gani kufikia lengo la maendeleo ya kijamii na kiuchumi kama Taifa.
Aidha ni busara mamlaka husika kutambua kioo huonesha taswira ya kilicho mbele yake, basi serikali ni kioo, kila ikiwekacho mbele huonwa na jamii, endapo itaweka lililo jema basi jamii italiona na kulishika. Hakuna shaka kila mwenye uzalendo yu pamoja na wengi kuhakikisha yaliyo mema yanakuwa juu ya wote.
UTAPELI TANASHSATI; Hata hivyo ni wengi tu wanaoamini uongozi ni kipaji, la hasha si kipaji cha ufundi wa maneno yenye kuwatukuza watu hali ya kuwa hawapati kinachostahili, mamlaka zitambue doa la sanaa ya maneno juu ya hesabu za haki kwa watu wake. Ajira ni biashara, muajiriwa anawekeza nguvu/ujuzi/muda na hata nafsi yake kwa lengo la kupata ujira, UTAPELI TANASHATI wa kipato cha watu wa kuwapa nyiongeza ndogo ya mshahara kulinganisha na kiwango cha ongezeko la kodi/makato mbalimbali katika jamii zetu.
Ni lazima hesabu za haki zihusishwe kwa masilahi ya wenye haki.Si halali kuongezwa ASILIMIA ambazo ni pungufu ya TOZO/KODI zilizoongezeka katika mzunguko wa kifedha/kiuchumi kwa maana ni kuwaongeza kwa namna ya kuwapunguzia kipato chao.
Maarifa ni chanzo cha ustawi,ndio maana kuajiriwa au kujiajiri kuna hitaji taaluma/maarifa ya jambo husika ama kwa kujifunza, kuona, kulifanya au kuelekezwa.Taifa limewapa mamlaka wenye kustahili Uongozi .Maarifa hayatenganishwi na Uongozi, kwa kuwa uongozi ni DHAMANA, wala si dhamana ya kula mema ya nchi, ama dhamana ya kuzuru nchi na dunia pasipo lengo liwafaalo watu wa Taifa husika,au ukuu wa kutoa matamko na maamuzi bila ya kujali madhara yake, bali ni KIBALI cha kupima weledi wa mwenye mamlaka katika kuongoza na kutatua matatizo ya jamii husika.
USALITI TANASHATI;Sanaa katika utatuzi wa matatizo ni FUMBO kwa wengi ,Ama kwa UFUNDI wa kutengeneza tatizo kwa namna inayoonekana kama MSAADA au UJUZI wa kutengeneza matatizo kwa lengo la kuyatatua baadae ili kujipatia MTAJI wa kisiasa au KIUTAWALA.
Huu ni USALITI TANASHATI, kutoa maamuzi yanayoweza kuathiri biashara na ujira wa watu bila kushirikisha au kuwasilikilza jamii kwa ukaribu zaidi, kutoa maamuzi ambayo tangu yatangazwa TAIFA linalalama kuhusu madhara yake, baada ya kuona madhara yake unayaondoa ikiwa tayari wengi wameethiriwa na mfumo.
Ni vema kuwe na ushirikishwaji madhubuti wa jamii za waajiriwa na wafanyabiashara ili kulinda masilahi yao ambayo ni msingi wa maendeleo ya uchumi wa TAIFA.
MAJIVUNO TANASHATI,sio ufahari TAIFA kujisifia uwezo wa kuongeza bajeti ya kuwakopesha wanufaika wa ELIMU YA JUU pasipo kuwa na juhudi za kuhakikisha mbinu na uwezo wa pesa hizo kurejeshwa. Taifa lina idadi kubwa ya WASOMI waliosoma kwa pesa za serikali na hawana uwezo wa KUZILIPA/KUREJESHA mikopo hiyo kwa kuwa hawamudu kujiajiri au hawajaajiriwa. Ni muhimu kuona madhara ya kiasi kinachopotea kwa kutozingatia suala la AJIRA/KUJIAJIRI kwa walionufaika na uwekezaji husika.
HASARA TANASHATI;Vita ya maendeleo ni mapigano yanayopiganwa kwa ushirikiano wa jamii zote,kila baya huja na madhara. HASARA TANASHATI ambayo ni tishio kwa kodi za raia wema na wazalendo.
Kama Taifa linakusanya kodi nyingi ili lijenge taasisi mbalimbali za kutoa huduma, linanunua rasilimali vitu na kulipa railimali watu ili kuwezesha kutolewa kwa huduma husika, linakusanya PESA kwa wapokea huduma kwa jina la ADA ili kuwapa hitaji tarajiwa.
Kwa tafsiri nyepesi MAMLAKA hizi zinafanya biashara wakati wa kutoa huduma. Basi ni SHARTI Taifa lizingatie uwekezaji huo wa pesa za wananchi unatoa matunda kwa waliochangia kodi au waliolipia ada kupata kile walichokilipia wahusika.
Lazima kuwe na takwimu za wasomi wetu na waajiriwa wetu wana mchango gani kupelekea kuhakikisha taasisi hizi zitaendelea kusimamia utolewaji wa huduma.
Maendeleo ni Watu ,Watu ni Kipato,Kipato ni Ajira na Biashara.

Upvote
1