Biashara ya Barakoa na Sanitizer ni kilio tu sasa hivi

Kwa wafanyabiashara wazoefu hilo wala sio jambo la kushangaza
 
Kuna jamaa nilikaa naye karibu kwenye daladala, yale mafua yanavyombana na kukohoa nikajua korona hii ikabidi nihame siti nisogee mbele, baada ya muda nikamwona na jamaa ambaye naye alikuwa jirani yake akihamia siti ya mbele. Wabongo ni wepesi sana kupuuzia tahadhari, saa hizi unawakuta wapo kibao wanazurura na kupanda daladala bila barakoa. Nilichogundua ni tatizo la elimu ndogo hasa uswahilini, IQ ziko chini sana......ndo maana lowasa kwenye kampeni kipindi kile aliweka vipaumbele vyake namna hii, 1. Elimu 2. Elimu. 3. Elimu.....ndo sasa naanza kumwelewa.
 
Ushauri tafuta ofisi karibu na Chuo utapiga ela mpaka ukimbie, nishukuru baadae baada ya kupiga hela wanavyofungua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…