Biashara ya Cable TV

Biashara ya Cable TV

KANYEGELO

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,238
Reaction score
4,885
Wakuu habarini,

Poleni na michakato ya weekend samahani naomba kwa aliye na muongozo wa kufungua biashara ya cable anipe muongozo.

Nafikiria sana kufungua biashara ya kusuply cable tv

Katika majumba ya watu....nimefanya utafiti wa eneo mahitaji nimeona uhitaji ni mkubwa kuna watu hawananuwezo wa kununua vingamuzi

Kuhusu ufundi na istalation za madish nipo vizuri kwa hilo sina tatitizo...kabisa

1.Anayefahamu lessen TCRA sh ngapi wanalipia anijuze kwa huduma hiyo

2.Anayefahamu (transmiter kable TV) zinauzwa wapi na kiasi gani pia nitashukuru! Ili niweke katika mpango wa biashara hiyo au kama mtu anajua kutengeneza aje ani P.m nipe tenda hiyo ya kunitengezea

Mwisho natanguliza !! Shukran za dhati kwa maoni na michango yenu

sent from HUAWEI
 
Mkuu yaani una maanisha unataka kuanzisha "Mohamed Cable" yako?
Yaani "kanyegelo cable".
If so, wazo zuri sana.
Kila la kheri umewaza mbali.
 
Mkuu wachawi wako wa hiyo biashara watakuwa ni Azamu na Dstv labda kama uta sambaza baadhi ya channels tu ila ukisambaza za kuonyesha ligi ya bongo Azamu utawa kuta mlangoni kwako na kama ukiweka na ligi ya England napo Dstv utawakuta mlangoni kwako hata kama channels zako sio za superspots watakwambia wao ndiyo wana hatimiliki kwa Tz....

Hapo ukitaka we kwenye cable tv yako weka channels zako zote za FTA za bongo na za nje za movie na music ila napo wadau wengi kwenye cable wanataka ligi pendwa hapo juu ambapo ukiziweka tu hizo channels ndiyo vita inapo anzia.
 
Mkuu wachawi wako wa hiyo biashara watakuwa ni Azamu na Dstv labda kama uta sambaza baadhi ya channels tu ila ukisambaza za kuonyesha ligi ya bongo Azamu utawa kuta mlangoni kwako na kama ukiweka na ligi ya England napo Dstv utawakuta mlangoni kwako hata kama channels zako sio za superspots watakwambia wao ndiyo wana hatimiliki kwa Tz....hapo ukitaka we kwenye cable tv yako weka channels zako zote za FTA za bongo na za nje za movie na music ila napo wadau wengi kwenye cable wanataka ligi pendwa hapo juu ambapo ukiziweka tu hizo channels ndiyo vita inapo anzia.
Hii biashara ilishamiri sana kanda ya ziwa yaani wakati Dar wanahangaika na kuzunguusha antena mikoa mingine wao walikuwa wanapeta tu, ving'amuzi vya star times ndio vilikuja kuharibu deal kutokana na teknolojia ilionekana rahisi kwa kutumia antenna ya ndani.

Kuna miaka maeneo mengine ya mkoa wa Kagera ilikuwa wanapeta tu na DSTV kutokana na kipindi kile ofisi za DSTV kuwa miji mikubwa tu na maeneo mengine ya mipakani wanahudumiwa kupitia nje ya nchi
 
  • Thanks
Reactions: 7ve
Hii biashara ilishamiri sana kanda ya ziwa yaani wakati Dar wanahangaika na kuzunguusha antena mikoa mingine wao walikuwa wanapeta tu, ving'amuzi vya star times ndio vilikuja kuharibu deal kutokana na teknolojia ilionekana rahisi kwa kutumia antenna ya ndani. Kuna miaka maeneo mengine ya mkoa wa Kagera ilikuwa wanapeta tu na DSTV kutokana na kipindi kile ofisi za DSTV kuwa miji mikubwa tu na maeneo mengine ya mipakani wanahudumiwa kupitia nje ya nchi
Yeah sure kuna kipind nilikuwa mkoani huko jamaa alikuwa ana sambaza huduma ya cable tv na ana kupa na digital cable box so hiyo hakuna tofauti na mtu mwenye dish kitu kinakuwa ni clear hakuna chenga na ni mwendo wa HD tu hapo tulikuwa tuna chek ligi zote kubwa mpaka UEFA na channels zote za movie zile HBO sijui SONY Pix na zingne nyingi tu halafu kwa mwezi mna toa elfu kumi tu wakat ingekuwa Dstv ni premium laki na shingap huko ila wajomba wa Dstv wakitimba mkoani jamaa ina bidi azi switch off zile channels zote za mpira mpaka waondoke na jamaa walikuwa wanakuja kwenye msimu wa UEFA walikuwa wana niboa.
 
