Biashara ya bucha la samaki hai kabisa

shule e

Member
Joined
Oct 19, 2016
Posts
28
Reaction score
23
Habari, niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuna hili wazo la kibiashara la kuuza samaki angali bado hai, kama wafanyavyo China, kwamba unaenda fish market unanunua samaki fresh kabisa kwenye maji yake .

Je kuna faida na hasara gani ya hii biashara?
 
Ndugu yangu wewe kama umeiona fursa endelea, siku ukija kutahamaki utakuta hiyo fursa watu walishaanza kitambo na wanapiga hela.kiukweli hiyo biashara kwa tz ni mpya nakushauri kama una hela anzisha pale Dodoma aquarium utapiga hela mbaya Mimi mwenyewe hilo wazo lipo sema nakosa mtaji tu.
Habari, niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuna hili wazo la kibiashara la kuuza samaki angali bado hai, kama wafanyavyo China, kwamba unaenda fish market unanunua samaki fresh kabisa kwenye maji yake .

Je kuna faida na hasara gani ya hii biashara?
 
Habari, niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuna hili wazo la kibiashara la kuuza samaki angali bado hai, kama wafanyavyo China, kwamba unaenda fish market unanunua samaki fresh kabisa kwenye maji yake .

Je kuna faida na hasara gani ya hii biashara?
Hiyo biashara inabidi uwe na bwawa kabisa la kufugia au boti na nyenzo za kuwatoa hai huko baharini/mtoni maana ukitegemea wavuvi unaletewa samaki mfu .
 
Habari, niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuna hili wazo la kibiashara la kuuza samaki angali bado hai, kama wafanyavyo China, kwamba unaenda fish market unanunua samaki fresh kabisa kwenye maji yake .

Je kuna faida na hasara gani ya hii biashara?
Faida au Hasara ni baada ya formula ifuatayo:-

Faida au Hasara = Kipato(mauzo) minus gharama za uendeshaji

Sasa bila kujua hao samaki utawapata wapi, kwa bei gani utawauzaje, na gharama za sehemu umeme n.k. pia wanunuzi kama wapo kuweza kumaliza mzigo na kwa bei unayotaka wewe..., kwakweli itakuwa ni sawa na kupiga ramli....

Kama market segment yako ni yenye watu wenye kipato na kwao sio tatizo kulipia premium products utapata ila kama watu hata kununua dagaa wana-bargain hii kwao itakuwa ni anasa..
 
Kuna Bar ipo Ununio, jamaa ana bwawa ukitaka samaki (sato) anakuvulia mzima mzima.
Ni wazo zuri, kama una hela na eneo unaweza kufanya ila kumbuka
1. Gharama ya bwawa
2. Gharama ya kusafirisha samaki ( maana kuanza kuwafuga wakiwa wadogo sio viable)
3. Gharama ya chakula kwa samaki
4. Gharama ya mtunzaji wa hao samaki

Swali: je baada ya kuondoa gharama zote hizo bado utakuwa na faida kwa biashara yako?!
 
Kuhusu bwawa tiyari ninalo na samaki wapo wana miezi 4 sasa bado miezi 2 waende sokoni sema nimeona nitafute jinsi ya kujitofautisha na wauzaji wengine .
 
Shukrani mkuu
 
Shukrani mkuu
 
Inawezekana sana na utapata wateja kadha wa kadha, zingatia muda wa hao kuanza kuvuliwa ili wasikupe garama kubwa.
 
Habari, niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuna hili wazo la kibiashara la kuuza samaki angali bado hai, kama wafanyavyo China, kwamba unaenda fish market unanunua samaki fresh kabisa kwenye maji yake .

Je kuna faida na hasara gani ya hii biashara?
Nb. Samaki ninao wapo bwawani tiyari.
 
Anzisha biashara faida na hasara baadae
Hiyo biashara kwa Tanzania itabuma .Ukienda nchi za Lesotho,Swaziland Botswana kwenye bucha unakuta watu wananunua wanajichomea wenyewe kwenye majiko hapo hapo buchani.Tanzania hupati mtu.Watanzania ghatama za kufuata hao samaki hawako tayari kugharimia mtu anaona heri anunue Marehemu samaki bucha ya samaki jirani.Culture ya customer ni kitu muhimu kuangalia.Hiyo biashara utashindwa.Ni Kama unavyoona supermakert nyingi Tanzania zinakufa sababu watanzania hawana supermakert culture Kama Wakenya.Mtanzania kujenga ujirani atanunua nyanya ,nk genge la jirani au sokoni hanunui supermakert .Mtanzania culture Yake kula samaki Marehemu ndio anapenda huyo hai wako Wala Sio motivation kwake ya kuchoma mafuta kupanda daladala au bodaboda kuwafuata huko waliko
 
Yaonyesha ni biashara ya kipekee na ngeni kabisa. Mteja anakuja na beseni la maji kabisa ili amfikishe home akiwa hai? au akishachagua unammalizia wewe?. Kwa china ufugaji wa samaki wako mbele na labda wateja wanao wa kununua hai, fanya utafiti kwanza mkuu
 
Mimi nilianzisha hiyo bucha ya samaki hai. Wateja / watu wakifika wanaanza kukuuliza maswali juu ya samaki hao: chakula, dawa, matunzo etc na kuendelea kushangaa shangaa halafu wanatoka; wanaenda sokoni kununua samaki mfu. Ya kwangu ilikuwa kama banda la maonesho. Nakushauri uanzishe ili uone uzoefu utakuwaje huko kwako.
 
Nadhani Ile bar inaitwa songambele kama sikosei....nilishawahi kaa one time miaka kama 3/4 iliyopita sijui kama papo bado!?
 
Mteja akishachagua anatengenezewa tu kama kawaida
 
Ni bei ilikua kubwa kidogo tofauti na wengine au sababu ilikua ni nini mkuu.

Mm ninavyoona bei iwe ya kawaida tu kama za wale wanaokaa kwenye friji .
 
Mteja akishachagua anatengenezewa tu kama kawaida
Mkuu inaweza kuwa biashara nzuri sana kama itakuwa viable. Kwa sisi tuliokulia ziwani na sasa tuko mijini huku hiyo nitaweza kuwa mteja kabisa. Yaani samaki unamla mpaka unakaa chini kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…