Biashara ya Barakoa na Sanitizer ni kilio tu sasa hivi

Biashara ya Barakoa na Sanitizer ni kilio tu sasa hivi

Wakuu Salaam;

Hii kazi ya barakoa na sanitizer imekua kilio tu saivi. Mwanzoni mambo yalikua safi, ukilala ukiamka hela hii hapa, ni tofauti na sasa hivi.

Serikali ingetoa updates za maambukizi ya Corona mara 2 au 3 hivi yenye peak nzuri tu mzigo najua ungeisha maana kipindi cha nyuma kila ikitangaza tu, mauzo na faida ni kemkem.

Sasa hivi ni kilio tu. Nilichukua barakoa 2 niwape rafiki zangu hawakupokea, wakadai wanakereka kuzivaa. Nilichoka.

Kuna hasara inataka kuninyemelea nikiona mchana kweupe. Sasa hii hasara inatakiwa kupita mbali.

Wito wangu umeshaeleweka.
Kwa wafanyabiashara wazoefu hilo wala sio jambo la kushangaza
 
Kuna jamaa nilikaa naye karibu kwenye daladala, yale mafua yanavyombana na kukohoa nikajua korona hii ikabidi nihame siti nisogee mbele, baada ya muda nikamwona na jamaa ambaye naye alikuwa jirani yake akihamia siti ya mbele. Wabongo ni wepesi sana kupuuzia tahadhari, saa hizi unawakuta wapo kibao wanazurura na kupanda daladala bila barakoa. Nilichogundua ni tatizo la elimu ndogo hasa uswahilini, IQ ziko chini sana......ndo maana lowasa kwenye kampeni kipindi kile aliweka vipaumbele vyake namna hii, 1. Elimu 2. Elimu. 3. Elimu.....ndo sasa naanza kumwelewa.
 
Back
Top Bottom