Mkuu wachawi wako wa hiyo biashara watakuwa ni Azamu na Dstv labda kama uta sambaza baadhi ya channels tu ila ukisambaza za kuonyesha ligi ya bongo Azamu utawa kuta mlangoni kwako na kama ukiweka na ligi ya England napo Dstv utawakuta mlangoni kwako hata kama channels zako sio za superspots watakwambia wao ndiyo wana hatimiliki kwa Tz....hapo ukitaka we kwenye cable tv yako weka channels zako zote za FTA za bongo na za nje za movie na music ila napo wadau wengi kwenye cable wanataka ligi pendwa hapo juu ambapo ukiziweka tu hizo channels ndiyo vita inapo anzia.
Mkuu nimefanya tafiti za kutodha mfano ukiwa na alpha box hd decoder kwa satelite 52e unapata mipira yote ya UEFA,LALIGA,

Halafu pia dstv ...wanaruhusu channel zao kirishwa kwenye cable kwa hilo halina tatizo ...azamu ndio hairuhusiwi ni kosa la kisheria

Mbona ulaya kuna cable tv mpk leo zinafanya vizuri pamoja na kuwa na vingamuzi kikubwa ni ubora tu wa huduma yako na transmiter unayotumia

DSTV hawaruhusu wengi wenye cable tv wanatumia canal sports kuonyesha mpira

Sent from my SM-G950U using Tapatalk
 
Biashara ipo na inafanyika vizuri nipo mwanza mfano mwanza kuna barmedas,na mwanza satelite wamesambaza jiji zima wanapiga hela tu

sio wote wanauwezo na vingamuzi nafikiria hii itakuwa ni programu nzuri kwa wenye kipato cha chini

sent from HUAWEI
Kwa Mwanza labda uchague maeneo ya pembezoni, labda kwa kuanzia chagua eneo kama Buswelu maana Mwanza satelite na Barmeda hawajafika na sidhani kama wana mpango wa kufika, kwa siku za usoni unaweza ukatengeneza himaya yako huko
 
Mimi nimekulia kwenye matumizi ya cable tv. Mohammed cable tumetumia sana tangu niko awali mpaka form two sijui. Then kuna family member mmoja alikuwa na cable tv yake nilikuwa napenda kwenda likizoni.

Ile control room ina feni flani kubwa za kutosha lakini kuna joto balaa.
Nje kuna dish zaidi za kumi aina tofauti. Azam ndo walikuwa wakorofi mno ukionesha channel yao leo kesho wako ofisini. Movies mpya zikitoka tunawawekea raia.

Shida ya hii biashara ni vigumu kutambua mapato kama una wafanyakazi.
 
Kwanza nikupongeze kwa wazo lako zuri la kuanzisha biashara ya cable Tv. Wengi wasichojua ni kwamba hizi channel nyingi za muziki, movie, michezo kama ngumi na mieleka na documentary ni Free to air (FTA). Kikubwa ujue direction na satelaiti wanazorushia masafa yao. Za mpira nyingi ni za kulipia ingawa zipo za free pia. Biashara ya cable bado ipo ipo sana, wapo tanga Cable Tv, Upanga Dar zipo, Mwanza wapo barmedas, Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma wapo pia wasambazaji, Tabora mjini wapo akina Shashi, Mbeya alikuwepo Dhandho nk.

