Wadau mwezi wa saba mwaka huu nilikua katika harakati za kuanzisha biashara ya car wash. Kama kawaida yangu nikaanza kufanya research sehemu mbali mbali hasa humu JF na kwa watu mbali mbali ambao walishanza kufanya. Nilikua na hela ndogo Sana kama laki 7 hivi. Katika kuhangaika hapa na pale nikawa naona mijadala ambayo ilikua inaonyesha kwamba pesa nyingi sana inahitajika nikataka nikakata tamaa. Sasa nikaamua kutembea kimtaa mtaa nikaanza kutafuta kitu hasa vile vya muhimu kama vacum na pressure kwa kutafuta kwa watu (used) nilisota mpaka kama mwezi wa nane hivi nikapata vacum moja na pressure moja. Nikapata eneo la kawaida Sana pale madale saiz business iko poa Kwa vitu hivyo viwili tu. Sisemi kwamba kila mtu anaweza fanikiwa, kwa kufanya hivyo bila bora kujaribu kuliko kudhani kwamba unahitaji vitu vingi au pesa kubwa.
Mjini vitu vingi vinawezekana ila ni kukosa muunganiko na watu wenye uzoefu wa hivyo vitu.
Mjini vitu vingi vinawezekana ila ni kukosa muunganiko na watu wenye uzoefu wa hivyo vitu.