Ushauri wangu Ni huu;
Niliwahi kumiliki bodaboda mwaka Jana,wiki ya kwanza alinipa vizuri 70k yangu,wiki ya pili vikaanza visingizio,Mara juzi nilikuwa naumwa mafua kwa hiyo bosi utanidai nakuongezea katika hesabu ya wiki hi. Unamkubalia Cha ajabu na hiyo wiki analeta visingizio tena,deni linazaa deni.
Haujapita mwezi Kuna mtu anakuja kuniambia "pikipiki yako nimeona Kuna madogo Kama watano wamepakizana wameipiga mtungo huo mwendo Kama ngiri anawahi shimoni. Jamaa nampigia anasema anaumwa kifua kampa mshikaji wake amletee hela. Miezi mitatu pikipiki imechakaa. Kwa kuona aibu maaana alinifuata mwenyewe nimnunulie bodaboda Hali tete mtaani,akaanza visingizio kibao anataka tuvunje mkataba,nikamuuliza Sasa wewe ndiye uliniambia maisha magumu nikununulie boda angalau upate hela ya kula na kijiwe ulisema unacho maana ulikuwa unapiga day worker boda za wanao,akajibu bosi me naona Kama Nina gundu maana chombo kinaharibika,madeni mengi,bodaboda zimekuwa nyingi kijiweni,hell hakuna. Akaniambia namleta ndugu yangu umkabidhi. Wiki ya kwanza huyo ndugu yake kavunja side mirror.
Ni mfano tu ndugu,na to make story short niliiuza kwa Bei ya hasara. Ila Kama umeipenda hii biashara Kuna ambao inawalipa,na nilichojifunza Ni kwamba ukinumua bodaboda usimpe kijana asiye na majukumu, au hawa wanyoa viduku na wasikiliza singeli...Mpe pikipiki yako mtu mzima mwenye familia aliyekomaa akili. Ataifanya kazi kwa bidii na nidhamu maana ndiyo itamfanya apeleke mboga na unga nyumbani. Mimi nilifeli katika hiko kipengere.
Kuhusu duka tatizo linaweza lisiwe mtaji. Una mtaji mkubwa sana. Kuna watu wanaanza na Duka na mtaji wa chini ya milioni mbili na wanatoboa. Kitu Cha kuzingatia ni location. Jamaangu niliyesoma nae ambae amefanikiwa kwenye biashara ya viatu alinipa ushauri kwamba usione watu wanalipia fremu Hadi milioni ukawaona hawana akili,location Ni mtaji mkubwa kwenye biashara kuliko pesa,Kuna sehemu unakutana na fremu nzuri lakini hazina watu,ukiingia kichwakichwa na milioni kumi yako utalia kilio Cha mbwa. Fanya utafiti katika Hilo eneo utakuja kunishukuru.