ANZA HIVI
1. Tafuta eneo zuri ambalo unaweza kuweka madishi mengi (20 ama zaidi) makubwa na madogo (KU na C band).
2. Nunua RF modulator kubwa (hii inasaidia kupanga frequency za channels mbalimbali kutoka kwenye disecqs switches.
3. Nunua heavy duty coaxial cable pamoja na trunk amplifiers (wanaita booster).
4. Nunua vingamuzi kadhaa hasa vinavyofungua encrypted channels kama vile Strong, Android box, canal sat na BeIn sports.
5. Malizia kwa kununua vifaa vidogo vidogo kadhaa kama rf splitter, pin na connectors.

ZINGATIA
1. Makaburu pamoja na lambalamba hawaruhusu channels zao kurushwa kwenye cable (zile zenye nembo zao kama vile sinema zetu, maisha magic nk).
2. Omba leseni halali za biashara kutoka TCRA na halmashauri ya mji ulipo ili ulipe kodi halali na kukuza uchumi wetu.
3. Vifaa karibia vyote nilivyotaja hapo juu unaweza kuvipata kule Kariakoo Dsm kwa bei nafuu sana

Nikutakie kila la kheri
Biashara ipo na inafanyika vizuri nipo mwanza mfano mwanza kuna barmedas,na mwanza satelite wamesambaza jiji zima wanapiga hela tu

sio wote wanauwezo na vingamuzi nafikiria hii itakuwa ni programu nzuri kwa wenye kipato cha chini

sent from HUAWEI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu samahani naweza kukuPM

Typed Using KIDOLE
 
Kwanza nikupongeze kwa wazo lako zuri la kuanzisha biashara ya cable Tv. Wengi wasichojua ni kwamba hizi channel nyingi za muziki, movie, michezo kama ngumi na mieleka na documentary ni Free to air (FTA). Kikubwa ujue direction na satelaiti wanazorushia masafa yao. Za mpira nyingi ni za kulipia ingawa zipo za free pia. Biashara ya cable bado ipo ipo sana, wapo tanga Cable Tv, Upanga Dar zipo, Mwanza wapo barmedas, Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma wapo pia wasambazaji, Tabora mjini wapo akina Shashi, Mbeya alikuwepo Dhandho nk.

ANZA HIVI
1. Tafuta eneo zuri ambalo unaweza kuweka madishi mengi (20 ama zaidi) makubwa na madogo (KU na C band).
2. Nunua RF modulator kubwa (hii inasaidia kupanga frequency za channels mbalimbali kutoka kwenye disecqs switches.
3. Nunua heavy duty coaxial cable pamoja na trunk amplifiers (wanaita booster).
4. Nunua vingamuzi kadhaa hasa vinavyofungua encrypted channels kama vile Strong, Android box, canal sat na BeIn sports.
5. Malizia kwa kununua vifaa vidogo vidogo kadhaa kama rf splitter, pin na connectors.

ZINGATIA
1. Makaburu pamoja na lambalamba hawaruhusu channels zao kurushwa kwenye cable (zile zenye nembo zao kama vile sinema zetu, maisha magic nk).
2. Omba leseni halali za biashara kutoka TCRA na halmashauri ya mji ulipo ili ulipe kodi halali na kukuza uchumi wetu.
3. Vifaa karibia vyote nilivyotaja hapo juu unaweza kuvipata kule Kariakoo Dsm kwa bei nafuu sana

Nikutakie kila la kheri

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana mkuuu

Mkuu vp! nasikia pia ukifungua ukumbi ukatumia ving'amuzi vyao kuonyesha mpira wanaleta usumbufu, ni kweli sio halali kurusha kwenye ukumbi, hata kama unakisimbuzi cha Azam au DSTV?
 
Mkuu nimefanya tafiti za kutodha mfano ukiwa na alpha box hd decoder kwa satelite 52e unapata mipira yote ya UEFA,LALIGA,

Halafu pia dstv ...wanaruhusu channel zao kirishwa kwenye cable kwa hilo halina tatizo ...azamu ndio hairuhusiwi ni kosa la kisheria

Mbona ulaya kuna cable tv mpk leo zinafanya vizuri pamoja na kuwa na vingamuzi kikubwa ni ubora tu wa huduma yako na transmiter unayotumia

sent from HUAWEI
Aliyekuambia dstv wanaruhusu channel zao kusambazwa kakudanganya acha kuokota habari toka vijiweni vitakupotosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom