Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,355
- 14,408
Mkuu, Huyo jamaa yako wa Mbeya, hiyo Elfu 50 ni FAIDA au ni makusanyo ya jumla?
Mkuu hiyo ni makusanyo ya jumla,ambapo faida yake ni kati ya 20,000/- hadi 25,000/-,kwa siku ambayo ni sawa na 600,000/- hadi 750,000/-,kwa mwezi.hiyo ni kwa mwaka 2009.
Mkuu nimekusoma... Nashukuru sana
wewe graduate wa finance na banking unahitaji ushauri wa kufungua banda la chips kweli?
Mkuu naomba uniulizie bei ya hizo Mashine na lile Huko la gesi la kipikia chipsi na chapati
Mmmh sawaa
HellowNina mtaji wa laki 3 na nusu, wakati natafuta ajira nimeona nijiajiri niuze chips, vipi mtaji unatosha? Any idea ya how to make them in a way it suits me (kisomi)?
Ushauri wenu unahitajika.
mkuu rejea huu uzi kuanzia namba 1,kila kitu kimezungumziwa kwa kadir ya uzoefu wa wadau ktk hii biasharaHellow
mie pia nna wazo la kujihusisha na uuzaji wa chips....tafadhali naomba msaada ako
Ubarikiwe mkuu,umeleeza vizuri sanaa,na jamaa ana bonge la Idea aisee.Mtaji wa laki saba unatosha sana mkuu, kuna jamaa yangu yeye huwa anaanza na laki mbili tu, anachofanya anatafuta vijana wanaoaminika wa kitaa ambao hawana kazi, anatafuta location nzuri na kuilipia ,anawanunulia jiko na vikoro koro kibao, na mtaji wa kuanzia anawakabidhi kwa maandishi kwa sharti la kila siku wanamletea Tshs 10,000 tu.
Jamaa anapiga sana hela, na bahati nzuri hawa vijana nao huwa wanafurahia kazi maana jamaa huwa hawabani wala nini,na wanakula hapo hapo, wengi chipsi hizo hizo ndio msosi wao wa mchana, jioni ndio wanahangaika kula magetoni kwao, yeye anachotaka ni Tshs 10,000 yake daily na kazi isife, ukipata hata millioni kwa siku yeye hana habari ilimradi umpe mwekundu wake.
Ukiwa na nia nzuri tafuta location hasa maeneo ya vyuo au sehemu zenye muingiliano wa kibiashara au gesti nzuri ambayo kuna wazinzi wengi, utapiga sana hela.
Kwa uswahilini maneno ya Sinza, Mabibo NIT sokoni, Manzese barabara ya kutokea tiptop kuelekea Mabibo jeshini, Kigamboni chuo cha mwalimu Nyerere, Mabibo Hostel, Tabata yote, Kawe Ukwamani, Temeke sokoni, Kinondoni mwajuni, Kinondoni studio, Mikocheni maeneo ya Kisiwani pale yana biashara kubwa sana ya chipsi.
Nimeona pia watu wanaingia mpaka kwenye shule za msingi na sekondary wanatengeneza chipsi kavu kidogo za 200 wanazifunga, watoto wanakula sana, na kwa kuwa wanaofanya hivi wanaongezeka kila siku inaonekana mfumo huu wa mashuleni unalipa sana.
Mungu atakusimami,maana Umejitambua katika hatua ya awali saana.Thanx sana mkuu..nimejifunza kitu hapo.. Na nitakifanyia kazi..unajua napiga chuo mwaka wa pili huu so natafuta kitu cha kufanya ili kuepuka kuhangaika pindi nitakapohitimu maana ajira zenyewe tabu sana za kusubiria halafu ukiangalia kitu kinacho matter sana ni kipato na sio ajira so nitalifanyia kazi lakini pia unaweza kunipatia kitu kingine mbadala wa huo maana life popote cha msingi ni kupigana na changamoto za hapa na pale